CAF yatangaza makundi ya kuwania AFCON 2019, Tanzania kuivaa Uganda

CAF yatangaza makundi ya kuwania AFCON 2019, Tanzania kuivaa Uganda

Kwenye ranking ya FIFA ya mwezi huu jan 2017 uki google utaona Uganda ni ya 73, Cape Verde 79, Tanzania 156. Lesotho sikuangalia. Ina maana uganda na cape verde wanatuzidi sana kimpira.

Hata ukiangalia Tanzania imecheza mara ngapi katika fainali za CAF ukilinganisha na Uganda na Cape Verde utaona kuna ukweli wa ranking za FIFA.

Kwahiyo wandugu tuwe makini unapoandika kuhusu hawa washindani wetu. Msiwadharau sana.

Kwanza Uganda na Cape verde wameishawahi kutufunga na wakatutoa kwenye mashindano ya kimataifa.
 
Naunga mkono kabisa tangia nifuatilie historia hili ni kundi kwa Tanzania tukijipanga tunapita. Tusipopita hapa sijui nitumie lugha???? Kundi hili jamani ni nafasi. Pointi 9 nyumbani sare 2 ugenini saaafi hao kwenye luninga. Tusipopita hapo tuachane na soka na shrikisho lifutwe na tuwekeze kwenye mchezo wa bao na kubishana. Viwanja vya mpira virudishwe malls za biashara.
 
Unaijua Cape verde vizuri??
Kama tuliwatoa ulimi Nigeria, Cameroon, Bukinafaso Nk Cape Verde tutavaana nao tu. Hapo tujikaze kwa Uganda kwani anajua udhaifu kwetu. Hakika timu ikiandaliwa vizuri, tunapita hapo.
 
Naunga mkono kabisa tangia nifuatilie historia hili ni kundi kwa Tanzania tukijipanga tunapita. Tusipopita hapa sijui nitumie lugha???? Kundi hili jamani ni nafasi. Pointi 9 nyumbani sare 2 ugenini saaafi hao kwenye luninga. Tusipopita hapo tuachane na soka na shrikisho lifutwe na tuwekeze kwenye mchezo wa bao na kubishana. Viwanja vya mpira virudishwe malls za biashara.
sidhani kama tutakuja kupata kundi jepesi kama hili
 
Uganda&cape Verde visiki hivyo
timu ngumu zinafahamika lakini siyo hizo tukijipanga vizuri zote hizo tutazipiga hapa nyumbani sijui Mungu atupe nini jamani yaani hawajatupanga na waarabu,nigeria,cameroni wametupanga vilaza watupu came on taifa stars
 
Kimpira hili linaweza kuwa kundi gumu kuliko makundi yote aliyowahi kupangwa maana hujui hizo timu zimejipanga vipi mpira ni dakika tisini sio maneno maneno kama mlivyo zowea kuucheza magazetini na mdomoni kikubwa ni mipango endelevu kwa vijana
 
Hapo inavuka team moja au mbili?
Inapita moja labda wapili apate bahati ya best looser, na kwa mazingira yalivyo kama itatokea bahati kundi hili wakapita wawili basi ni uganda na verde
 
tanzania haiwezi kufuzu 2019.. naomba wote humu tuwepo hai na thread tuifufue...

simba, yanga na tff ndio wachawi wa soka letu..

ligi yetu mbovu mfano okwi kwetu ni bonge la mshambuliaji timu zinamgombea.....ila uganda anatokea benchiiii yaani bwege tu
 
Nilitamani tim letu lipangwe kati ya hawa!

Algeria,
Egypt,
Tunisia
Morocco
Nigeria
Congo
 
Tusipoenda Afcon 2019, basi TFF ivunjwe iundwe TSF ( Tanzani a Singeli Federation) ili tuendelee na mambo mengine. Ila tukikosa tushukuru pia, kwa mfano tupo Afcon halafu unacheza na Cameroon ambaye kapigwa bao 3 na Misri, hebu vuta picha
Kwani nini.
 
Yaani hamna waarabu hapo tushindwe kufuzu jaman tuache utani hapo hata kama kutakuwa na kubet nitaweka mzigo hata laki najua tutapita
 
Hahahaha Mkuu ndio kwanza wameanza..Morocco,egypt na libya bado hawajacheza


Utakumbuka maneno yangu haya

Algeria-Egypt final

Egypt bingwa..

Kila la heri egypt...
Tafadhal blaza nataka nitengeneze kibubu cha kuweka pesa niende hizo afcon 2019 nikamshuhudie samata hivi zitafanyika wap
 
Kwakweli sifahamu kamanda wangu..mimi na kibubu mbali muno...wapo wataalamu humu watakusaidia jibu...ahsante
Zitafanyika Cameroon tu hapo na kwa nauli ya basi ukianzia Tunduma au Kigoma ni laki moja na sabini tu mpaka younde....na kwa hapa uhamiaji tunatoa pasipoti ya muda mfupi kwa nchi za afrika ya kati kwa shilingi elfu 10000 tu......naamini utaenda Cameroon 2019
 
Tusivyojielewa tunaweza kushindwa kufuzu
 
Tusipoangalia vizuri nafasi yetu ya mkiani inatungoja
 
Back
Top Bottom