CAG: Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970

CAG: Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa kuhuisha vipengele vyote vya upembuzi yakinifu uliofanyika awali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), imeeleza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Badala yake ripoti hiyo ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 imesema Tanesco lilitegemea upembuzi yakinifu ambao ulifanywa katika miaka ya 1970 na 1972 na kampuni ya M/S Norconsult ya Norway.

Pia shirika hilo linatumia mpango mtambuka wa mradi na ripoti ya uchunguzi wa kiufundi uliofanywa na kampuni ya M/S Hafslund na M/s Norplan pia kutoka Norway ambayo ilihuisha vipengele vya taarifa ya upembuzi yakinifu miaka ya 1980.

“Vipengele ambavyo havikufanyiwa mapitio na kuhuishwa ni pamoja na utafiti wa kiuchumi na kifedha wa mradi, tafiti za kuwepo kwa maji na uendeshaji endelevu wa mradi,” imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imesema maofisa waandamizi wa Tanesco waliozungumza na CAG walieleza kwamba, upembuzi yakinifu uliofanyika katika miaka ya 1970 ulionesha kwamba mradi unawezekana kitaalamu, kiuchumi na kifedha.

“Maofisa waliongeza kuwa kutokana na uharaka wa kuanza utekelezaji wa mradi, taarifa za upembuzi za awali hazikuweza kupitiwa upya zote ili kuzihuisha,” inaeleza.

Ripoti hiyo imesema kuhuishwa huko kwa upembuzi kunatakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Umeme ya mwaka 2008, Sheria ya Umwagiliaji ya Kitaifa ya mwaka 2013, Sheria za Usimamizi ya Vyanzo vya Maji ya mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004.

Mwananchi



PIA SOMA


TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA
 
Ilani ya CCM 2020 - 2025 inasema tutaendelea kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote.

Haisemi ufisadi umeisha.

Hata Ulaya kina Morinyo, Messi, Ronaldo mara kwa mara tunasikia aamepelekwa mahakamani kwa kukwepa kodi.

Hata Chadema wabunge wengi walihama mwaka jana sababu ya ufisadi michango yao. Kinachotakiwa ni kuendelea kupambana na ufisadi.
 
So what!!?
nyuzi za upondaji na watu wenye wivu zipo nyingi sana humu, nyuzi mojawapo hii hapa.
kazi nzuri za JPM zimeonekana.

Magufuli kashakufa siku nyingi, mbona mnateseka sana na kivuli chake!
CAG ndo anateseka sio sisi mkuu

Sisi tulishateseka mpaka tukawa wapole siku nyingi.

Swali kweny: CAG alikua na ripoti mbili au ni hii hii alikua kajiandaa kumsomea Chuma? Manaake sipatii picha ingekuwaje
 
Aliiharibu mno nchi na Ustawi wake pia.
Nchi ipo hivyo hivyo tu, ni nyie tu na mihemko yenu kwani kwa JK mlisemaje? Watu wenye upeo mdogo sana wa kufikiri(Low thinking capacity) ndo wanaongeaga huo uk.uma. hakuna Raisi aliyeharibu wala kuipaisha nchi. Nchi ipo hivyo hivyo na CCM ni ileile tu. Nyie mnaofuata upepo na akili finyu ndo mnakuja na hivi vioja.
 
Nchi ilikuwa inaendeshwa kwa utashi was MTU sheria zooote ziliwekwa pending!

Kwa taratibu za kifedha karibu miradi yooote ya stoni itakuwa nje ya utaratibu!

Kunahaja serikali yooote ijiuzulu tufanye uchaguzi upyaaa!! Stone hakushauriwa vyema na makamu wake,waziri mkuu,spika,bunge,chama nk.
Kama walijua hashauriki kwanini walituletea kama mgombea na wakawa wanamsifu kila dakika?

Kistaarabu serikali yooote ijiuzulu tuchague upya asisingiziwe MTU mmoja asiyeweza kurudi kuitetea!
  • bandari hovyo
  • atcl hovyo
  • utalii hovyo
  • mawasiliano hovyo
  • elimu hovyo
  • afya hovyo
  • demokrasia hovyo
Embu serikali istep down kidogo turudie uchaguzi maana Samoa alisema stone alikuwa mwalimu wake sasa kama mwalimu kaharibu hivi mwanafunzi wake je??
 
Hii inaonesha kuwa upembuzi yakinifu Wa mwaka 1972 bado haujapitwa na wakati!! Si mnaona mradi unaendelea vizuri! Si kila kitu huwa kinapitwa na wakati!! Hata Newton laws of motion hazijapitwa na wakati hadi leo!! Inaonekana wazi Kabisa kuwa upembuzi yakinifu ulikuwa projected kwa miaka mingi ya mbele!

Wapigaji walitaka upembuzi yakinifu mwingine ufanyike ili wapige pesa tena!! Upembuzi yakinifu wa mradi kama ule ungechukua muda usiopungua miaka miwili!! Mafisadi wana hasira walikoseshwa ulaji!! "We are watching".
 
Jiwe alikuwa ni big propagandist Mkubwa wa kudraw attention za futureless people called wanyonge kwa kupitia kutobanduka kwenye camera.Amekaa kwenye camera mda mrefu sana kuliko mda aliokaa ofisini.Kitu kimoja akizindua urudiwa tbc mara elf 10 kumi.Mara cheap propaganda za kuaandaa wauza chips, mahindi, kuku, mapapai, nk.Jamaa alikuwa na shallow mind reasoning capacity.
 
Nchi ipo hivyo hivyo tu, ni nyie tu na mihemko yenu kwani kwa JK mlisemaje?.. watu wenye upeo mdogo sana wa kufikiri(Low thinking capacity) ndo wanaongeaga huo uk.uma. hakuna Raisi aliyeharibu wala kuipaisha nchi. Nchi ipo hivyo hivyo na CCM ni ileile tu. Nyie mnaofuata upepo na akili finyu ndo mnakuja na hivi vioja.

Swine wakitakiwa Watu very Brainy na Wewe Pimbi utajitokeza kabisa ukiwa mkavu hivi?

Utamtetea ila bila hata hiyo CAG Report inajulikana kuwa Mnafiki wenu kasabisha Hasara kubwa tu.

Kuwa mwana CCM au Team Hayati hakukufanyi usimkosoe eti kwakuwa ameshafariki. Hopeless!!

Wakongo na Waganda hadi leo wanawasema akina Mobutu na Idi Amin kwa Matendo yao mabaya.

Sasa kama mnampenda hivi si nanyi Mfe makusudi tu mkazikwe mkabala ( jirani ) nae huko Ziwani alikolala?

Mmekalia tu Unafiki na kumfanya Hayati kama alikuwa ni Mungu Mtu hapa Tanzania. Tumewachokeni!!

Wenzake waliiba Kistaha ( Kidiplomasia ) ila Yeye alikuwa anakwapua na Kunyakua kwa fujo.
 
Back
Top Bottom