kikiboxer
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 3,668
- 9,809
Kwani utaratibu wa sasa ukoje? Mtoto akiwa mdogo au shule anasajiriwa akiwa akiwa mzima wala si mgonjwa, same kwa mfanyakazi na wategemezi wake wote wanakuwa sio wagonjwa. Hata hivyo ukijiunga kama mwanacha binafsi kuna kusubiri miezi kadhaa kabla hujaanza kutumia baadhi ya huduma.changamoto za mfumo wa bima ya afya nchini hasa wa umma haziwezi kupata suluhu kwa kubadilisha bodi au menejiment Au wafanyakazi bila kujua kiini cha tatizo.
Mfumo wa bima ya afya lazima uboreshwe kwa kuweka sera au sheria ambayo itaweka mazingira kwa kila mtanzania kushiriki kuchangia bima ya afya.
Duniani kote hakuna mfumo wa bima ya afya unaoweza ku survive kwa kutegemea wanachama wanaojiunga kwa hiari wakiwa tayari ni wagonjwa.
Suluhu ni kuwa na sheria ya bima ya afya kwa wote au kuondoa makundi yote ya hiari na mfuko kubaki na watumishi wa Umma tu. Kuhusu mikopo, NHIF ni taasisi ya umma inayoendeshwa bila kutegemea ruzuku kutoja Serikalini , mikopo inayotolewa kwa wafanyakzi wake ni sehemu ya motisha kwa wafanyakazi kama ilivyo kwa watumishi wengine wa taasisi za umma na binafsi. Mapato yatokanayo na riba ya mikopo hiyo ya wafanyakazi huwezesha mfuko kupata mapato ya ziada na kujiendesha na kuboresha huduma kwa wanufaika wake.
Mkuu hapa tatizo ni kwenye matumizi ya mfuko ndio hakuna udhibiti sababu ya upigaji na 10%. Kama watu wanalipa huduma hewa unatarajia nini? Watu wanajikopesha hela za wanachama unategemea nini?
Tena unashauri watu wajiunge wote ili michango iwe mingi mtupige vizuri?