CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

Bila shaka mkuu ndo maana amehudumu kama auditor kwa muda mrefu
Kwa hiyo aliweza kuandika diploma ya wiki tatu kwenye CV akasahau kuandika CPA au ACCA.
Saa nyingine mtu unatoa hoja inayokudhalilisha tu bila hata kujijua.
 
Sasa ndio mtakoma watakavyo chota mipesa kesha fanya family members business naona.
 





 
Duu we akili zako wazijua mwenyewe hivi unaelewa ulichokiandika kweli?
 
Tupunguze au tuhifadhi maneno. Fact1: Mkataba wa CAG Assad unakwisha kesho hivyo mtuaji ameamua mafungano na Prof. yaende kimkataba. Sioni kosa liko wapi (sizungumzii dhamira ya mteuaji. Fact 2: Kachere kielimu ana vigezo vya kuwa CAG na ndiye alieteuliwa. Kiongozi humchagua mtu atakaefanya nae kazi na kamuona Kachere anafaa. Katiba inamruhusu kumchagua huyo. Sasa issue ni ya nini.
Kwa likatiba letu hapa mengine yote ni speculation na hisia. Tumuachie Kachere achape kazi huku tukimonitor utendaji wake. Anaweza kuwashangaza, kwani sasa atalindwa na katiba. Hatuna njia nyengine ya kuchagua maCAG. Kama haturidhiki basi tuendelee kudai katiba mpya, mbona wenzetu wakenya nafasi zote nyeti zina usaili wa wazi na si mtu mmoja ana amua.
Prof. nafikiri ata amua kule chuo sasa retirement ni 65 years.
 
That "Diploma in Financial Management of Donor Funded Project" is a joke. It was conducted in 3 weeks, what sort of a diploma is that? I went through the same "course" but I dare NOT tell people of it.


Huo ni Wivu tu!
 
Wafuate hao wakoloni kwani hapo duniani? Kama unawapenda sana!
 
Cheo ni dhamana
Tuntemeke Sanga aliwahi kubadilishiwa wizara saba ndani ya miezi miwili,kidogo ajinyonge lakini alipeta
 
uteuzi wa CAG mpya ni uteuzi ambao unakwenda kuiweka Tanzania katika hali mbaya ya matumizi ya pesa za uma. sasa hapa tutegemea report za kupikwa. tutaambiwa kila kitu kiko perfect wakati kila kitu kiko ovyo.
 
Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Prof.Mussa Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano kwenye nafasi hiyo. Lakini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (ambayo ndio sheria mama) haelezi hicho kinachoitwa "kipindi cha miaka mitano"
_
Katiba inaeleza kuwa CAG atakoma utumishi wake atakapotimiza umri wa miaka 60. Yani akifikisha umri wa miaka 60 anapumzika bila kujalisha ametumikia nafasi hiyo kwa muda gani. Iwe miezi miwili, miaka nane, au miaka kumi.

Ndio maana maCAG wote waliotangulia wameongoza ofisi hiyo kwa vipindi tofauti. Mzee Mohamed Aboud aliongoza kwa miaka 27 tangu 1969 hadi 1996. Thomas Kiama akaongoza kwa miaka 9 tangu 1996 hadi 2005. Ludovick Utouh akaongoza kwa miaka 8 tangu 2006 hadi 2014. Sasa hii kauli ya kusema Assad amemaliza kipindi chake cha "miaka mitano" imetoka wapi?

Matakwa ya kikatiba ni umri wa miaka 60, unless aondolewe kwa kushindwa kutimiza majukumu yake. Na ikitokea hivyo Katiba imeweka utaratibu wa kumuondoa kwa kuunda tume.

Lakini taarifa ya Ikulu inaeleza Assad amemaliza kipindi chake cha miaka mitano. Je hiki kipindi cha miaka mitano Ikulu wamekitoa wapi? Kwenye sheria ipi? Kama ipo sheria hiyo ipo ni batili maana inapingana na katiba.

Na kwa kawaida unapotokea mgogoro kati ya sheria na katiba, basi Katiba ndiyo inayoshika hatamu (When a state law conflicts with a Constitution, then constitution prevails because constitution rules supreme above all state laws).
_
Prof.Assad amezaliwa tar.06 October mwaka 1961. Kwa sasa ana umri wa miaka 58. Atafikisha umri wa miaka 60 October 06 mwaka 2021. Hivyo kwa mujibu wa KATIBA alipaswa kustaafu nafasi yake ya CAG akifikisha umri huo, na si kwa hiki kinachoitwa "miaka mitano". I stand to be corrected.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…