mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Mh CAG Assad Mungu ampe maisha marefu sana,aliweka wazi kuwa bunge ni dhaifu halafu kuna watu wakaja juu na kumuondoa. Ule udhaifu aliousema ni huu uliotufikisha hapa leo. KATIBA imeweka wazi kazi ya bunge ni KUSIMAMIA na KUISHAURI serikali. Hii kazi ya KUSIFU tu wameitoa wapi?
Tulijiuliza mbona enzi za mwalimu watu hawakusimama kujiita wazalendo? Wakati huu mtu akisimama anajiita Mzalendo
Tofauti ni kwamba wazalendo wa Nyerere walikuwa wanaitwa na watu kwa sababu ya matendo, Wazalendo wetu wanajiita ili kuficha UFISADI.
“Matumizi mabaya ya Ofisi” “Kuisababishia Serikali hasara” haya mambo si yanaingia kama Rushwa na Uhujumu uchumi?
Kuna namna Katiba yetu inatakiwa kubadilishwa. Kiongozi akiiba hela za nchi kama hivi anatakiwa azirudishe na kufutwa uongozi kabisa maana akiendelea kuwa kuongozi ataendelea kuiba tu. Jela ndo sehemu inawafaa baada ya kufilisiwa.
Mr mkiki
View attachment 1746824