CAG fanya ukaguzi maalum kwa waliotumbuliwa ili kuona hasara Taifa iliyopata na ushauri mbinu kukabiliana na utumbuaji usio na tija

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Hakuna Jambo linalodhorotesha Utumishi wa umma nchini Kama hii style yakutumbuana kila siku. Viongozi wa nchi wameacha kutafuta suluhu ya matatizo ya wananchi badala yake wamejikita kutumbua kila siku na bila hoja ya msingi. Clip ikirushwa mtandaoni tayari mtu amefukuzwa kazi bila kujali uhusika wake.

Lakini pia utaratibu huu umeligharimu taifa fedha nyingi sana ambazo zingeweza kusaidia kufanyika kwa shughuli nyingine zakulisaidia taifa.

Kumtumbua mtu kunaambatana na kumlipa maslahi yake na kama alikuwa mwajiriwa wa kudumu serikalini anarejea kazi yake ya awali bila kushuka kwa mshahara wake Jambo linalopelekea mtu kulipwa fedha nyingi kwa majukumu yasiyolingana na mshaara.

Wananchi wamekuwa wakishangilia lakini wakumbuke anayetumbuliwa analitia taifa hasara kwa kulipwa benefits za cheo alichokuwa nacho pamoja na gharama nyingine ikiwemo kusafirisha familia na mizigo kurejea eneo lake la makazi au kituo Cha kazi kwa wale wanaorejea ofisi zao za awali.

Wanaharakati nao pia wamekuwa wakipiga kelele kushangilia na kufurahia, wanasiasa vilevile na wasomi kwa jumla.

Kiwango Cha uteuzi na utumbuaji Tanzania ni kikubwa kwa miaka mitano iliyopita nadhani kuliko Taifa lolote Duniani. Je watu wanaoteuliwa Wana sifa? Kama Wana sifa je, anayetengua ana sababu zakutengua au nikufurahisha adhara?

Kwa mfumo huu unaoendelea, ni mteule gani wa Rais atakayekuwa na courage ya kusimama na kuongoza wakati anajua akitumbuliwa jamii inamzomea? Kwanini viongozi wasiwe unpopular kulinda cv zao? Leo hii kwa style inayoendelea kama tungepewa nafasi yakuwatumbu Marais kwa mapungufu yao tungekuwa na Marais wangapi?

Nadhani ni wakati wakusema kutumbua No la sivyo wanaotumbuliwa watiwe hatiani ili wakose stahiki zao na kuliepusha Taifa na gharama za mishahara mikubwa ya watendaji wanaorudi kukaa benchi huku wakinufaika na marupurupu ya vyeo vyao.
 
Ndugu usiandike kitu kwa miemko ujui changamoto wanazopitia wananchi kwa viongozi mizigo kama hao unao watetea wanajiona mungu watu wanapokua kwenye utendaji wao wanashindwa kutatua changamoto za wananchi ndugu yangu morogoro kuna uozo mwingi sana kuhusu watendaji wa halmashauri
 
Hivi ni tatizo ni utumbuaji usokuwa na tiba au uteuzi wa kimazoea??
Ifike kipindi Rais apunguziwe kazi... Na kuwepo inclusive national vetting committee!
 
Naunga mkono hoja, na hili hata mimi niliwahi kulisema hapa
P.
 
Bite, hili uliwahi lisema, jana limetajwa Bungeni Kwenye hotuba ya bajeti kuu ya serikali
Mkuu Johnny Sack , kumbe hili wewe ndio umelijua jana!, karibu angalia tarehe ya bandiko hili uone watu tulisema nini na lini
Nilisema
P.
 
Dhana ya kutumbua ni kielelezo cha kutofuata misingi ya utawala wa sheria na utawala bora. Aliyekua mtumbuaji mkuu wa serikali alikua kilaza kwenye sheria za kazi na hakuwa na abc za implications za kiuchumi wakati anatekeleza hiyo kazi kikatili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…