CAF yatoa viwango vipya vya ubora wa klabu, Simba yaporomoka

CAF yatoa viwango vipya vya ubora wa klabu, Simba yaporomoka

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Viwango vipya vya ubora wa klabu za Afrika (CAF Clubs' Ranking) msimu wa 2026/27 vinaonyesha Simba SC ikiwa nafasi ya 11 kwa alama 38, huku Yanga SC ikishika nafasi ya 12 kwa alama 35.

Azam FC ipo nafasi ya 39 ikiwa na alama 5, wakati Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini inaongoza orodha kwa alama 73, ikifuatiwa na Al Ahly ya Misri yenye alama 66.

Heres how Africas clubs rank ahead of the 2026-27 #TotalEnergiesCAFCL & #TotalEnergiesCAFCC P.webp
 
Yaani kelele zote zile za sisi ndio tuko vizuri CAF kumbe gap limebaki la pointi tatu tu? Msimu huu ukiisha kazi mnayo.
 
Viwango vya CAF inaonekana na vya kihistoria zaidi kuliko hali halisi ya sasa..
Simba kuwa top 20 ni kuwapaka mafuta kwa Mgongo wa chupa washindi wa CRDB conf Cup 😂😂
 
Jamani simba alifika fainali shirikisho, akapanda point hadi 48, iweje awe na point 38!!!
 
Alivyo kua juu uliwahi kureta uzi hapa?
Kazi ni kipimo cha utu
 
CAF wanapendelea haiwezekani Simba iwe nafasi ya 11.

Itakuwa tunahujumiwa tu simba timu kubwa sana Afrika.
Hapo lazima marefa wamehusika. Na hapo itakuwa tu ksbb ya lile goli la Mwalimu tulilokataliwa Zanzibar. Na lazima GSM anahusika
 
Usajili wa Yanga msimu huu unaogopesha sana. Hizo pointi tatu zinaenda kufutwa msimu huu kupitia akina Shalulile na Toure.
 
Simba inaongozwa na machizi zaidi ni magori.
Nimekuja kugundua Lile lizee bure kabisa.

Lilikuwa linatembelea nyota ya Hanse poppe.
 
Back
Top Bottom