The wave
JF-Expert Member
- Feb 27, 2021
- 283
- 318
Usafiri wa anga kwa Tanzania umekuwa anasa, hasa baada ya kuondoka fast jet. Ieleweke wazi usafiri wa anga kwa nchi za wenzetu ni kitu cha kawaida. Wala bei haiko juu Kama kwetu, Atcl ili iweze kujiendesha kwa faida inabidi ipate abiria wa kutosha. Na ili ipate abiria inabidi nauli ishuke kidogo, simaanishi washushe bei Kama mabasi ya kutoka Shinyanga kwenda Simiyu. Sina maana hiyo wanajamvi, ninachomaanisha washushe bei inayostahimilika hata kwa wananchi wa hali ya kawaida. Mfano majuzi nimesafiri kwa 328,000/= one way, ndani ya nchi hii hii tz ni wangapi wanamudu nauli hiyo?. Usafiri wa anga usiwe anasa, tuache ushamba usafiri wa ndege uwe Kama usafiri wa kawaida. Kwani tunaporuka angani siyo kwamba tunaenda peponi moja kwa moja, inapofika destination ya safari tunatua aridhini tena, why so expensive in tz?!!!!.