Canada, China, Mexico wajiandae dhidi ya Trump

Canada, China, Mexico wajiandae dhidi ya Trump

Mkuu una tatizo kwenye kuangalia uchumi. 15% ya export yako unaona ni sehemu ndogo ya uchumi? 500bln USD unaona ni pesa ndogo kweli. Unafikiri ni mamilioni mangapi ya ajira ndani ya China yanategemea hiyo export ya 500bln usd? Kwenye biashara China anamtegemea US kuliko US anavyomtegemea China.
Kitu ambacho hujaelewa asilimia kubwa ya hizo exports kwenda USA ni malighafi za viwanda sio finished products.
China akisema agome na yeye Kuna viwanda vingi USA vitasimama uendeshaji maana cheap quality raw materials zinatoka China.
 
Hiyo 15% ni upande wa Marekani kwenye importation zake

Lakini hiyo 500 bln ya Marekani ni 2% tu ya GDP ya China

Kusema China anaitegemea Marekani sio sahihi kabisa.

Tuseme mataifa yote yanaamua yasinunue bidhaa za mwenzake unajua kuwa

Export ya Marekani kwenda China peke yake ni sawa na 7.5% ya total ya exports.

Hili nalo unalizungumziaje? Kuna ajira ngapi kwenye hiyo 7.5% zitapotea na viwanda vingapi vinavyotegemea crucial components na parts kutoka China vitashindwa kuzalisha?
 
Acha upotoshaji. Sehemu kubwa ya export ya China kwenda USA, zaidi ya 90% ni finished products. Malighafi gani China inaiuzia US?
 
Hiyo 15% ni upande wa Marekani kwenye importation zake

Lakini hiyo 500 bln ya Marekani ni 2% tu ya GDP ya China

Kusema China anaitegemea Marekani sio sahihi kabisa.

Tuseme mataifa yote yanaamua yasinunue bidhaa za mwenzake unajua kuwa

Export ya Marekani kwenda China peke yake ni sawa na 7.5% ya total ya exports.

Hili nalo unalizungumziaje? Kuna ajira ngapi kwenye hiyo 7.5% zitapotea na viwanda vingapi vinavyotegemea crucial components na parts kutoka China vitashindwa kuzalisha?
Tafiti vizuri. 15% ya export ya China inaenda USA. Na nyingine 16% inaenda EU. Na huwezi tu ukasema 500bln ni 2% ya GDP wakati hiyo export ya 500bln inazalisha mamilioni ya ajira ndani ya China na kuwa na effect kubwa kwenye GDP ya China kuliko kusema kirahisi 2%
 
Kwa hiyo 500 bln kwa value ya GDP ya uchumi wa China ni asilimia ngapi mkuu?
  • Je, umefikiria Marekani hata ikisema haiagizi bidhaa kutoka China nayo itaathirika jinsi gani?​
  • Na China ikisema haigaizi bidhaa za Marekani unajua Marekani nayo itaathirika jinsi gani?​
Mbona hizo hoja 2 unazikimbia sana?

Wewe si mchumi njoo tudiscuss hizo hoja 2
 
GDP ni thamani ya goods and services zilizozalishwa na kutolewa ndani ya nchi kwa kipindi husika. Huwezi chukua thamani ya export na kuiweka kama percent ya GDP wakati export ina multiplier effect. Hiyo export ya 500bln haiishii hapo. Inakuza skta ya usafiri wa anga. Bandari. Mahoteli. Ishu zingine za logistics na vitu vingine kibao. Mchango wake kwenye GDP hauishii kwenye 500bln tu ya bidhaa zilizouzwa.

Nimisha kuambia. China anamtegemea zaidi US. Ndiyo maana unaona US anampiga China mikwara ya tariffs kila siku. China ikikosa kuuza US uchumi wake unaweza kucollapse. Lakini US akikosa kuuza au kununua kutoka China uchumi wake hauwezi kucollapse. Na ndiyo maana unaona US ana kiburi cha kuanzisha tariffs war.
 
Na ndiyo maana unaona US ana kiburi cha kuanzisha tariffs war.
Mzee tariffs ni hidden tax sio Wachina wanayolipia ni Wamarekani ndiyo wanailipia wanapotumia bidhaa za China.

Kwa hiyo Trump akiongeza tariffs kwanza anawaumiza tu raia wanaonunua finished goods kutoka China

Pili, manufacturers wa Marekani wanaponunua raw materials, components na parts kutoka China watakapotengeneza bidhaa zitapanda bei kwa hiyo mwisho wa siku anayeumia ni final consumer aliyeko Marekani
 
Mzee tariffs ni hidden tax sio Wachina wanayolipia ni Wamarekani ndiyo wanailipia wanapotumia bidhaa za China.

Kwa hiyo Trump akiongrza tariffs kwanza anawaumiza tu raia wanaonunua finished goods kutoka China

Pili, manufacturers wa Marekani wanaponunua raw materials, components na parts kutoka China watakapotengeneza bidhaa zitapanda bei kwa hiyo mwisho wa siku anayeumia ni final consumers
Inafahamika. Lengo ni kufanya bidhaa za wachina ziwe bei juu ndani ya Marekani na hivyo kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka China. Na labda kuwezesha uzalishaji wa ndani. Marekani anamtishia China habari za tariffs kwa sababu kwenye biashara yao China ndiyo mwenye kufaidika zaidi, ndiyo mwenye trade surplus.
 
Wamarekani wenyewe wanakiri ni vigumu sana kukimbia bidhaa za China

Hata wakiagiza bidhaa kutoka mataifa mengine kama Mexico na Vietnam bado hayo mataifa yanaitegemea China kupata materials, components na parts za kutengeneza bidhaa za kuexport Marekani.

Na kama haitoshi pia Mchina amewekeza kwenye hayo mataifa. Na ndiyo sababu unaona Trump anasema ataongeza tariffs kwa bidhaa za Mexico kwa sababu nyingi ni investment ya makampuni ya China yaliyowekeza Mexico.

Kwa hiyo zinaingia Marekani kupitia mataifa ambayo ni kama 3rd party. Kwa kifupi Marekani anaruka majivu anakanyaga moto

Soma hii ripoti ya serikali ya Marekani ya Federal Reserve.

Halafu uje uniambie kati ya Marekani na China nani anamhitaji zaidi mwenzake. Msipende kuongea kishabiki.

Sehemu ya ripoti ilisema hivi:

The most important U.S. suppliers increased their own reliance on Chinese goods

In the remainder of the note, we document that the increase in China's share of U.S. suppliers' imports reflect two factors. First, the most important U.S. suppliers have increased their own reliance on Chinese imports. Second, the U.S. has imported more from countries that have stronger trade ties with China. Later, we also show evidence suggesting that rerouting of Chinese goods toward the U.S. through other countries was quite limited.
Ila isome yote uongeze uelewa ujionee Marekani hawezi kumkimbia Mchina

Achana na maneno ya wanasiasa angalia uhalisia wa uchumi wa Marekani unavyotegemea China

Na labda kuwezesha uzalishaji wa ndani.
Kwa supply chain gani aliyo nayo Marekani?

Mpaka leo mfano tu defense contractors na watengenezaji wa vifaa vya electronic na bidhaa nyingine Marekani wanategemea suppliers kutoka China.

Marekani hana supply chain ya kuweza kutengeneza components muhimu za kulisha utengenezaji wa bidhaa zake za viwandani bila mkono wa Mchina

20240711_102556.jpg

Defense contractors wa Marekani wanaitegemea sana China
 
Marekani anamtishia China habari za tariffs kwa sababu kwenye biashara yao China ndiyo mwenye kufaidika zaidi, ndiyo mwenye trade surplus.
Hata Marekani ifanyaje haitaweza kuondoa trade deficit kwenye biashara na China. Marekani inaihitaji China
 
Nachojua biashara kati ya wawili kuna faida na mkisitisha miamala kati yenu lazima wote muathirike
 
Kwa supply chain gani aliyo nayo Marekani?

Mpaka leo mfano tu defense contractors na watengenezaji wa vifaa vya electronic na bidhaa nyingine Marekani wanategemea suppliers kutoka China.

Marekani hana supply chain ya kuweza kutengeneza components muhimu za kulisha utengenezaji wa bidhaa zake za viwandani bila mkono wa Mchina

View attachment 3163521
Defense contractors wa Marekani wanaitegemea sana China
Siyo kwamba hana, waliudumuza ili wachache wapige hela
 
Yeye Trump na Wamarekani wamejiandaaje na ongezeko la bei za bidhaa kutoka hizo nchi wakiimport? Naona watakuwa wanajiumiza wenyewe

Kwa sasa soko la Marekani linachangia 2% tu ya GDP ya China ambayo ni sawa na $500 bln katika uchumi wa China ambao ni $18 trillion.

Kwa hiyo kiuchumi China wala haimshtui. Miaka 6 iliyopita alifanya hivyo hakuna alichofanikiwa.

Waswahili walisema mfa maji haachi kutapatapa ndipo Marekani alipofikia kwenye ushindani na China

Na wakati huohuo Marekani ndiyo anaongoza kwa kuimport bidhaa kutoka China. Sasa nani anamtegemea mwenzake zaidi?

Najua kwa Mexico ni kwa sababu kuna investment nyingi za China zinazoingia Marekani kupitia Mexico kama 3rd part
Well said. Rais wa Mexico amemwambia Trump apambane na watu wake waache kutumia madawa ya kulevya.
 
Well said. Rais wa Mexico amemwambia Trump apambane na watu wake waache kutumia madawa ya kulevya.
Umesema vyema

Trump anaionea wivu Mexico kwa sababu ya jinsi China imewekeza sana hapo Mexico. Na ikumbukwe Mexico ni biggest trade partner wa Marekani kwa hiyo bidhaa nyingi za makampuni ya China zinaingia Marekani kupitia Mexico ikiwa kama third party

BYD wana mpango wa kufungua kiwanda Mexico, Trump kwenye kampeni zake alishasema hayo magari ikiwa yataingia Marekani kutoka Mexico atayawekea tariffs kubwa

La sivyo hizo kampuni za Kichina zikafungue factories Marekani ili zisikumbane na hilo rungu la tariffs atakapokuwa raisi.

Alichokifanya sasa kwa Mexico tulikitegemea ndicho alichosema kwenye kampeni zake

20240729_012402 (1) (1).png
 
GDP ni thamani ya goods and services zilizozalishwa na kutolewa ndani ya nchi kwa kipindi husika. Huwezi chukua thamani ya export na kuiweka kama percent ya GDP wakati export ina multiplier effect. Hiyo export ya 500bln haiishii hapo. Inakuza skta ya usafiri wa anga. Bandari. Mahoteli. Ishu zingine za logistics na vitu vingine kibao. Mchango wake kwenye GDP hauishii kwenye 500bln tu ya bidhaa zilizouzwa.
Kwa hiyo kusoma kwako kote uchumi haujawahi kusoma kuhusu export to percentage of GDP?

Mbona hii calculation kiuchumi inafahamika mzee. Haujawahi kuona, angalia hapo analysis ilivyofanyika

20241127_212421.jpg
 
Hata Marekani ifanyaje haitaweza kuondoa trade deficit kwenye biashara na China. Marekani inaihitaji China
Unaangalia mambo kinyumenyume. Mwenye trade surplus ndiye anayemhitaji mwenye deficit. China ambaye anauza sana Marekani kuliko anavyonunua ndiye anamhitaji zaidi Marekani.
 
Back
Top Bottom