CAG na waliojikopesha Sh41 bilioni NHIF

CAG na waliojikopesha Sh41 bilioni NHIF

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
Dar es Salaam. Wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ikibainisha wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) walijikopesha Sh41.42 bilioni na kusuasua kuzilipa, menejimenti ya uongozi wa mfuko huo umetoa ufafanuzi.

Katika ripoti hiyo ya mwaka 2021/22, CAG Kichere anasema kuna kupungua kwa ukwasi wa mfuko huo unaochangiwa na mambo mengi, kutorejeshwa kwa mikopo ya watumishi wa NHIF.

“Nilibaini kuwa hadi Juni 30, 2022, NHIF ilikuwa na mikopo ya wafanyakazi ambayo haijalipwa Sh41.42 bilioni, kati yake Sh11.18 bilioni ikiwa mikopo mipya iliyotolewa 2021/22.”

CAG anasema mikopo hiyo ilitolewa bila kuzingatia mahitaji ya aya 1.4 ya sera ya mikopo ya wafanyakazi wa mfuko ambayo inahitaji mikopo kutolewa chini ya mfumo wa kukopa na kulipa,” anasema CAG.

Aliongeza: “Nilibaini kupungua kwa ukwasi wa fedha za mfuko huo, hata hivyo mfuko uliongeza ukomo wa mkopo kwa wafanyakazi, hii inatokana na mfumo usioridhisha wa usimamizi wa mfuko wa mkopo kwa wafanyakazi”

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano NHIF, Angela Mziray alisema “mikopo inayotolewa kwa wafanyakazi wa mfuko ipo kisera kama ilivyo kwa taasisi nyingine za umma na binafsi kwa ajili ya motisha na inarejeshwa kila mwezi na watumishi kupitia mishahara yao pamoja na riba, pia ina bima ili kuhakikisha hakuna hasara,” alifafanua Mziray.

Hata hivyo, katika mapendekezo yake, CAG anasema NHIF itekeleze sera ya mikopo na kuanzisha mfuko wa kukopa na kulipa ili kuepuka kuathiri ukwasi wa mfuko.

cag-info.png

Malipo hewa
Si mikopo tu, ripoti hiyo ya CAG imeonyesha NHIF ilivilipa vituo vya afya madai yasiyo ya kweli yanayofikia Sh14.46 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2019/20 hadi 2021/22.

Mbali na hili, CAG amebaini watumishi 146 wakiwemo 129 wa vituo vya afya na wa mfuko huo walijihusisha na vitendo vya udanganyifu.

“Watumishi 146 wa NHIF na wa vituo vya afya walijihusisha na vitendo vya udanganyifu, lakini Kitengo cha Kupambana na Udanganyifu kiliripoti maofisa 17 tu wa mfuko waliojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwa kamati za nidhamu,” anasema CAG.

Kuhusu suala hilo, Mziray alisema; "hapa 129 ni watumishi wa vituo vya matibabu, hawa NHIF tuliwaripoti kwenye mabaraza ya kitaaluma na watumishi wa NHIF 17 wameripotiwa kwenye kamati za nidhamu za Mfuko na Jumla ni 146.”

Vilevile, CAG anasema ripoti za kupambana na udanganyifu kati ya 2019/20 na 2021/22 zilibaini kuwepo na madai yasiyo ya kweli na yasiyo sahihi ambayo NHIF ilivilipa vituo vya afya.

“Kati ya Sh1.71 trilioni ambazo zililipwa kwa vituo vya kutolea huduma za afya kwa miaka mitatu ya fedha kuanzia 2019/20 hadi 2021/22, Sh14.46 bilioni zililipwa kwa madai ya uongo na yasiyo sahihi.

“Uchambuzi zaidi ulifanyika ili kupata malipo ya madai yasiyo ya kweli, katika vituo vya afya vya binafsi, Serikali na vile vya mashirika ya dini na kubaini vituo binafsi vya huduma ya afya vilikuwa na kiasi kikubwa cha madai yaliyolipwa yasiyo ya kweli ikilinganishwa na vya Serikali.

“Zaidi ya Sh10.38 bilioni zililipwa kwa vituo binafsi na madai katika vituo vya mashirika ya dini ilikuwa ni Sh2.49 bilioni na vituo vya Serikali ilikuwa Sh1.57 bilioni,” alisema CAG.

CAG alisema kumekuwa na ongezeko la madai yasiyo ya kweli na yasiyo sahihi kutoka Sh4.32 bilioni mwaka wa fedha 2019/20 hadi Sh4.55 bilioni kwa mwaka wa fedha 2020/21 na Sh5.59 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/22.

Kufuatia hilo, Mziray alisema, "hiyo ya Sh14.46 bilioni ni madai yaliyowasilishwa na vituo vya huduma za matibabu yasiyo ya kweli, ambayo yamepatikana kwenye ripoti za udanganyifu baada ya mfuko kufanya uchunguzi. Na sababu za madai haya zimetajwa hapo kwenye ripoti."

Hasara
Kwa upande mwingine, CAG alibaini mfuko huo ulipata hasara ya Sh205 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ikilinganishwa na hasara ya kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 ambapo ni Sh104 bilioni.
Akifafanua hilo, Mziray alisema fedha hizo si hasara, bali nakisi iliyotokana na mfuko kuelemewa kwa kuhudumia wagonjwa wengi ikilinganishwa na kiasi kinachokusanywa.

“Nakisi ya Sh205 bilioni inatokana na kwamba mfuko unalipa fedha nyingi zaidi za huduma wanazopata wanachama wake kwenye vituo, kuliko michango wanachama wanayochangia.”

Alisema kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza ambayo awali hayakuwepo nchini ambayo gharama yake ni kubwa kuyatibia ni mojawapo ya NHIF kupata nakisi hiyo.

Katika ripoti hiyo, CAG alisema katika mfuko huo kumekuwa na mtiririko hasi wa fedha katika shughuli zake za uendeshaji ambapo michango inaongezeka kwa asilimia 12.9 wakati matumizi yanaongezeka kwa asilimia 24.6.
CAG anasema taarifa ya tathmini ya mfuko kujiendesha inaonyesha mapato ya matumizi yataendelea kuwa chini na mfuko utatumia ziada iliyokusanywa na hivyo kusababisha ukwasi kuwa hasi ifikapo mwaka 2025.

CAG anapendekeza kuangaliwa upya namna ya kuuboresha mfuko, kuongeza wanachama wa hiari na kuboresha kanzidata ya Tehama na kuboresha usimamizi wa watoa huduma za afya.

Akizungumzia matokeo ya ukaguzo huo, Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za afya binafsi Tanzania (Aphta), Dk Egina Makwabe alisema vituo binafsi vinaonekana kutumia fedha nyingi katika udanganyifu kwa kuwa hata malipo, kwa asilimia kubwa yanakwenda huko.

Dk Makwabe alifafanua kuwa madai ya udanganyifu kwa mfuko yapo chini ya asilimia 2 ambayo ni ndogo, kwani kwa viwango vya dunia ni asilimia 5.

Hata hivyo alisisitiza hatua za Serikali kuelekea Bima ya Afya kwa Wote ni suluhisho kwa sababu wengi wakichangia si wote wataugua kwa wakati mmoja, hivyo huduma zitaongezeka na wengi watanufaika.

MWANANCHI
 
Dar es Salaam. Wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ikibainisha wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) walijikopesha Sh41.42 bilioni na kusuasua kuzilipa, menejimenti ya uongozi wa mfuko huo umetoa ufafanuzi.
Katika ripoti hiyo ya mwaka 2021/22, CAG Kichere anasema kuna kupungua kwa ukwasi wa mfuko huo unaochangiwa na mambo mengi, kutorejeshwa kwa mikopo ya watumishi wa NHIF.
“Nilibaini kuwa hadi Juni 30, 2022, NHIF ilikuwa na mikopo ya wafanyakazi ambayo haijalipwa Sh41.42 bilioni, kati yake Sh11.18 bilioni ikiwa mikopo mipya iliyotolewa 2021/22.”
CAG anasema mikopo hiyo ilitolewa bila kuzingatia mahitaji ya aya 1.4 ya sera ya mikopo ya wafanyakazi wa mfuko ambayo inahitaji mikopo kutolewa chini ya mfumo wa kukopa na kulipa,” anasema CAG.
Aliongeza: “Nilibaini kupungua kwa ukwasi wa fedha za mfuko huo, hata hivyo mfuko uliongeza ukomo wa mkopo kwa wafanyakazi, hii inatokana na mfumo usioridhisha wa usimamizi wa mfuko wa mkopo kwa wafanyakazi”.
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano NHIF, Angela Mziray alisema “mikopo inayotolewa kwa wafanyakazi wa mfuko ipo kisera kama ilivyo kwa taasisi nyingine za umma na binafsi kwa ajili ya motisha na inarejeshwa kila mwezi na watumishi kupitia mishahara yao pamoja na riba, pia ina bima ili kuhakikisha hakuna hasara,” alifafanua Mziray.
Hata hivyo, katika mapendekezo yake, CAG anasema NHIF itekeleze sera ya mikopo na kuanzisha mfuko wa kukopa na kulipa ili kuepuka kuathiri ukwasi wa mfuko.
cag-info.png

Malipo hewa
Si mikopo tu, ripoti hiyo ya CAG imeonyesha NHIF ilivilipa vituo vya afya madai yasiyo ya kweli yanayofikia Sh14.46 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2019/20 hadi 2021/22.
Mbali na hili, CAG amebaini watumishi 146 wakiwemo 129 wa vituo vya afya na wa mfuko huo walijihusisha na vitendo vya udanganyifu.
“Watumishi 146 wa NHIF na wa vituo vya afya walijihusisha na vitendo vya udanganyifu, lakini Kitengo cha Kupambana na Udanganyifu kiliripoti maofisa 17 tu wa mfuko waliojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwa kamati za nidhamu,” anasema CAG.
Kuhusu suala hilo, Mziray alisema; "hapa 129 ni watumishi wa vituo vya matibabu, hawa NHIF tuliwaripoti kwenye mabaraza ya kitaaluma na watumishi wa NHIF 17 wameripotiwa kwenye kamati za nidhamu za Mfuko na Jumla ni 146.”
Vilevile, CAG anasema ripoti za kupambana na udanganyifu kati ya 2019/20 na 2021/22 zilibaini kuwepo na madai yasiyo ya kweli na yasiyo sahihi ambayo NHIF ilivilipa vituo vya afya.
“Kati ya Sh1.71 trilioni ambazo zililipwa kwa vituo vya kutolea huduma za afya kwa miaka mitatu ya fedha kuanzia 2019/20 hadi 2021/22, Sh14.46 bilioni zililipwa kwa madai ya uongo na yasiyo sahihi.
“Uchambuzi zaidi ulifanyika ili kupata malipo ya madai yasiyo ya kweli, katika vituo vya afya vya binafsi, Serikali na vile vya mashirika ya dini na kubaini vituo binafsi vya huduma ya afya vilikuwa na kiasi kikubwa cha madai yaliyolipwa yasiyo ya kweli ikilinganishwa na vya Serikali.
“Zaidi ya Sh10.38 bilioni zililipwa kwa vituo binafsi na madai katika vituo vya mashirika ya dini ilikuwa ni Sh2.49 bilioni na vituo vya Serikali ilikuwa Sh1.57 bilioni,” alisema CAG.
CAG alisema kumekuwa na ongezeko la madai yasiyo ya kweli na yasiyo sahihi kutoka Sh4.32 bilioni mwaka wa fedha 2019/20 hadi Sh4.55 bilioni kwa mwaka wa fedha 2020/21 na Sh5.59 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/22.
Kufuatia hilo, Mziray alisema, "hiyo ya Sh14.46 bilioni ni madai yaliyowasilishwa na vituo vya huduma za matibabu yasiyo ya kweli, ambayo yamepatikana kwenye ripoti za udanganyifu baada ya mfuko kufanya uchunguzi. Na sababu za madai haya zimetajwa hapo kwenye ripoti."

Hasara
Kwa upande mwingine, CAG alibaini mfuko huo ulipata hasara ya Sh205 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ikilinganishwa na hasara ya kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 ambapo ni Sh104 bilioni.
Akifafanua hilo, Mziray alisema fedha hizo si hasara, bali nakisi iliyotokana na mfuko kuelemewa kwa kuhudumia wagonjwa wengi ikilinganishwa na kiasi kinachokusanywa.
“Nakisi ya Sh205 bilioni inatokana na kwamba mfuko unalipa fedha nyingi zaidi za huduma wanazopata wanachama wake kwenye vituo, kuliko michango wanachama wanayochangia.”
Alisema kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza ambayo awali hayakuwepo nchini ambayo gharama yake ni kubwa kuyatibia ni mojawapo ya NHIF kupata nakisi hiyo.
Katika ripoti hiyo, CAG alisema katika mfuko huo kumekuwa na mtiririko hasi wa fedha katika shughuli zake za uendeshaji ambapo michango inaongezeka kwa asilimia 12.9 wakati matumizi yanaongezeka kwa asilimia 24.6.
CAG anasema taarifa ya tathmini ya mfuko kujiendesha inaonyesha mapato ya matumizi yataendelea kuwa chini na mfuko utatumia ziada iliyokusanywa na hivyo kusababisha ukwasi kuwa hasi ifikapo mwaka 2025.
CAG anapendekeza kuangaliwa upya namna ya kuuboresha mfuko, kuongeza wanachama wa hiari na kuboresha kanzidata ya Tehama na kuboresha usimamizi wa watoa huduma za afya.
Akizungumzia matokeo ya ukaguzo huo, Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za afya binafsi Tanzania (Aphta), Dk Egina Makwabe alisema vituo binafsi vinaonekana kutumia fedha nyingi katika udanganyifu kwa kuwa hata malipo, kwa asilimia kubwa yanakwenda huko.
Dk Makwabe alifafanua kuwa madai ya udanganyifu kwa mfuko yapo chini ya asilimia 2 ambayo ni ndogo, kwani kwa viwango vya dunia ni asilimia 5.
Hata hivyo alisisitiza hatua za Serikali kuelekea Bima ya Afya kwa Wote ni suluhisho kwa sababu wengi wakichangia si wote wataugua kwa wakati mmoja, hivyo huduma zitaongezeka na wengi watanufaika.

MWANANCHI
Bima Kwa wote ni nzuri lkn kama ubadhirifu ni kiasi hicho, je NHIF imejipanga vipi Ili kuzuia wizi ubadhirifu na wanachama wapate huduma nzuri ,sio unaenda hospitali unaambiwa dawa hizi kanunue bima haitoi nk?

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Bima ya afya kwa wote my [emoji3097][emoji3097].

Serikali ya CCM haiwezi kusimamia bima ya afya kwa wote.....KAMWE haiwezi ..

Lengo lao ni kama kwenye KIKOKOTOO tu kuukoa mfuko basiii...
 
NHIF wezi, eti wagonjwa wameongezeka, sio kweli, hakuna wagonjwa kuongezeka, sbb kila mgonjwa ambaye analipiwa na NHIF tayari ni mwanachama wa NHIF, hivyo namba za wagonjwa wa NHIF ni wale wale member wa NHIF..

Wanataka kusema uongo labda frequencies za wagonjwa kwenda hosp zimeongezeka, which is not true, NHIF ni jipu kubwa sana, Mh. Rais aangalie haraka management ya NHIF, wizi ni mwingi sana kwa kusingizia wagonjwa. Wanatumia michango ya wanachama kujikopesha mabilioni, hili ni kosa kubwa sana sbb hizo hela ni za wanachama, alafu wanasema wanapata hasara wakati wanajikopesha hovyo hovyo, management yote kamata piga ndani, put in place new management and serious investigation ifanyike, we can't do what they do as usual, wataua NHIF very soon.
 
Wajinga kabisa

Hili ni tatizo kubwa fund yeyote management fee inatakiwa isizidi 20 percent ya contribution

NHIF management walicomply hilo? Hawatakiwi kula contribution za watu kuendesha shughuli za kila siku above 20 percent ya contribution fees

Wanaposema mikopo ina bima na wao ni bima inayoendeshwa kwa michango ya contributors hiyo bima walikowrka ni private insurance au public? Kama ni public kana National Insurance Corporation maana yake waki default pesa zetu walipa kodi ndizo zitatumika kulipa hiyo mikopo sababu NIC ni kampuni ya umma lakini mtu binafsi akikopa benki ya umma NIC wakaweka bima hakuna shida sababu mkopaji yuko nje ya public sector

OK waweke hesabu zao audited humu tuone source ya hiyo mikopo yao iko eneo lipi kwenye financial statements zao Wanatoa wapi kukopeshana? NHIF inatoa pesa eneo lipi kukopesha wafanyakazi wake

Mwenye financial statements zai aweke hapa tuwahoji hiyo mikopo yao wanakopeshana wafanyakazi inatoka eneo lipi? Kwenye financial statements zao?

Waandishi wa habari rudini mkazidai

Waonyeshe kabisa mikopo tunakopesha inatoka hqpa
 
Hapo inakuwaje kuwe kuna madai hewa kwenye vituo vya afya vya serikali? Hama kuna kitu hakiko sawa.
 
CA,G aanike mahesabu wazi ya NHIF tujue hiyo mikopo wanakopeshana wanatoa fungu gani badala ya kwenda kukopa kwenye mabenki ya biasharaa

Wanakula hela za NHIF contributors kupitia eneo lipi?

Mahesabu ya fund yawekwe humu tujue hela za wagonjwa walizochangia mfuko wanazokopeshana wanatoa eneo lipi

Wagonjwa wanachanga ili wafanyakazi wa NHIF wakopeshane? CAG weka hesabu za NHIF hadharani
 
Hii nchi inatafunwa mnoo,mpaka huruma aisee.
 
NHIF wezi, eti wagonjwa wameongezeka, sio kweli, hakuna wagonjwa kuongezeka, sbb kila mgonjwa ambaye analipiwa na NHIF tayari ni mwanachama wa NHIF, hivyo namba za wagonjwa wa NHIF ni wale wale member wa NHIF..

Wanataka kusema uongo labda frequencies za wagonjwa kwenda hosp zimeongezeka, which is not true, NHIF ni jipu kubwa sana, Mh. Rais aangalie haraka management ya NHIF, wizi ni mwingi sana kwa kusingizia wagonjwa. Wanatumia michango ya wanachama kujikopesha mabilioni, hili ni kosa kubwa sana sbb hizo hela ni za wanachama, alafu wanasema wanapata hasara wakati wanajikopesha hovyo hovyo, management yote kamata piga ndani, put in place new management and serious investigation ifanyike, we can't do what they do as usual, wataua NHIF very soon.

Ni simpo sana TOA chama mboga mboga
 
Huu mfuko kuna ufujaji sana wa pesa, ndiyo maana wanaweka vikwazo vingi watu wanapotaka kuingiza wategemezi kwenye nafasi zao, mara utasikia huyu mtoto siyo wako majina hayajafanana kwenye vyeti na upuuzi mwingine mwingi.

Halafu inakuwaje wao wajikopeshe pesa za mfuko wakati watumishi wengine wa umma wakitakiwa kwenda kukopa benki, hapa kuna walakini.​
 
Hii nchi kila sehemu imeoza. Yaani watumishi wengi wa umma wa ngazi za chini wanakopa benki, na kwenye taasisi za kifedha kwa riba kubwa!

Halafu wengine wanakopeshana tu hela za michango ya watumishi hao hao wa chini, tena kwa vigezo walivyojiwekea wenyewe!!
 
Back
Top Bottom