CAG Mstaafu Ludovick Utoh: Kuna ukakasi kusema Rais ametoa hela inapaswa kuwa Serikali imetoa hela kutekeleza miradi

CAG Mstaafu Ludovick Utoh: Kuna ukakasi kusema Rais ametoa hela inapaswa kuwa Serikali imetoa hela kutekeleza miradi

Mbona unaandika kama unafukuzwa kama mbwa koko?

Nilipoona tu uandishi wako ulivyo wa hovyo nime ignore hata kusoma content aise, huwa mnaboa sana kukosea KISWAHILI chetu fasaha, unaandika kama kilugha wakati lugha yetu ni kama dhahabu.
 
Magufuli ndio katuletea mkosi wote huu, unashangaa jitu kubwa zima limesimama mbele ya mwendakuzimu linaomba kitu "eti ikikupendeza" naomba abcd.

Na lenyewe lilivyo shetani likajiaminisha isipompendeza imekula kwenu, wakati ni kodi zenu.

Utalisikia eti ukiweka betri na gunzi tochi itawaka kweli? Na wajinga waliomzunguka walikuwa wanamuona kichwani yupo sawa tu.
mzee alituharibia Nchi kabisa,
 
Haya yote ni matunda ya serikali ya mama ya awamu ya sita, kutowajaza wananchi hofu na woga.

Magufuli tutamkumbuka kama mtu katili, aliyejaza watu hofu na woga na kuwaambukiza mazuzu wake kina Profesa Kabudi roho mbaya, na vitisho na kujipendekeza kulikovuka viwango.

Tuliambiwa na Kabudi kwenye awamu ya tano kama ukubaliani nao uwasaidie tu kwa kukaa kimya kabisa.

Nadhani mama afanye afanyavyo huyu Kabudi hastahili kuwemo kwenye cabinet ya awamu ya sita hata kama sifa anazo haijarishi, bado wananchi tukimuona pale nyogo zetu zinaongezeka, hawa ni malaika wa kuzimu wa mungu wa chato.
kiukweli Kabudi niwakutimuliwa, ni masalia ya yule bwana katili
 
Mzee Ludovick Utoh, Sasa akiongoza taasisi iitwayo wajibu, alikuwa CAG kwa miaka 8.

CAG mmoja hivi amenyooka Kama rula, akipiga kila palipostahiki pasi na kusita mradi tu maslahi ya imma yasipindishwe.

Akihojiwa na Chief Odemba wa Star TV, Jana usiku alupoulizwa Kama, ni sawa kwa Viongozi kusema raisi ametoa hela za kutekeleza mradi fulani?

Lutoh anajibu, hapana, si sawa, anasema hela ni za wananchi, za imma, bunge huidhinisha matumizi yake kwa niaba ya wananchi.

Serikali Ni wakala tu, anasimamia yakiyopitishwa/ yakiyoidhinishwa na bunge. Si sawa kubinafsisha jukumu la utoaji hela za serikali (za watu) kwa Rais, sio zake.

Kwa maana hiyo,baada ufafanuzi huo wa Mh. LUDOVICK Utoh tunategemea kuona viongozi wakianza kutumia neno, SERIKALI IMETOA HELA YA MRADI X, badala ya kutumia neno RAIS ametoa, wenye akili hutafsiri kuwa hiyo ni lugha ya kujikomba kwa Rais na kumpa Ukuu wa Uwezo kifedha ambao kimsingi sio wake yeye bali ni wa wananchi.

Jumapili njema!
Katiba tuliiweka pembeni, siku hizi haututumii bajeti za bunge , tunatumia pochi la mama mpaka hapo uchumi utakapotengamaa.
 
Ushasema fedha ni za wananchi, kwamba serikali ni wakala tu…. basi isemwe kabisa wananchi wametoa fedha za mradi X.
Ni fedha za umma zimekusanywa na serikali. Ili fedha hizo ziweze kutumika serikali inaomba kibali cha bunge. Hivyo ni fedha zinazotumiwa na serikali katika shughuli mbalimbali za umma baada ya kuidhinishwa na bunge.
 
Kama kweli Uto ametoa kauli hiyo, basi na yeye hana maana na ni wa kudharauliwa kabisa. Yani msomi wa aina yake anasumbuliwa na maneno/kauli za wapambe! Shame on him Utto!
 
Zamani hata haikuwa Rais ilikuwa Magufuli ametoa na akiamuru kitu hasemi tumeamua alikuwa anasema nimeamua...ndio aina ya uongozi tulioupenda acha kazi iendelee🏃🏃🏃
 
Mzee Utoh yuko sahihi,sema wapambe wa Rais kupenda kujipendekeza na kujikombakomba kwake. Vilevile uonekane kwa wananchi as if Rais kawaonea. huruma kusapoti miradi yao wakati ni kodi zao.
 
Sitasahau ile siku Mwaluko alivyomu address mwendazake Kama mheshimiwa Mungu. Hiyo ndiyo siku tulipochonganishwa na malaika Israeli.
 
Mbona unaandika kama unafukuzwa kama mbwa koko?

Nilipoona tu uandishi wako ulivyo wa hovyo nime ignore hata kusoma content aise, huwa mnaboa sana kukosea KISWAHILI chetu fasaha, unaandika kama kilugha wakati lugha yetu ni kama dhahabu.
Muhimu ujumbe umefika. Kiswahili wengine ni lugha ya pili.
 
Kama kweli Uto ametoa kauli hiyo, basi na yeye hana maana na ni wa kudharauliwa kabisa. Yani msomi wa aina yake anasumbuliwa na maneno/kauli za wapambe! Shame on him Utto!

Uto ni kifupi cha utopolo?
 
Kwa hiyo unapingana na Mzee Lutoh?

Hili haliko sawa. Hatukuwahi kulisikia kwa JK, Mkapa, Mwinyi na Nyerere.

Tuungane na Mzee Lutoh kupinga hizi lugha za kilaghai.

Mnawapa utukufu viongozi wasioustahili matokeo yake mamalaka ya wananchi ambao ndio wenye hela zao yanakua yamedogoshwa Sana.
Miaka 6 imepita na huu ndo ulikuwa mtindo na watu walikuwa kimyaaaa, wakiongea basi ni kupongeza tu. Leo hao wameshaanza... mama anaupiga mwingi na kuna watu nawaona kabisa wanachanganyikiwa na kufadhaika, mwishowe vinabishwa vitu ambavyo hata maana hakuna. HV msomi gani anashindwa kuelewa maana kusudiwa hapo hadi Iwe kelele?!!!
 
Back
Top Bottom