Canada yahitaji zaidi watu (soma)

Canada yahitaji zaidi watu (soma)

Hayo mkaratasi yako ya mzumbe na udsm mwisho airport,ukifika Canada hawayatambui lazima urudi darasani,kwenye elimu wacanada wako strictly sana Kuna mdada ailingia na degree ya nursing ya muhimbili university,aliambiwa hana sifa za kuwa nurse kaishia kufanya kazi za care sikukatishi tamaa
alingiq na degree ya nursing
Kuna mitihani wana fanya na kuwa certified, registered nurse. So anaweza fanya hizo kazi za care huku anasoma apate licence. Inawezekana na akifudhu tu hapo aliowaacha huku tz anawapiga gape mara 20 kwa kipato.

Hata accountant, anaweza jiongeza kuaoata certification huko na akafanya kazi.!
 
Aisee ndoto zangu zitatimia kumbe,Mungu ajaalie ,mkuu nikipata 4m inatosha nauli,pakuanzia kukaa ntakuomba unitaftie[emoji18]naomba namba yako ya WhatsApp ya Canada pls .
Changamkia fursa , fanyia kazi malengo yako..!
Usisikilize sauti za kukukatisha tamaa.. iwe implicitly, au kutoka kwa watu wengine...
Kile unachoona ni risk kubwa kwako kwa wengine ni jambo la kawaida sana...!
 
Hii kitu ipo kweli and true watu wanaenda. .hatahizo English test sio ishu km unajua kiingereza. ..ishu kubwa inayowapa changamoto wengi ni salio. ..hakuna kitu kigumu mjini km unahela...tafuta km 5mil ya process zote hapo juu unaingia kule bala shida
Elezea hizo process na ichambuwe hiyo 5mil namna gani itatosha kufika Canada
 
Habari wana Jamii Forums,

Leo napenda kuwashirikisha ndugu zangu ninyi mambo kadha wa kadha juu ya uhamiaji.

Najua Tanzania tuna watu wengi sana wanapenda kufanya kazi nje, pia ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu, na pia hata walioajiriwa bado hawana tofauti na wasiyo na ajira (wao pia hulalamika maisha magumu). Afadhali yao na wasiyoajiriwa ni moja tu wameridhika.

Tanzania ukitaka ufurahie maisha na ajira hakikisha unakua 'single', usiwe na mtoto, wala usiwe na wanaokutegemea, yaani pesa yako ni wewe tu. Hakika utafurahia kidogo ulambishwacho.
  • Daktari analia hana ajira na mshara hautoshi.
  • Injinia nao wanalia.
  • Manesi na wakunga wanalia.
  • Wachumi nao wanalia n.k.
Ndugu zangu tuchangamkieni fursa za uhamiaji (information is power), ninayoandika hapa jitahidi ufanye mwenyewe kama utaweza.

Canada wameongeza orodha ya kuhitaji nguvu kazi katika nchi yao, ni kweli wanahitaji, Watanzania tuchangamke ndugu zanguni, Wahindi wanatumia hizi fursa sana. Sasa hivi wnaruhusiwa kujiunga na Jeshi kwa walio na ukazi wa kudumu na hata Kingereza ni tatizo ila wanatoboa.

View attachment 2419005
View attachment 2419006

Ukifika hapa nakuhakikishia baada ya miaka 4 toka umefika tu wewe siyo huyo, yaani nyumbani utarudi kutalii tu, mfano ($ in CAD)
  • Mshahara wa daktari kwa mwaka (general doctor) ni $260,000.00.
  • Mfamasia $90,000 kwa mwaka.
  • Nesi $75,000 kwa mwaka.
  • Injinia $109,000 CAD.
  • Mwalimu $70,000.
  • Dereva wa lori $45,000 kwa mwaka.
  • Fundi seremala $43,100 CAD kwa mwaka.
  • Mmwaga zege $45,187.
  • Mpiga rangi $38,400.
  • Kibarua wa ujenzi $38,026.
  • IT $100,000.
Hapa kuna 'child support' ni;
  • $6,997 kwa mwaka($583.08 per month) kwa kila mtoto anayestahiki chini ya miaka 6.
  • $5,903 kwa mwaka ($491.91 per month) kwa kila mtoto anayestahiki mwenye miaka 6 mpaka 17.
Hapo huduma za kijamii zote ni uhakika kwa 100%, kwa hapa swala la afya ni changamoto kidogo, madaktari ni wachache kuliko watu kwa afya 60%. Unaweza kwenda kumuona daktari saa 3 asubuhi ukatoka saa 10 jioni, hadi umeenda kwa daktari wewe unaumwa kweli, wengi naona huwa wanaenda kutibiwa kwao au wengi wanaenda Dubai.

Hivi mtu una GPA ya 3.5+ unalia Tanzania,wakati wewe ni lulu kwa jirani?!

Unatakiwa vitu wiwili 2 tu;

1) Nenda British Counsil pale kafanye IELTS score band 7+ hakikisha unajiandaa kweli, usiende kupoteza 700,000 yako,

2) Unatakiwa uwe na “Educational credential assessment (ECA)” hii ni kama TZS 550,000 ndani ya miezi 5 unakua tayari kwa kuomba “Ukazi wa kudumu”.

Watakuja wazee wanaochaji watu TZS 10,000,000 kuwaombea kusema nimekurupuka, bado kuna vitu vingi. Hivyo vitu vingi kikubwa ni pesa ya kuonesha unaweza kuishi mwaka mmoja ambacho wanataka CAD 12,000 sawa na TSH 17,000,000.00, uoneshe benki (kwa mfanya kazi wa serikali unakopa unaweka bank, kuna wazazi wana pesa wanaweza kuwapa watoto wao), wengineo anzeni na hivyo vya juu kwanza kuna njia za wahindi wanatumia, nitawaeleza wakati mwingine.

Watakuja tena watu ukiwa na hiyo pesa si bora ubaki bongo, utatoboa, Bongo kutoboa mpaka uibe na rushwa

Siku ukiwa na IELTS 7band nitakuelekeza jinsi ya kuomba LCA, ambayo ni wewe, chuo na Ubalozi wa Canada. Malipo unalipia kwa kadi, wala usije hangaika lipa mamilioni kufanyiwa wakati ni vitu rahisi.
Mtaibiwa fedha zenu bure. Matapeli wengi wa kihindi na wengine wanatumia matangazo kama haya kuwaibia watu. Kanada ina upungufu wa kazi kwa kiwango cha aslimia kama tano na saba hivi. kwa habari zaidi soma hii The Daily — Labour Force Survey, November 2022
 
Nendeni jaman hio nchi inahitaji nguvu kazi last week nina rafiki yangu ameenda huko na mambo taratibu yanaanza kufunguka
 
Back
Top Bottom