CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

Mimi nashuhudiwa moyoni hata ile miradi ya'' Stigler gorge na SGR'' ni white elephants nyingine!
 
Kweli mambo yanaenda kasi sana.

Miaka 5 iliyopita nani alikuwa anawasilisha ripoti, Kichele au Prof Assad?
Mara zote CAG amekuwa akitoa taarifa ya hasara kwa ATCL, hakuna mwaka ambao CAG amewahi kusema kuwa wametengeneza faida.
Kuna tofauti kubwa Kati ya fedha za mauzo na hasara.
Hasara inatokana na vitu vingi,vijiwemo
1-Matumizi
2-Uchakavu.
Kwa mfano thamani ya ndege moja no Tshs 290,000,000 na uchakavu ni asilimia 10,kwa hiyo ndege moja gharama ya uchakavu ni Tshs 29,000,000
X
Hizo sio fedha ni uchakavu ambao unahesabiwa Kama gharama za matumizi kitaalamu.
 
Kwenye uwekezaji unaotumia mitaji mikubwa kama ndege hasa kwa shirika linalofufuliwa kama ilivyo Air Tanzania, ambalo liko kwenye maboresho na kulifufua upya, ni wazi hesabu zake zitaonekana kwenye hasara.

Hivi ninanyoandika kuna Airbus mbili mpya ziko kwenye hatua za mwisho mwisho kabla ya kuanza kuruka, hizi ukizipigia hesabu utakuta kuwa kila moja inagharimu Dollar 91 Million sawa na TZS 211 Billion. Pamoja na janga la COVID hiyo hasara ya Billion 60 kwa ATCL ni cha mtoto ukilinganisha na mashirika mengine ya ndege yaliyosimamisha huduma zake.

Kazi ieendelee na wabadhirifu wadhibitiwe tu.
 
Kuna Kenya airways, Ethiopia airways, Rwanda airways. Ili la kwetu ni uongozi mbovu na kukosa ubunifu!
Usifikiri hayo mashirika uliyotaja yanatengeneza faida na usidhani kwamba yanamilikiwa na serikali kwa asilimia mia, Kenya airways almost haijawahi kutengeneza profit, hata Quantas airways ya Australia katika statement yao ya hivi karibuni wamepata faida kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 9, na haya yote tulishatahadharisha kwamba serikali isijiingize kwenye biashara ya ndege kichwa kichwa...
 
Ripoti za Kimataifa zinaonesha Mashirika mengi ya ndege katika Afrika yamekuwa yakijiendesha kwa hasara sana.

Ripoti za CAG 2015/16 hasara ilikuwa bilioni 94.3, mwaka 2016/17 iliongezeka ikafikia bilioni 109.3 wakati mwaka 2017/18 iliongezeka na kuwa bilioni 113.

Hii ya bilioni 60 ni kama imepungua sana.
 
Hii midege imesababisha watumishi hawajapata ongezeko la mishahara kwa miaka 5 wakati sheria inaelekeza kufanya hivyo.
 
Sure
 
Upo sahihi, serikali ingeungua hisa kwenye mashirika ya ndege, Kama wanavyofanya S A A na Kenya airways.
 
Mama asaidie CAG akakague hata jezi zetu yanga ile bendera ya Afrika ni kama tulipigwa pale
 
Ukubwa wa pua siyo wingi wa kamasi
 
Yaani hivi sasa nawaza kwa sauti,"hivi huyu CAG hii ripoti angeisoma mbele ya al marhum magufuri kuhusiana na hasara iliyoleta midege yake mpaka saa hii bado angekuwa kazini au angekuwa kijijini kwake"?
 
Mkuu tazama vizuri Victor Mlaki

Ripoti za CAG
2015/16 hasara ilikuwa bilioni 94.3,
2016/17 iliongezeka ikafikia bilioni 109.3
2017/18 ilipungua na kuwa bilioni 113.

Swali 109.3 >> 113 imepungua!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…