Cami vs vitz vs Sienta vs spacio

Fuqin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2018
Posts
306
Reaction score
625
wadau naombeni ushauri kati hizi gari 4 ipi ni nzuri... uimara, ulaji mafuta,show nzuri mbele ya jamii
 
show nzuri mbele ya jamii
Ondoa hii zana.
Itakurudisha nyuma.

----------
C & P
Mwandishi: Makirita Amani

Macho Ya Wengine Ndiyo Yanayokutesa...

Kama ungekuwa unaishi porini, wewe peke yako na hakuna mtu mwingine yeyote unayekutana naye, unafikiri ungesumbuka kama unavyosumbuka sasa.

Unafikiri ungejali sana kwamba unavaa nini, unaendesha nini, unakaa wapi na hata unafanya nini?

Kwa hakika usingesumbuka, ungeweka mkazo wako kwenye nini ufanye ili uendelee kuwa hai.
Macho ya wengine ndiyo yanayokutesa, kutaka kuwaridhisha wengine ndiyo kunakufanya uwe na maisha magumu.

Kujilinganisha na wengine, kutaka na wewe uonekane upo au unaweza kufanya vitu fulani ndiyo kunakufanya uwe mtumwa kwenye maisha yako.

Watu wengi wanaoingia kwenye mikopo isiyozalisha, huwa siyo kwa ajili yao, bali kwa ajili ya wengine, kutaka nao waonekane wapo.

Tafakari hili kwenye kila unachojisukuma kufanya, jiulize je unafanya kwa ajili yako au ili uonekane na wengine. Kama msukumo pekee ni uonekane na wengine, basi jua unajitesa, unaacha kuishi maisha yako na mbaya zaidi, hao unaofanya vitu kwa ajili yao, wala hawajali sana kuhusu wewe.

Chagua kuishi kwa ajili yako, chagua kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwako na fanya kwa umakini na usahihi. Usijitese kwa ajili ya wengine.
 
shukran sana.. ila sina maana mbaya... nakusudia machoni kwangu pia nilione zuri
 
Unalihitaji la kufanyia nini,
Ukubwa wa familia?
Una mizigo kiasi gani
Unaenda umbali gani
Bajeti yako?
kutembelea hapa hapa town Dar.
tupo 4
sina mizigo
town trip
Milioni 10 tu.
 
Unalihitaji la kufanyia nini,
Ukubwa wa familia?
Una mizigo kiasi gani
Unaenda umbali gani
Bajeti yako?
kutembelea hapa hapa town Dar.
tupo 4
sina mizigo
town trip
Milioni 10 tu.
 
Spacio iko poa ya cc 1490 lkn usije ingia cha kike kuna kubwa na ndogo
 
Spacio ndo jibu kwa hapo.
Jitahidi isizidi cc 1500
Nakuongezea IST old model
 
Kama ni machoni kwako.. Wewe ndio mtu pekee wa kujua nini unaitaji na kwa wakati gani
 
Kwenye Vits hutojutia spare, mafuta na uchakavu wa body.
Pia Toyota Spacio nayo inavumilia na kwa mafuta kidogo chukua Spacio ya 1298cc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…