KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ameitaka Ofisi ya Rais TAMISEM kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kwa watumishi waliohusika na upotevu wa fedha za mapato ya ada za leseni, ikiwa pamoja na kuhakikisha jumla ya Sh. Milioni 45.99 zinarejeshwa kutoka kwa watumishi husika na kuwasilishwa katika akaunti ya Halmashauri.
Katika Ripoti yake ya ukaguzi wa Tawala za Mikoa ya serikali za mitaa mwaka 2021/22, CAG alifanya ukaguzi maalumu wa fedha za mapato yanayotokana na ada za leseni za biashara kwa kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2022 na kubaini uwepo wa upotevu wa fedha.
CAG amesema kuwa alibaini kati ya leseni 5,352 alizohakiki, leseni 596 zenye jumla ya Sh. Milioni 45.99 zilitolewa kwa wafanyabiashara bila ya malipo yake kuwasilishwa Halmashauri kupitia benki, huku kati ya kiasi hicho Sh. Milioni 33.81 zinatokana na leseni 423 zilizotolewa kwa wafanyabishara bila ya kulipa kiasi chochote katika akaunti ya Halmashauri.
Mbali na hilo CAG alibaini Sh. Milioni 21.37 zilizotolewa kwa wafanyabiashara waliolipa jumla ya Sh. Milioni 9.19 pekee.
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anasema kuwa kutowasilishwa kwa fedha benki kunatokana na na kukosekana kwa uhaminifu baina ya watumishi wa halmashauri hiyo kupokea fedha toka kwa wafanyabiashara na kutumia shughuli zao binafsi na kupelekea Halmashauri kupata hasara ya Sh. Milioni 45.99.