Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles Kichere amesema baadhi ya taasisi hazikuzingatia mapitio ya kisheria wala ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kusaini mikataba yenye thamani ya Tsh. Bilioni 56.
Ameeleza hayo Machi 30, 2026 wakati akisoma Ripoti ya ofisi yake ya Mwaka 2024/2025, ambapo ametaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kilichosaini mkataba wenye thamani ya Tsh. Bilioni 4.87 pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkataba wa Dola Milioni 4.79 ambayo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 12.45.
===================
Kwa msingi huu kuna uwajibikaji kweli kwenye ofisi zetu za Umma au tutaendelea hivi hivi kusikia hizi ngonjera kisha hakuna kinachofanyika kama kawa?