Can Myopia be cured bila ya kuvaa miwani

Can Myopia be cured bila ya kuvaa miwani

mwl frank

R I P
Joined
Jul 11, 2011
Posts
78
Reaction score
27
Siku za karibuni kumejitekeza tatizo la kuvaa miwani kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 hasa walio shuleni,nini chanzo chake hasa na ni kipi cha Kufanya ili kutopata taabu hii?

Wataalamu okoeni kizazi hiki.

=============================

Habar zenu wakuu,

Nina sumbuliwa na uono hafifu ni mwaka wa saba sasa huu navaa mawani yenye lense ya minus 5 na
sioni mabadiliko yoyote ya kuboreka kwa uono wangu.

Ni njia gani nitumie kuweza kuboresha uono wangu na vitu gani ni epukane navyo ili kuzui tatizo kuwa kubwa.

Computer screens causes ultra radiation inturn damages the retina. It is recommended to fix radiation filters ontop of the screens or otherwise use LCDs.
 
siku za karibuni kumejitekeza tatizo la kuvaa miwani kwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 hasa walio shuleni,nini chanzo chake hasa na ni kipi cha kufanya ili kutopata taabu hii?wataalamu okoeni kizazi hiki.

Mtoto wangu wa pili anazaliwa 2004 na baada ya kuanza kutembea mwaka 2005 mwaka 2007 alianza kuvaa miwani tena ile yenye lenzi ya balaa na amepewa pale KCMC idara ya macho yani kwa kweli ilinitouch sana lakini sikuwa na namna zaidi ya kukubali masharti na mpk sasa kila mwaka lazima tumpeleke kliniki pale mara moja kwa mwaka naye amezoea utafikiri amezaliwa nazo,yani hili tatizo nimejaribu kuwauliza na majibu wananiambia wameridhi sasa kwetu na hata kwa wakwe wangu hakuna hata mtu yeyote anayevaa miwani. YANI NIMEMWACHIA MUNGU AFANYE MIUJIZA MAANA NAAMINI ANAWEZA!
 
pole sana mr/mrs Liverpool,mie wawili wote ni watumiaji wa hii miwani wakati wazazi wao yaani sisi,babu/bibi zao pande zote hawajawahi kutumia miwani hadi uzeeni wanasoma bila miwani! ndugu yetu mtimkavu na wengineo mnasemaje?
 
Habar zenu wakuu,

Nina sumbuliwa na uono hafifu ni mwaka wa saba sasa huu navaa mawani yenye lense ya minus 5 na
sioni mabadiliko yoyote ya kuboreka kwa uono wangu.

Ni njia gani nitumie kuweza kuboresha uono wangu na vitu gani ni epukane navyo ili kuzui tatizo kuwa kubwa.
 
Habar zenu wakuu,

Nina sumbuliwa na uono hafifu ni mwaka wa saba sasa huu navaa mawani yenye lense ya minutes 5 na
sioni mabadiliko yoyote ya kuboreka kwa uono wangu.

Ni njia gani nitumie kuweza kuboresha uono wangu na vitu gani ni epukane navyo ili kuzui tatizo kuwa kubwa.

Mkuuu inamaana na mm nitafika huko??? Ulianza na minus ipiii??? Nimeshituka sana😯
 
Habar zenu wakuu,

Nina sumbuliwa na uono hafifu ni mwaka wa saba sasa huu navaa mawani yenye lense ya minutes 5 na
sioni mabadiliko yoyote ya kuboreka kwa uono wangu.

Ni njia gani nitumie kuweza kuboresha uono wangu na vitu gani ni epukane navyo ili kuzui tatizo kuwa kubwa.

Una umri gani na je uliambiwa una myopia au unahisi kuwa unayo?
 
Ulipima hospitali gani na je unaona vizuri karibu huku ukiwa huoni vizuri mbali au huoni vizuri karibu na mbali?

nilipima tinnah optical clinic au wanajulikana kama shumahofa siuoni vizur mbali na kila muda unavyoenda uono wangu wa kuona karibu unazid kufifia
 
Mkuu hizi mewani nazo huwa zinaongeza tatizo.Jitahidi kutafuna karoti au kunywa jwisi yake.Pia kula sana spinach.

Kuna uthibitisho upi kuwa miwani inaongeza tatizo?

Matatizo ya uono wa mbali na karibu yanaweza kurekebishwa kwa upasuaji(surgery) ila madaktari wanashauri uvae miwani kwa kuwa hakuna ulazima wa kufanya upasuaji ambao kwa watoto na vijana sio mzuri ingawa wanaweza kufanya hivyo kama kuna uhitaji.
 
Daah! Mkuu hiyo namba ni kubwa sana, pole aisee....wataalam wa masuala ya macho toeni ushauri ,nahisi huenda wengine wanye tatizo kama lake wakafaidika na ikawa msaada kwa wengi
 
nilipima tinnah optical clinic au wanajulikana kama shumahofa siuoni vizur mbali na kila muda unavyoenda uono wangu wa kuona karibu unazid kufifia

Myopia ni tatizo la kutoona vizuri vitu vilivyoko mbali.

Astigmatism ni tatizo la kutokuona vizuri masafa yote, mbali na karibu. Huenda ukawa na astigmatism ila hayo matatizo yote yanarekebishwa kwa kuvaa lens kama unayovaa na kuna matibabu ya upasuaji.

Kuna LASIK na LASER surgery inayoweza kukuondolea tatizo hilo ila kwa kuwa umri wako ni mdogo ndio maana umeshauriwa kutumia miwani.

Kama uko Dar es salaam nenda hospitali ya CCBRT ipo msasani kuna wataalam watakusaidia.

Kuna matibabu ya dawa za mimea(asilia) kuna matabibu unaoweza kuwaona wakakusaidia kama Dr. Isack ndodi na wengine ambao unaweza kuulizia hapa jamii forum.
 
Kuna watu alienda kufanyiwa upasuaji CCBRT ikawa ni upofu kabisa
 
Back
Top Bottom