CAG na waliojikopesha Sh41 bilioni NHIF

CAG na waliojikopesha Sh41 bilioni NHIF

Dar es Salaam. Wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ikibainisha wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) walijikopesha Sh41.42 bilioni na kusuasua kuzilipa, menejimenti ya uongozi wa mfuko huo umetoa ufafanuzi.

Katika ripoti hiyo ya mwaka 2021/22, CAG Kichere anasema kuna kupungua kwa ukwasi wa mfuko huo unaochangiwa na mambo mengi, kutorejeshwa kwa mikopo ya watumishi wa NHIF.

“Nilibaini kuwa hadi Juni 30, 2022, NHIF ilikuwa na mikopo ya wafanyakazi ambayo haijalipwa Sh41.42 bilioni, kati yake Sh11.18 bilioni ikiwa mikopo mipya iliyotolewa 2021/22.”

CAG anasema mikopo hiyo ilitolewa bila kuzingatia mahitaji ya aya 1.4 ya sera ya mikopo ya wafanyakazi wa mfuko ambayo inahitaji mikopo kutolewa chini ya mfumo wa kukopa na kulipa,” anasema CAG.

Aliongeza: “Nilibaini kupungua kwa ukwasi wa fedha za mfuko huo, hata hivyo mfuko uliongeza ukomo wa mkopo kwa wafanyakazi, hii inatokana na mfumo usioridhisha wa usimamizi wa mfuko wa mkopo kwa wafanyakazi”

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano NHIF, Angela Mziray alisema “mikopo inayotolewa kwa wafanyakazi wa mfuko ipo kisera kama ilivyo kwa taasisi nyingine za umma na binafsi kwa ajili ya motisha na inarejeshwa kila mwezi na watumishi kupitia mishahara yao pamoja na riba, pia ina bima ili kuhakikisha hakuna hasara,” alifafanua Mziray.

Hata hivyo, katika mapendekezo yake, CAG anasema NHIF itekeleze sera ya mikopo na kuanzisha mfuko wa kukopa na kulipa ili kuepuka kuathiri ukwasi wa mfuko.

cag-info.png


Malipo hewa
Si mikopo tu, ripoti hiyo ya CAG imeonyesha NHIF ilivilipa vituo vya afya madai yasiyo ya kweli yanayofikia Sh14.46 bilioni kwa kipindi cha mwaka 2019/20 hadi 2021/22.

Mbali na hili, CAG amebaini watumishi 146 wakiwemo 129 wa vituo vya afya na wa mfuko huo walijihusisha na vitendo vya udanganyifu.

“Watumishi 146 wa NHIF na wa vituo vya afya walijihusisha na vitendo vya udanganyifu, lakini Kitengo cha Kupambana na Udanganyifu kiliripoti maofisa 17 tu wa mfuko waliojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwa kamati za nidhamu,” anasema CAG.

Kuhusu suala hilo, Mziray alisema; "hapa 129 ni watumishi wa vituo vya matibabu, hawa NHIF tuliwaripoti kwenye mabaraza ya kitaaluma na watumishi wa NHIF 17 wameripotiwa kwenye kamati za nidhamu za Mfuko na Jumla ni 146.”

Vilevile, CAG anasema ripoti za kupambana na udanganyifu kati ya 2019/20 na 2021/22 zilibaini kuwepo na madai yasiyo ya kweli na yasiyo sahihi ambayo NHIF ilivilipa vituo vya afya.

“Kati ya Sh1.71 trilioni ambazo zililipwa kwa vituo vya kutolea huduma za afya kwa miaka mitatu ya fedha kuanzia 2019/20 hadi 2021/22, Sh14.46 bilioni zililipwa kwa madai ya uongo na yasiyo sahihi.

“Uchambuzi zaidi ulifanyika ili kupata malipo ya madai yasiyo ya kweli, katika vituo vya afya vya binafsi, Serikali na vile vya mashirika ya dini na kubaini vituo binafsi vya huduma ya afya vilikuwa na kiasi kikubwa cha madai yaliyolipwa yasiyo ya kweli ikilinganishwa na vya Serikali.

“Zaidi ya Sh10.38 bilioni zililipwa kwa vituo binafsi na madai katika vituo vya mashirika ya dini ilikuwa ni Sh2.49 bilioni na vituo vya Serikali ilikuwa Sh1.57 bilioni,” alisema CAG.

CAG alisema kumekuwa na ongezeko la madai yasiyo ya kweli na yasiyo sahihi kutoka Sh4.32 bilioni mwaka wa fedha 2019/20 hadi Sh4.55 bilioni kwa mwaka wa fedha 2020/21 na Sh5.59 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/22.

Kufuatia hilo, Mziray alisema, "hiyo ya Sh14.46 bilioni ni madai yaliyowasilishwa na vituo vya huduma za matibabu yasiyo ya kweli, ambayo yamepatikana kwenye ripoti za udanganyifu baada ya mfuko kufanya uchunguzi. Na sababu za madai haya zimetajwa hapo kwenye ripoti."

Hasara
Kwa upande mwingine, CAG alibaini mfuko huo ulipata hasara ya Sh205 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ikilinganishwa na hasara ya kipindi cha mwaka wa fedha 2020/21 ambapo ni Sh104 bilioni.
Akifafanua hilo, Mziray alisema fedha hizo si hasara, bali nakisi iliyotokana na mfuko kuelemewa kwa kuhudumia wagonjwa wengi ikilinganishwa na kiasi kinachokusanywa.

“Nakisi ya Sh205 bilioni inatokana na kwamba mfuko unalipa fedha nyingi zaidi za huduma wanazopata wanachama wake kwenye vituo, kuliko michango wanachama wanayochangia.”

Alisema kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza ambayo awali hayakuwepo nchini ambayo gharama yake ni kubwa kuyatibia ni mojawapo ya NHIF kupata nakisi hiyo.

Katika ripoti hiyo, CAG alisema katika mfuko huo kumekuwa na mtiririko hasi wa fedha katika shughuli zake za uendeshaji ambapo michango inaongezeka kwa asilimia 12.9 wakati matumizi yanaongezeka kwa asilimia 24.6.
CAG anasema taarifa ya tathmini ya mfuko kujiendesha inaonyesha mapato ya matumizi yataendelea kuwa chini na mfuko utatumia ziada iliyokusanywa na hivyo kusababisha ukwasi kuwa hasi ifikapo mwaka 2025.

CAG anapendekeza kuangaliwa upya namna ya kuuboresha mfuko, kuongeza wanachama wa hiari na kuboresha kanzidata ya Tehama na kuboresha usimamizi wa watoa huduma za afya.

Akizungumzia matokeo ya ukaguzo huo, Mwenyekiti wa Chama cha watoa huduma za afya binafsi Tanzania (Aphta), Dk Egina Makwabe alisema vituo binafsi vinaonekana kutumia fedha nyingi katika udanganyifu kwa kuwa hata malipo, kwa asilimia kubwa yanakwenda huko.

Dk Makwabe alifafanua kuwa madai ya udanganyifu kwa mfuko yapo chini ya asilimia 2 ambayo ni ndogo, kwani kwa viwango vya dunia ni asilimia 5.

Hata hivyo alisisitiza hatua za Serikali kuelekea Bima ya Afya kwa Wote ni suluhisho kwa sababu wengi wakichangia si wote wataugua kwa wakati mmoja, hivyo huduma zitaongezeka na wengi watanufaika.

MWANANCHI
Kwahiyo anachosema mama Mziray ni kwamba CAG ni muongo, maana naona kakanusha kila taarifa iliyotolewa na CAG. Na kama hayo maswali yote yalikua na majibu hayo aliyotaja, kwanini hakuyampa CAG ili hizo hoja ziondolewe kwenye ripoti?
 
Wajinga kabisa

Hili ni tatizo kubwa fund yeyote management fee inatakiwa isizidi 20 percent ya contribution

NHIF management walicomply hilo? Hawatakiwi kula contribution za watu kuendesha shughuli za kila siku above 20 percent ya contribution fees

Wanaposema mikopo ina bima na wao ni bima inayoendeshwa kwa michango ya contributors hiyo bima walikowrka ni private insurance au public? Kama ni public kana National Insurance Corporation maana yake waki default pesa zetu walipa kodi ndizo zitatumika kulipa hiyo mikopo sababu NIC ni kampuni ya umma lakini mtu binafsi akikopa benki ya umma NIC wakaweka bima hakuna shida sababu mkopaji yuko nje ya public sector

OK waweke hesabu zao audited humu tuone source ya hiyo mikopo yao iko eneo lipi kwenye financial statements zao Wanatoa wapi kukopeshana? NHIF inatoa pesa eneo lipi kukopesha wafanyakazi wake

Mwenye financial statements zai aweke hapa tuwahoji hiyo mikopo yao wanakopeshana wafanyakazi inatoka eneo lipi? Kwenye financial statements zao?

Waandishi wa habari rudini mkazidai

Waonyeshe kabisa mikopo tunakopesha inatoka hqpa
waandishi wetu wa habari hawana huo uwezo wa kuhoji hiki ulichokiandika hapa
 
NHIF halafu unakuta dawa zingine hazipo kwenye bima!!!! unatakiwa uingie mfukoni!!!!

Kumbe wao wapo tu wanajikopesha fedha zetu!!!!

Kwakweli Serikali/viongozi wetu walio pewa dhamana wanapaswa wawe wakali ili kuepusha baadhi ya mambo ya ovyo kama haya.

Kinacho shangaza zaidi, viongozi wapo, watendaji wapo!!!!! Wee Mungu wangu duh!!!

Nimechoka Moyo unaenda mbio.

Sent from my V2118 using JamiiForums mobile app
 
Hii nchi kila sehemu imeoza. Yaani watumishi wengi wa umma wa ngazi za chini wanakopa benki, na kwenye taasisi za kifedha kwa riba kubwa!

Halafu wengine wanakopeshana tu hela za michango ya watumishi hao hao wa chini, tena kwa vigezo walivyojiwekea wenyewe!!
Unapoenda kupata huduma hospitali unaambiwa hii hailipiwi na bima, kumbe pesa wameshajikopesha........

Huu mfuko una madudu mengi, wabadili namna ya kuuendesha kwa kutumia watu wachache tu wa utawala, wataalamu wa IT na wahasibu.

Waweke na kikomo cha asilimia ya makusanyo ambacho kinatakiwa kutumika kwenye shughuli za uendeshaji maana hawachelewi kujikopesha za kununua ma viieite huku wagonjwa wakisoteshwa kwenye mahospitali kwa kunyimwa huduma au kupewa huduma duni.​
 
waandishi wetu wa habari hawana huo uwezo wa kuhoji hiki ulichokiandika hapa
Kipindi cha Magufuli alitaka waandishi wote wa habari wawe na degree na bodi ya kuwasajili ya taaluma yao na kuwasimamia utendaji wao Kama mainijinia,madaktari,manesi mswada ukaandaliwa wakapinga kafa haujapita

Matokeo ndio haya sasa

Tanzania hatuna waandishi wa habari tuna Reporters wa habari wa ku ripoti tu Raisi kasema nini,NHIF wamesema nini nk.,

Ni Reporters tu

Kazi ambavyo bwege yetote aweza fanya hata bila kwenda chuo cha uandishi wa habari hata mkulima aweza kuwa Reporter wa habari hata panya Road aweza

Hawezi shindwa ripoti kilichotokea au ambacho raisi,au mbunge au mbowe au Lisu au Lema kasema
 
Waondikane na nfuno huo, wawape madhirika binafsi ya bims ya uendeshe uone kama yatatokea huko yanayotojea hili shirika la serikali.

Serikqli haiwezi kuendesha biashara yoyote ile.
 
Taasis za kifedha zilivyo nyingi hivi bado taasis na mashirika ya umma yanakopesha wafanyakazi wake?
 
Lau kama ningekuwa na dawa ya kuwaloga mafisadi, wabadhiriifu,wezi na wazembe wa fedha za umma basi ningefanya hivyo haraka kabla ya kusubiria Kamati za Bunge zikae na kujadili ripoti ya CAG na Kisha kutoa mapendekezo mwakani 2024!!!!!

naumia sana moyo
 
Kwahiyo anachosema mama Mziray ni kwamba CAG ni muongo, maana naona kakanusha kila taarifa iliyotolewa na CAG. Na kama hayo maswali yote yalikua na majibu hayo aliyotaja, kwanini hakuyampa CAG ili hizo hoja ziondolewe kwenye ripoti?
Hoja ndio zinajibiwa sasaivi, isiyopata majibu sahihi haifutwi inafikushwa bungeni na mahakamani kama ikibidi. Kila kitu kinajibiwa kwa time frame, auditing haiingiliwi kwamajibu ya papo kwa papo.
 
Hii nchi kila sehemu imeoza. Yaani watumishi wengi wa umma wa ngazi za chini wanakopa benki, na kwenye taasisi za kifedha kwa riba kubwa!

Halafu wengine wanakopeshana tu hela za michango ya watumishi hao hao wa chini, tena kwa vigezo walivyojiwekea wenyewe!!
Inasikitisha mnoo,sijui ni kiongozi gani atakuja kulikomboa hili taifa letu la Tanzania
 
Bima Kwa wote ni nzuri lkn kama ubadhirifu ni kiasi hicho, je NHIF imejipanga vipi Ili kuzuia wizi ubadhirifu na wanachama wapate huduma nzuri ,sio unaenda hospitali unaambiwa dawa hizi kanunue bima haitoi nk?

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Naomba kufahamishwa vizuri. CAG anasema: wafanyakazi wa mfuko wamejikopesha hizo fedha mabilioni ya shilingi, gharama zinazolipwa, hasa kwa hospitali binafsi ni kubwa kuliko uhalisia, mfuko umelipa madawa yaliyoisha muda etc... Sasa wao solution wanasema watanzania wote waingizwe kwenye huu mfuko (NHIF), how? Yaani una wanachama milioni 2 kwa mfano kwenye huo mfuko but umeshindwa kuzikabili changamoto za watu milioni mbili, sasa itawezekanaje kuwamudu watu milioni 60??
 
Hawa VIONGOZI wanyonyaji wanataka kuleta bima ya afya kwa wote.!! ??

Bima ya Afya kwa wote lengo lake ni kuukoa mfuko kama ilivyo kwa KIKOKOTOO.
Mimi ndiyo ninaposhangaa kwamba CAG anasema huu mfuko kwa hawa wanachama wachache na michango yao michache tuu ubadhirifu ni mkubwa, je bima ya afya kwa wote hayo mabilioni au Trilioni si ndiyo watajipigia Mpaka wavimbiwe??
 
Chief acha ujinga😂😂😂😂, mimi sihusiki na NHIF, maisha yangu na ajira wapi na wapi!
Umeamua kuwaruka siyo. Zingatia hoja zetu hawa jamaa ni bomba la kutuibia wala si vinginevyo:

FtP5ui9WwAAcX6v.jpg
 
Back
Top Bottom