Hili swala ni mpaka ligi za nchi nyingne ziishe ndipo wale wanaoshika nafasi ya 11,12,13 na 14 ndipo wanajua kama wataanzia hatua ya awali au ya kwanza
Kwasbb ktk top10 ya CAF club rank kuna Vilabu kama Pyramids, Rs Berkane, Raja Casablanca wao hawana nafasi ya ushiriki ktk CAf klabu bingwa hvyo zile favour zao za kuanzia hatua ya kwanza zimechukuliwa na aliyeshika nafasi ya 11,12 na 13
Na kama Esperance asingekuwa bingwa nchini kwao basi angeenda kushiriki shirikisho na hvyo ile favour ya kuanzia round ya kwanza ingeenda kwa anayeshika nafasi ya 14 ktk CAF club rank ambae ni Simba
Lakn pamoja na hayo bado Simba kwa rank yake atapangiwa timu dhaifu dhaifu inayoshika nafasi za mbali huko,
ilhali Yanga kwakuwa anashika nafasi ya 74 basi ana uwezekano akapangiwa timu zinazoshika nafasi ya juu juu ktk CAF rank