CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

Ameungana na Askofu Dallu wakati wa mazishi ya askofu maluma kule njombe, naona alilisema hili kwa hisia kali kwamba "serikali inatoa huduma, sio biashara" akashukuru kwa "miundombinu mizuri" na kuomba "tusirudi tulikotoka" sikumwelewa haraka ila sasa naanza kumwelewa.
 
Halafu anatokea mpumbavu mmoja sijui anaitwa Kibajaji au yule shwaini mwingine anajulikana kwa jina la msukuma anataka kuleta hoja za mtaani huko kupingana na wasomi waliokaa darasani wakati yeye anachunga Ng'ombe huko porini
 
Tena aliongea huku amemkazia macho waziri Lukuvi!
 

Kunanjambo haujui,unapoongeza mishara kwa Pesa iliyopangwa kufanyia Bihashara ikiisha miaka inayofuta utatumia hela gani kuongeza mishahara?
 
Halafu anatokea mpumbavu mmoja sijui anaitwa Kibajaji au yule shwaini mwingine anajulikana kwa jina la msukuma anataka kuleta hoja za mtaani huko kupingana na wasomi waliokaa darasani wakati yeye anachunga Ng'ombe huko porini
Kibajaji alikuwa kiongozi mkubwa Chadema kabla ya kuhamia CCM!

Kibajaj ni bure kabisa
 
Serikali haitakiwi kufanya biashara bali wajibu wa Serikali kutoa huduma kwa wananchi. Biashara hufanywa na Sekta binafsi. Acha KUKURUPUKA na kuandika ujinga. Serikali ikishajiingiza kwenye biashara na sekta binafsi inafanya nini!? 😳😳
Kunanjambo haujui,unapoongeza mishara kwa Pesa iliyopangwa kufanyia Bihashara ikiisha miaka inayofuta utatumia hela gani kuongeza mishahara?
 

Kwa hiyo zile bilioni 28 tulizotangaziwa na mmiliki wa nchi akisema ni faida ya ATCL haikusawa kweli?
Hiyo ni gross profit
 
Hapa mwamba kachemka kidogo
Tanapa ni shirika la umma
Tanesco ni shirika la umma
Dawasa ni shirika la umma
Yote hayo yanafanya biashara
Uttoh amesema wasiite dividend watafute jina chengine....maana kulipa dividend kama shirika lina hisa kwenye stock exchange kama DSE kuna wanahisa. Huwezi lipa dividend kama hujapata faida kwenye mahesabu yako ndio maana akashauri litafutwe jina chengine na ambayo kwangu kwa elimu ndogo ya uhasibu itakuwa ni moja ya matumizi yaani expenditure na sio faida wala dividend!
 
Serikali haitakiwi kufanya biashara bali wajibu wa Serikali kutoa huduma kwa wananchi. Biashara hufanywa na Sekta binafsi. Acha KUKURUPUKA na kuandika ujinga. Serikali ikishajiingiza kwenye biashara na sekta binafsi inafanya nini!? 😳😳
Serikali ya wapii hiyo isiyotakiwa kufanya biashara
 
Nadhani we ndio unajiangusha, Kwanza hakuna sekta yogote ambayo budget yake ilipanda zaidi ya sekta ya ujenzi (Rudi uangalie utekelezaji wa budget Kwa kipindi chote cha miaka mitano ya JPM) issue ya inflation na deflation ni issue ya kisera ambayo inafanya automatically kusiwe na inflation au deflation na kamwe sio state organized kwamba hakuna inflation huku mtaani unaona inflation inapaa.

Issue ya salary increment ni takwa la kisheria na bahati nzuri focus huwa Iko Kwa wafanyakazi wa umma ambao basically Kwa mfumo wa Dunia wanatoa service and not business unayoweza kusema inaleta faida. Sasa ukirudi kwenye Sera ambazo zinawekwa na serikali na utekelezaji wake utakuta kuwa huko ndiko kunakotakiwa kutiliwa maanani hasa Sera ya uwekezaji ambayo itavutia wawekezaji na hivyo kuongeza Kodi kwenye pato la Taifa. Hawa wafanyakazi wa umma wanachoofa hapo ni PAYE tu labda na zile "Regressive Taxes" ambazo Kwa nchi hii ziko kila Kona. Sasa huku kwenye investment ndio alipaharibu mpaka wafanyabiashara wakakimbia na ili kujifanya tuko vizuri tukajikuta tunaunda task force ya kupora fedha ili kuonyesha mapato bado yapo.

The only place JPM alifanya vizuri ni kwenye ujenzi ambako nako kuna mgogoro maana Kwa taarifa ya CAG kuna demo la zaidi ya 700b wakandarasi walikuwa wanadai. So tuwe wakweli Tu mwendazake was awful
 
wewe jamaa huwa una matatizo ya akili kabisa fuatilia kabisa unachocoment mara nyingi unaonekana ni mtu mwenye uelewa mdogo sana na kama ulisoma basi wazazi wako walipoteza hela bure yaani ni full kilaza kwa kitaalamu tunasema you are mentally retarded
 
Hebu niambie Serikali za nchi za Ulaya zinazofanya biashara yoyote ile. Serikali wajibu wake ni kukusanya kodi na kutoa huduma. Nchi za Afrika Serikali zinajiingiza kwenye biashara na matokeo yake ni kuingia mkenge wa hasara kubwa kwa walipa kodi.
Serikali ya wapii hiyo isiyotakiwa kufanya biashara
 
Bak na Tindo hawana concepts yeyote juu ya uchumi na maendeleo utakesha mkuu na mbaya zaidi hawa taking Kujifunza , waulize nini maana ya elumu bure na impacts zake katika jamii? anaweza usiongeze mishahara uka chagua kutoa elimu bure maana yake mfanyakazi akipata pesa yake hachangii tena kwenye elimu inabaki kuwa yake mfukoni, naweza kukuongezea mshahara nikapandisha riba za mikopo, elimu ikawa ghari, huduma za jamii zikawa ghari na usione faida ya salary increments.
 
Reactions: Ame

Hunijui wewe! Ungekuwa unajua chochote kuhusu uchumi usingemuunga mkono dikteta magufuli na KUKURUPUKA kwake katika mambo ya kiuchumi ambayo hakuwa na ufahamu nayo matokeo yake kaua uchumi wa nchi. Ajira hakuna, pesa mtaani hakuna, wafanyabishara ama wamekimbia nchi au wamefunga biashara zao.

 
Gharama za maisha zilipanda kipindi Cha magufuli mfano mafuta ya kula, riba kwa mikopo ya chuo, sukari, dawa mswaki n.k au bado unaishi kwa baba huo unafuu mbona atukuuona
 
Gharama za maisha zimepanda sana kipindi Cha magufuli huo unafuu ni upi unaongelea
 
Kwanza tuelewe kwamba kuna tofauti ya ATC (Air Tanzania Corporation) ya enzi za mwalimu na ATCL (Air Tanzania Company Limited) hii ya Sasa hivi pamoja na kuwa ni public owned lakini ni biashara inayotakiwa kutengeneza faida. Kwahiyo yes lazima ilipe park fee na hizo tozo nyingine zote kama wanavhofanya Precision na wengine.

Na uelewe kwamba as of now ATCL hawamiliki ndege hata Moja ndege zote zinamilikiwa na serikali chini ya wakala wa ndege za serikali na ATCL no mkodishaji Tu. Kwa maana kwamba kama serikali imeamua kufanya biashara ya jukodisha ndege basi hata precision au auric wanaweza kwenda kukodi. Lakini kwasababu zinazoeleweka tukasema kwanini tumpe mtoto wa jirani chakula ilihali wa kwetu ana njaa? So wakapewa ATCL na mpaka Leo hii Kati ya tozo ya 75b waliyotakiwa kulipa Kwa kukodisha ndege hizo wamelipa 8b Tu.

Sasa ukirudi kwenye maana halisi ya gawio (Dividend) ni faida ambayo hupewa wawekezaji (Kwa maana ya serikali/umma) kwenye issue ya ATCL baada ya bodi kukaa na kupewa taarifa ya fedha ya mwaka pamoja na mipango ya maendeleo ya mwaka unaofuata so Ile faida itawekwa kwenye mipango iliyopitishwa na baadae wataamua kiasi gani wanakiacba Kwa dharura then kinachobaki ndio inakuwa gawio. Kwa muktadha huu inamaanisha ATCL walikuwa wanapata faida ya zaidi ya 28b jambo ambako sio sahihi ukaguzi umeonyesha wanapata hasara tena kubwa. Ndio maana Uttoh anasema like walichokitoa kiutaratibu hakiwezi kuwa dividend itakuwa kitu kingine tu

Jambo la msingi hapa la kukumbuka ni kwamba ATCL haimiliki uwanja wote wa ndege, pamoja na huduma zote zotolewazo hivyo lazima wazilipie na kwenye hesabu zao lazima zitokee kama cost of operations.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…