Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
By Luqman Maloto
RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha 2020-2021, imehitimisha awamu ya Dk John Magufuli. Ukaguzi ujao utaanza kummulika Rais Samia Suluhu Hassan.
Taifa lilitangaziwa kifo cha Magufuli Machi 17, 2021. Kipindi ambacho bajeti ya 2020-2021 ikiwa mwishoni mwa robo ya tatu ya utekelezwaji wake. Rais Samia alikula kiapo Machi 19, 2021, ikiwa ni chini ya mwezi mmoja kabla ya kuanza vikao vya Bunge la Bajeti la 2021-2022.
Ukipenda kuwa sahihi zaidi unaweza kusema kuwa hata bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2021-2022, ina vionjo vya awamu ya Dk Magufuli, maana Rais Samia aliingia madarakani ikiwa imeshaandaliwa kwa sehemu kubwa na ikielekea kusomwa bungeni.
Hutakuwa upande wa makosa endapo pia utasema bajeti ya 2021-2022 ni ya Samia peke yake japo iliandaliwa pakubwa na Magufuli kwa hoja kwamba ilitekelezwa kwa asilimia 100 na Samia.
Eneo ambalo hatupaswi kubishana ni kuwa bajeti 2020-2021, ambayo CAG Charles Kichere ameitolea ripoti ya ukaguzi hivi karibuni inahusu bajeti ya mwisho ya Dk Magufuli.
Sasa, tuwe kwenye ukurasa mmoja kuwa ripoti ya CAG Kichere ya hivi karibuni inasema hali halisi ambayo Dk Magufuli ameondoka nayo na inajenga picha ya kazi ambayo Rais Samia anapaswa kuifanya.
Angalau tunaelewana kuwa Magufuli aliacha deni la Serikali likiwa limefika Sh64.5 trilioni. Hiyo ni kwa mujibu wa ukaguzi wa hesabu za Serikali mpaka Juni 30,2021.
Jambo baya katika ripoti ya CAG Kichere ni kuwa karibu kila sehemu kuna madudu. Tafsiri ya moja kwa moja ni kwamba Rais Samia ana kazi kubwa ya kufanya. Anapaswa kuchukua hatua haraka.
Yupo mtu anaweza kujiuliza; kama kila sehemu kumekuwa na udhaifu mkubwa wa usimamizi wa fedha za serikali, kuanzia mapato, mikopo hadi matumizi, mifumo ilikuwa wapi?
Atakayesema mifumo iliharibika atakuwa sahihi. Hata hivyo, mifumo inaratibiwa na watu. Na hao ndio ambao Rais Samia anapaswa kuwashughulikia mara moja.
Mathalan, sasa hivi taifa linalia uhaba wa mafuta na kupanda kwa bei. Wakati huohuo, CAG ameripoti jinsi ambavyo kumekuwa na michezo ya mafuta. Udanganyifu ni mwingi.
Mafuta yanaingia Bandari ya Dar es Salaam. Yanalipiwa ushuru kidogo kwa hoja kuwa yanasafirishwa kwenda nje. Kwamba Tanzania ni njiani tu! Hata hivyo, ufuatiliaji unaonesha mafuta hayo hayakutoka nje ya mipaka kwa mwaka mzima. Mafuta hayo yaliyosomwa ujazo wake ni zaidi ya lita 2.6 milioni.
Hujakaa vizuri unasikia kuna watu walikusanya Sh18 bilioni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na kuzitumia juu kwa juu bila kuziwasilisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Ukiwa unawaza inawezekana vipi KIA mabilioni yatumike namna hiyo juu kwa juu, unasoma tena kuwa kuna taasisi za Serikali zilivunja sheria kwa kukusanya mapato Sh6.5 bilioni nje ya mfumo halali wa Malipo ya Serikali Kielektroniki (GePG).
Hapohapo kuna kituko cha aina yake. Sh2.4 trilioni zilisainiwa kama mkopo lakini fedha hizo hazijawahi kupokelewa. Maana yake, nyaraka zinaonesha kuna fedha zimekopwa na zinapaswa kulipwa lakini mkopo huo wa fedha hajawahi kuingia Hazina. Zimekwenda wapi? Kazi kwa Rais Samia!
CAG Kichere pia anatujuza kuwa Sh6.4 bilioni za Serikali zilitumiwa na taasisi 48 za Serikali bila kufuata utaratibu. Na kuna Sh2.6 bilioni zilitumika na matumizi yake hayakukaguliwa. Na kwa mujibu wa Kanuni ya Fedha ya mwaka 2001, fedha ambayo haikukaguliwa hiyo ni hasara ya Serikali.
Unaambiwa pia kuwa Serikali ilifanya malipo ya Sh6.2 bilioni nje ya bajeti. Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, inaelekeza matumizi ya Serikali kuendana na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge. Sh6.2 bilioni zikatumika kinyume na sheria. Kwa nini? Rais Samia ana kazi kubwa.
Ni kwa sababu kila eneo limetiwa dosari. Tanroads kuna shida, Wakala wa Majengo (TBA) hapako salama. Hapohapo anabainisha kuwa kasoro za matumizi ni kubwa kuanzia bajeti ya 2016-2017, inaendelea hivyo mpaka 2020-2021.
Bandarini kuna magari zaidi ya 600 yaliingizwa na kutolewa maelezo kuwa yanapelekwa nje ya mipaka. Hata hivyo, hayaonekani yakivushwa kwenye mpaka wowote. Maana yake yametumika ndani.
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) upo uozo wa kushangaza, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuna udhaifu wa hali ya juu, kisha unasimuliwa kuwa Bandari ya Tanga, yupo mjanja kapiga cha juu zaidi ya Sh130 bilioni katika mradi wa upanuzi wa bandari uliolipwa na Serikali zaidi ya bilioni 170. Mkandarasi aliyetekeleza mradi alilipwa Sh40 bilioni tu.
Wizara ya Mambo ya Nje, kuna upigaji wa Sh33 bilioni kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Addis Ababa, Ehiopia. Jengo la Tanzania, New York, wajanja wanalifanyia biashara taifa limelala. Kuna mchezo mkubwa wa kucheza na fedha za visa katika balozi za Tanzania.
Benki Kuu, kuna wajanja wamefanya uhuni wa kukata noti za Sh10,000 na kuunganisha na makaratasi kisha kuzisajili kama noti chakavu. Kwa udanganyifu huo Serikali imepata hasara ya Sh4 bilioni, ambazo zililipwa kama mbadala wa noti chakavu.
Kuna mengi, lakini hiyo ndio hali halisi ya bajeti ya mwisho ya Dk Magufuli. CAG Kichere ametoa mapendekezo mengi. Muhimu zaidi ni Rais Samia kuchambua na kufanya uamuzi ili makosa yaliyojitokeza yasirudiwe katika bajeti zijazo chini ya uongozi wake.
Wapo watu, pengine kwa kutojua, wanasema haya madudu ni ya kipindi cha Rais Samia. Tena wanasisitiza kuwa baada ya Dk Magufuli uozo umeibuka upya. Hapana, madudu haya ni ya mwaka wa mwisho wa Dk Magufuli. Kuhusu Samia, tuvute subira, tumsubiri Aprili mwakani, tutakaposomewa ripoti ya 2021-2022.
Ndimi Luqman MALOTO