BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia haijatoa Sh1.23 bilioni kwa ajili ya elimu bila malipo, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini.
Kulingana na ripoti kuu ya ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyowasilishwa leo Jumatatu, Aprili 15, 2024 katika Bunge la Tanzania, kutolewa kwa fedha pungufu kunaathiri uwezo wa shule kupata mahitaji na vifaa muhimu vya kufundishia na kujifunzia na pamoja na ukarabati wa miundombinu ya kutolea elimu.
CAG Charles Kichere amebaini kupitia taarifa ya elimu msingi na sekondari, kuwa mahitaji ya fedha kwa mwaka 2022/2023 yalikuwa Sh11.83 lakini kiasi kilichotolewa kilikuwa Sh10.57 bilioni, pungufu ikiwa ni Sh1.25 bilioni.
“Aya ya 1 & 2 ya waraka wa ruzuku kwa shule za Serikali kuhusu utoaji wa elimu bila malipo… uliotolewa Desemba 28, 2015 unaitaka Serikali kutoa fidia ya Sh10,000 na Sh25,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka kwa shule za msingi na sekondari mtawalia,” imeelezwa kwenye taarifa hiyo.
Pia soma:
Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2022/23
CAG Kichere: Licha ya kupewa Ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22