Habari wana Jamii Forum….
Leo napenda kushare na ndugu zangu nyinyi mambo kadha wa kadha juu ya uhamiaji,
Najua Tanzania tuna watu wengi sana wanapenda kufanya kazi nje, pia ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu, na pia hata walioajiriwa bado hawana tofauti na wasio na ajira(wao pia hulalamika Maisha magumu) afadhali yao na wasio ajiriwa ni moja tu WAMERIDHIKA.
Tanzania ukitaka uenjoy Maisha na ajira hakikisha unakua “single”, usiwe na mtoto, wala usiwe na wanaokutegemea yaani pesa yako ni wewe tu, HAKIKA utafurahia kidogo ulambishwacho.
- Daktari analia hana ajira na mshara hautoshi
- Engineer nao wanalia
- Manesi na wakunga wanalia
- Wachumi nao wanalia etc etc
Ndugu zangu tuchangamkieni fursa za uhamiaji (INFORMATION IS A POWER) ninayoandika hapa jitahidi ufanye mwenyewe kama utaweza.
CANADA wameongeza “list” ya kuhitaji nguvu kazi katika nchi yao, ni kweli wanahitaji, Watanzania tuchangamke ndugu zanguni, Wahindi wanatumia hizi fursa sana sasa hivi wnaruhusiwa kujiunga na Jeshi kwa walio na Ukazi wa kudumu na hata kingereza ni tatizo ila wanatoboa
View attachment 2419005
View attachment 2419006
Ukifika hapa NAKUHAKIKISHIA baada ya miaka 4 toka umefika tu wewe sio huyo, yaani nyumbani utarudi kutalii tu, mfn ($ in CAD)
- mshahara wa Dotka kwa mwaka (general doctor) ni $260,000.00
- Mfamasia $90,000 per year.
- Nurse $75,000 per year.
- Engineer $109,000 CAD
- Teacher $70,000
- Truck driver $45,000 per year
- Carpenter $43,100 CAD per year.
- Mmwaga zege $45,187
- Mpiga rangi $38,400
- Kibarua wa ujenzi $38,026
- IT $100,000
Hapa kuna child support ni
- $6,997 per year ($583.08 per month) for each eligible child under the age of 6
- $5,903 per year ($491.91 per month) for each eligible child aged 6 to 17
Hapo huduma za kijamii zote ni uhakika kwa 100%, kwa hapa swala la afya ni changamoto kidogo, Madaktari ni wachache kuliko watu, kwa afya 60%, unaweza Kwenda kumuona daktari saa 3 asubuhi ukatoka saa 10 jioni, hadi umeenda kwa daktari wewe unaumwa kweli, wengi naona huwa wanaenda kutibiwa kwao au wengi wanaenda DUBAI.
Hivi mtu una GPA ya 3.5+ unalia Tanzania,wakati wewe ni lulu kwa Jirani.
Unatakiwa vitu wiwili 2 tu, 1. Nenda British counsil pale kafanye IELTS score band 7+ hakikisha unajiandaa kweli, usiende kupoteza 700,000 yako, Pili unatakiwa uwe na
“Educational credential assessment (ECA)” hii ni kama
TZS 550,000 ndani ya miezi 5 unakua tayari kwa kuomba “Ukazi wa kudumu”
Watakuja wazee wanaochaji watu
TZS 10,000,000 kuwaombea kusema nimekurupuka, bado kuna vitu vingi, hivo vitu vingi kikubwa ni Pesa ya kuonyesha unaweza kuishi mwaka mmoja ambacho wanataka
CAD 12,000 sawa na
TSH 17,000,000.00 uonyeshe bank (kwa mfanya kazi wa serikali unakopa unaweka bank, kuna wazazi wana pesa wanaweza kuwapa Watoto wao), wengineo anzeni na hivyo vya juu kwanza kuna njia za wahindi wanatumia, nitawaeleza wakati mwingine.
Watakuja tena watu ukiwa na hiyo pesa si bora ubaki bongo, utatoboa,
BONGO KUTOBOA MPAKA UIBE na RUSHWA
Siku ukiwa na IELTS 7band nitakuelekeza jinsi ya kuomba LCA, ambayo ni wewe, chuo na Ubalozi wa Canada, malipo unalipoa kwa kadi wala USIJE HANGAIKA LIPA MAMILIONI KUFANYIWA wakati ni vitu rahisi.