Mwandishi: Nikikurudisha nyuma Profesa, 2018. Tupo kwenye uhuru. Unahisi maneno yako uliyotoa kwamba, "Bunge ni dhaifu," tungeweza kurudisha labda muda 2018, ungeyafuta yale maneno au ungesimama na msimamo wako wa Bunge ni dhaifu kipindi kile?
Professor Mussa Assad: Unajua, labda tukubaliane. Hakuna sehemu hata moja ambayo mimi nilisema Bunge ni dhaifu. Na bahati nzuri sana Bunge lenyewe lilifanya quotation ya mazungumzo yangu na Radio UN. Sikuwahi kusema Bunge ni dhaifu. Hayo ni mazungumzo ya Marehemu Ndugai, na kwa kweli watu wengi waliamini kwamba nilisema mimi Bunge ni dhaifu. Sikuwahi kusema, Nilisema mimi, "Kama kuna udhaifu ndani ya Bunge, itakuwa ni kwa sababu wanashindwa kutekeleza, kusimamia utekelezaji wa mapendekezo yetu." Kwa hiyo kama ni 'if' kuna udhaifu—weaknesses—ndani ya Bunge. Ndicho nilichosema,
Professor Mussa Assad: Sio Bunge ni dhaifu. Sikusema Bunge ni dhaifu, nilisema kuna udhaifu ndani ya Bunge kwa sababu definitely, kama unashindwa kusimamia utekelezaji wa mapendekezo—na nilikuwa na ushahidi.