Cameroon: Mpinzani wa Paul Biya akimbilia uhamishoni Gambia

Cameroon: Mpinzani wa Paul Biya akimbilia uhamishoni Gambia

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon, Issa Tchiroma Bakary, amekimbilia nchini Gambia kwaajili ya usalama wake kufuatia mvutano uliotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba, ambao ulimrejesha madarakani Rais Paul Biya katikati ya maandamano yenye vurugu.

Serikali ya Gambia imethibitisha kuwa Tchiroma aliingia nchini humo tarehe 7 Novemba kwa misingi ya 'kibinadamu', ili kuhakikisha usalama wake wakati mazungumzo ya kutafuta suluhu ya amani kuhusu mivutano ya baada ya uchaguzi yakiendelea.

1763970398244.png


Rais Biya, ambaye ametawala Cameroon kwa miaka 43, aliapishwa hivi karibuni kwa muhula wake wa 8 kufuatia uchaguzi ulioibua maandamano makubwa na ukandamizaji uliopelekea vifo vya waandamanaji kadhaa.

Akiwa na umri wa miaka 92, Biya ndiye kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani anayeongoza taifa akiwa madarakani. Kwa mujibu wa matokeo rasmi, Biya alipata asilimia 53.7 ya kura, huku Tchiroma akipata asilimia 35.2.

Hata hivyo, Tchiroma anapinga matokeo hayo, akidai kuwa yeye ndiye mshindi wa kweli wa uchaguzi huo. Ametangaza wazi kuwa Cameroon ina Marais Wawili. Alinukuliwa akisema "sasa kuna marais wawili – rais aliyechaguliwa na wananchi wa Cameroon (mimi) na rais aliyeteuliwa na Baraza la Katiba (mnayemfahamu).” Ameendelea kuhimiza wafuasi wake kupinga matokeo ya uchaguzi kwa njia mbalimbali.

Baada ya taarifa za vifo vya watu waliouawa na vikosi vya usalama wakati wa kukandamiza maandamano kabla na baada ya tangazo la ushindi wa Biya, Tchiroma aliwataka wafuasi wake kufanya operesheni ambazo zinahusisha kufunga maduka na kusitisha shughuli nyingine zote za umma kama njia ya kuonyesha kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi.

Serikali ya Cameroon imesema inapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Tchiroma kutokana na kile ilichokiita “wito wake wa mara kwa mara wa uchochezi na jaribio la kuandaa uasi.”

Tangu uhuru wa nchi hiyo kutoka Ufaransa mwaka 1960, Biya amekuwa mtu wa pili pekee kuiongoza Cameroon, akitawala kwa kiimla na kukandamiza upinzani wa kisiasa na wa Kijeshi
 

Attachments

  • 1763970246674.png
    1763970246674.png
    925 KB · Views: 31
Masheikh Bakwata na wahadhiri wao hapo watasema huo ni ukandamizaji wa mfumo kristo.
 
Biya mwenyewe yupo anaongoza nchi toka Nchi nyingine ,hayupo Cameroon...sasa anamkimbia nani?
 
Akiwa na umri wa miaka 92, Biya ndiye kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani anayeongoza taifa akiwa madarakani. Kwa mujibu wa matokeo rasmi, Biya alipata asilimia 53.7 ya kura, huku Tchiroma akipata asilimia 35.2.
Haka ka Haiti kamewang'ang'ania wa Cameroon mpaka basi!
 
Back
Top Bottom