CAG: Stendi ya Magufuli, Kibamba itaongeza foleni ya magari

CAG: Stendi ya Magufuli, Kibamba itaongeza foleni ya magari

CAG amesema stendi ya mabasi ya Magufuli iliyopo Kibamba manispaa ya Ubungo haikuwemo katika usanifu wa ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Ubungo hadi Kibaha.

Kwa maana hiyo stendi ya Magufuli itaongeza msongamano wa magari tofauti na lengo la mradi huo wa barabara la kuondoa kabisa foleni kati ya Ubungo na Kibaha.

Ukinizingua Nitakuzingua!
Hii minne ya mwisho inaweza kuwa vituko na mipasho tu. Sasa CAG hajaona upigaji kwenye ujenzi anahangaika na foleni?!
 
Stand haipo kwenye hifadhi ya barabara isipokuwa ili mabasi kutoka kituoni ni LAZIMA yatasababisha foleni,anachoelezea CAG ni kuwa wakati wa ramani ya mradi wa njia 8 hakukukuwa na hiyo plan ya stand kuwa hapo ilipo hivyo imeleta MWINGILIANO,yamkini kama kwenye ramani wangeambiwa wangejuwa namna ya kufanya.

Ku mjumbe katoa wazo hapa labda waijenge barabara ya mpigi magoe inayopitia magwepande na kutokea bunju ili mabasi ya kaskazini yapite huko na yasiingie kabisa morogoro road.

Kwasasa kama umefanikiwa kuitumia hiyo stand asubuhi utaelewa anachokisema CAG kuna kuwa na foleni sana wakati wanatoka stand.
Nishaitumia kidogo nichelewe basi, maana nilikadiria kutoka kimara stopover mpaka mbezi stendi nisingeweza tumia dak 30, zilizidi hadi 50.
 
Nilishangaa sana uamuzi ule wa hovyo kupata kutokea. Kastendi kwanza kidogo kuhimili mabasi ya mikoani na nje ya nchi. Pia miundombinu ya barabara haiatawanyika kama ubungo. Kisa eti kupisha UDA ya kifisadi iweke stendi Ubungo. Ni kujitoa ufahamu sana.

Kifupi mnaohoji CAT kuoditi kituo ni kwamba kwenye auditing siyo hesabu tu bali kuangalia ufanisi kiutendaji na miongozo ya utejekezaji. Hivyo yuko sawa. Hivyo wanaangalia pia utendaji wa Menejimenti za mihimili yote na Taasisi na wanatoa kitu inaitwa Management Letter yenye hoja zilizoibuliwa na kuhitaji maelezo na utekelezaji wake.
 
Mimi nadhani siyo kila kitu Lazima Serikali iwe inaongea. Kama Hili halikuwa na sababu ya kulitamka, maana wanaweza kulirekebisha vizuri tu, sitaki kuamini kuwa hiki kituo no tatizo kubwa Sana kiasi hicho. Ila shida kila mtu msemaji
Kuliweka wazi kunatoa fursa pana ya kutoa wazo ya nn kifanyike kuepuka tatizo...
Mfano kuna mdau kaeleza ushauri wa kutengeneza bypass kwa baadhi ya maeneo kutokea hapo Mbezi kuliko kutegemea njia moja ili kutoa uwezekano wa uwepo wa foleni...
Hii ni nzuri ili kama wanamacho, masikio, busara na hekima za kupokea ushauri...
Basi wafanyie kazi ili kuondoa usumbufu wa kuja kukosolewa hapo baadaye kama ilivyo/inavyotokea sasa..
 
Pia daraja lililojengwa hapo mloganzila ndilo lilitakiwa likajengwe na pale mbezi ili magari ya goba. Kwenda maramba mawili yapite juu , hii mada ilijadiliwa sana hapa Jf kabla hata ya ujenzi, ila kuna watu humu walijiona mainjinia ati tusubiri hadi pakamilike .
Pale kushakua tatizo sasa hivi,muda mwingine foleni ya kutokea goba kwenda mbezi inaanzia makabe kule
 
...Kwanza KIBAMBA hakuna Stendi ya Magufuli. IPO Mbezi Mwisho.
Na hii ya Mbezi Mwisho hata kwa kuangalia tu kwa macho, ipo NNE Kabisa ya Hizi Njia Name zinapopaswa kuishia!
Hata flyover inayojengwa mbele ya Stand hiyo inathibitisha hili!
Hiyo iliyopo Kibamba ni ipi? Jitahidi kufanya Upembuzi Yakinifu kwanza wa unachotaka kuandika au usikiacho...!
Mkuu mbezi iko jimbo la kibamba I guess
 
Mimi nadhani siyo kila kitu Lazima Serikali iwe inaongea. Kama Hili halikuwa na sababu ya kulitamka, maana wanaweza kulirekebisha vizuri tu, sitaki kuamini kuwa hiki kituo no tatizo kubwa Sana kiasi hicho. Ila shida kila mtu msemaji
Unaijua foleni ya mbezi wewe? Kumbuka kuna kituo cha daladala na mwendokasi pia. Achilia magari ya watu binafsi. Ukishuka Mbezi bus terminsl saa 11 jioni mpaka ufike nyumbani Mbande ni saa 5 usiku. Hapo kuna wa Mkuranga n.k
 
...Kwanza KIBAMBA hakuna Stendi ya Magufuli. IPO Mbezi Mwisho.
Na hii ya Mbezi Mwisho hata kwa kuangalia tu kwa macho, ipo NNE Kabisa ya Hizi Njia Name zinapopaswa kuishia!
Hata flyover inayojengwa mbele ya Stand hiyo inathibitisha hili!
Hiyo iliyopo Kibamba ni ipi? Jitahidi kufanya Upembuzi Yakinifu kwanza wa unachotaka kuandika au usikiacho...!
Huu siyo mtihani meku!
 
CAG amesema stendi ya mabasi ya Magufuli iliyopo Kibamba manispaa ya Ubungo haikuwemo katika usanifu wa ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Ubungo hadi Kibaha.

Kwa maana hiyo stendi ya Magufuli itaongeza msongamano wa magari tofauti na lengo la mradi huo wa barabara la kuondoa kabisa foleni kati ya Ubungo na Kibaha.

Ukinizingua Nitakuzingua!
Hv ni kweli hayo? watatuambia nn mataga waliokuwa wanasifu tu tunahitaji katiba mpya asije akatokea mtu mwingine kama jiwe na kuturudisha nyuma
 
Back
Top Bottom