CAG: Vitabu vya mahesabu vya CHADEMA vina tofauti na kasoro

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu nchini (CAG) amebaini mapungufu katika vitabu vya mahesabu ya CHADEMA na kuhitimisha kwa kuipa CHADEMA hati yenye mashaka ‘Qualified opinion' kutokana na mahesabu yake ya mwaka wa fedha unaoishia June 30, 2012 and June 30, 2013.

Katika macho ya ulimwengu wa mahesabu, hati yenye mashaka (Qualified Opinion) huwa inatolewa pale wakaguzi wanaposhindwa kupata vitabu vyote vya mahesabu na pia wanashindwa kupata maelezo yanayojitosheleza, vile vile vitabu ya mahesabu vilivyopo vinakuwa haviendani na misingi ya mahesabu inayokubalika kimataifa pamoja na kwamba, wakaguzi wanakuwa wamepata ushirikiano na taasisi au kampuni wanayoikagua vitabu vyake vya mahesabu.

1)Pamoja na mambo mengine, katika mwaka wa fedha uliomalizika June 30, 2012, CHADEMA ina akaunti zaidi ya 200, ikijumlisha akaunti za Makao Makuu, Kanda, Mikoa, Wilaya na Majimbo lakini Mkaguzi hakuona salio la kufungia kitabu likihusisha akaunti zote zinazotumia jina la CHADEMA.

2)Mkaguzi anasema katika ripoti hiyo kuwa Chadema kilionyesha kina mali zenye thamani zaidi ya Sh650 milioni, ambazo ni magari, mashamba, nyumba na pikipiki. Hata hivyo, CAG anasema hakuona kitabu cha usajili wa mali hizo.

3)Mahesabu ya mwaka unaoishia June 30, 2013 yalionyesha shilingi milioni 40 ambazo hazikuwa na vitabu vyenye mahesabu ya makusanyo yake.

4) CAG alihoji manunuzi ya magari 10 (Ford Ranger) yaliyofanywa bila kuhusisha Kamati ndogo ya chama inayohusika na utoaji wa zabuni za chama (Tender Committee).

5) CAG alihoji ununuzi wa generator yenye thamani ya shilingi milioni 27 bila kuhusisha mchakato wa zabuni.

6)CAG alihoji pia mahesabu yanayoonyesha deni la milioni 47 linalohusiana na vifaa vya ujenzi wakati hata havijawasili kutoka kwenye kampuni ya kichina.

Kwa habari zaidi,
 
Waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013 ulioasisiwa na Prof. Kitila Mkumbo na pia Samson Mwigamba umekuwa vindicated!

Tujikumbushe tena contents za walaka katika thread hii,


Kuna baadhi ya watu haitashangaza kuwaona wanaaza kulinganisha matatizo ya CHADEMA katika utunzaji wa vitabu vya mahesabu na matatizo ya CCM.

CCM haiwezi kuwa ndiyo kioo cha utendaji cha CHADEMA kama kweli CHADEMA inataka kufanya siasa ambazo ni tofauti na CCM, otherwise labda tukubaliane na Wazanaki watakaosema, CHADEMA na CCM ni manzi ga nyanza!
 
Haya sasa si unaona nilijua tu something was fishy CDM waje walete mahesabu mbele ya umma bila ya kuulizwa? kumbe wanawahi ripoti ya CAG iliyobainisha utapeli; mtu mzalendo kama Zitto kule lazima awekewe mizengwe CDM wanataka blind flowers only.
 
Mnaokoteza vikasoro mtuletee hapa wakati ninyi madudu yenu hayajahesabiwa! Nadhani ya Ccm yakiwekwa hadharani tutaomba dunia ipasuke tujifiche!
 
Oooooh, ni hati zenye "mashaka" na si hati "chafu"..... Hii inamaana kuwa pamoja na mambo mengine makaguzi mkaguzi alishindwa kupata kile alichodhamiria kukipata, Nikwakufichwa,Kujificha au uwezo mdogo wa mkaguzi kushindwa kubainisha hesabu hilo sisi hatujui. Au yawezekana mkaguzi kwa kutambua anaikagua Chadema (chama hasimu wa Ufisadi) alipewa maelekezo ya kuhakikisha analipata kosa lolote lile ili wale "Rafiki wa ufisadi" wapate cha kusema maana wao wanajijua wazi ni mafisadi na Hakika watapata hati chafu...ndiomaana Cag akaishia kutoa hati yenye mashaka baada ya "kushindwa kuliona kosa lolote..!!

Sasa tunaomba wazee wa Ufisadi na wao waweke hesabu zao wazi kama walivofanya Chadema ili tuone kipi ni kipi.. Ninahakika sana Lazima kwakuwa tunaelekea uchaguzi mkuu hapo mwakani ccm itapata hati "Safi" yenye bila mashaka yoyote tena watapewa hadi zawadi na ofisi ya CAG kwa kutunza "Vizuri" hesabu zao,

Tusubiri

BACK TANGANYIKA
 
Aisee. Nilikuwa sijui maana ya waandishi kanjanja. Hivi kweli qualified opinion ni kushindwa kupata taarifa na vitabu? No, hiyo inaitwa disclaimer of opinion.
Audit opinion ziko NNE
1. Unqualified - ya kuridhisha
2. Qualified - yenye Shaka
3. Adverse -
4. Disclaimer - Auditor hakupata taarifa na vitabu
 
Leteni na hizo report za ccm basi tujilidhishe na mapato na matumizi 'yenyu'! Ya cdm tumeona, tumeridhika na ni mwanzo mzuri kwa sababu utamaduni huu haujawai kuwapo ktk vyama vya siasa hasa ccm.....
 

Wape shule kamanda!
 
Nadhani CDM wamejitahidi!!!!kuweka report hii hadharani ni jambo jema sana! Wafanyie kazi mapungufu kama walivyosema! Imekaa poa
Mkuu hii ripoti hawajaweka chadema wenyewe bali imewekwa na baadhi ya wazalendo wao kama chadema waliweka ripoti yao jana ambayo imejaa upotoshaji tofauti na hii zitto alisema chadema kunawizi mtu haruhusiwi kuhoji matumizi ya pesa unaona sasa.
 
Kwahiyo kwako wewe yenye shaka ni sawa haina shida?
 
Wachaga kwa wizi tu hamjambo kwani hizo pesa mlizaliwa nazo?
 

[h=2]DEFINITION of 'Unqualified Opinion'[/h] An independent auditor's judgment that a company's financial records and statements are fairly and appropriately presented, and in accordance with Generally Accepted Accounting Principles (GAAP). An unqualified opinion is the most common type of auditor's report.

Unqualified Opinion Definition | Investopedia
 
Kwahiyo kwako wewe yenye shaka ni sawa haina shida?

[h=2]DEFINITION of 'Qualified Opinion'[/h] A statement written upon the front page of an audit done by a professional auditor. A qualified opinion suggests that the information provided was limited in scope and/or the company being audited has not maintained GAAP accounting principles.
 
Mbona kelele nyingi, hebu tuwewawazi nini kimetokea kwenye halmashauri zilizopata hati chafu mfululizo,
maana naona CDM hawajapata hati chafu, na
vipi kuhusu chama tawala, taarifa yao iko wapi, mbona hatuiona hapa mtandaoni au wamepiga mkwara mzito wasikaguliwe? Wenye habari tuhabarisheni hasa wale wa pale Lumumba tupeni taarifa kinachoendelea huko
 
Mkuu hii ripoti hawajaweka chadema wenyewe bali imewekwa na baadhi ya wazalendo wao kama chadema waliweka ripoti yao jana ambayo imejaa upotoshaji tofauti na hii zitto alisema chadema kunawizi mtu haruhusiwi kuhoji matumizi ya pesa unaona sasa.

Siasa pigeni wenyewe!Mimi mwananchi wa kawaida najua kwamba CDM wamefanya vizuri angalau kwa kukaguliwa achilia mbali ripoti yenyewe!
 
Lazima hesabu zigome kuna zile hela alizokopa katibu nyingine mwenyekiti alipowauzia mafuso hewa na nyingine za kumlipa girlfriend kuinstall antivirus kwny kompyuta na ule mpango wa dubai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…