Can't you Love Someone with all your eyes Clear?

Can't you Love Someone with all your eyes Clear?

SnowBall

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Posts
3,052
Reaction score
2,842
Wanabodi salama?

Najua ni BLUE MONDAY..lakini sio issue sana mradi jamvi lipo naamini hakuna kinachoharibika... Kumekuwepo na 'myth' kwamba LOVE IS BLIND...ikimaanisha kuwa mara nyingi mapenzi ni UPOFU..na unapokuwa unampenda mtu huwezi kuona hata yale yanayoonekana kwa wenzio (kwa wale waabudu limbwata mtanisamehe..hapa naongelea mapenzi yasiyo na catalyst yeyote....)

Gwiji wa miondoko laini (blues) Michael Bolton katika wimbo wake wa 'WHEN A MAN LOVES A WOMAN anasema hivi..na hapa namquote
..when a man loves a woman deep down his soul she can bring him such misery...
If she's playing him for a fool, he's the last one to know..LOVING EYES CAN NEVER SEE

Sasa hapa ndio najiuliza hivi ni kweli 'loving eyes can never see'?....hebu EMT, Mtambuzi , snowhite , gfsonwin , King'asti , BADILI TABIA , AshaDii , Dark City , saudari , lara 1 , nivea , Mr Rocky Eiyer na wengineo wote nisaidieni hapa..Nataka nione at the same time nipende....

Karibuni..........
 
Last edited by a moderator:
kaka mkubwa heshima kwako.

kwanza kabisa when we say love eyes never see huwa tunamaanisha kwamba jicho la kuona huwa halion mapungufu ya apendwae.

it is true that if you see every thing by its color huwez kumpenda unayempenda manake waweza kukuta dosari ndogo sana na ikakurudisha nyuma but , kinachotokea ni kwamba jicho la nyama huona hata ubaya wa mwenza wako ila jicho la moyoni husema hii siyo big deal as utaweza kumanage upungufu huo.

labda nikupe mfano, mkeo sio mwanamke mzuri kuliko wanawake wote duniani hadi ukamuoa wala hakuwa mwanamke aliyekamili kuliko wote hadi ukamchumbia ila ni mwanamke pekee aliyeuteka moyo wako kiasi kwamba hukuona mwingine anayeweza kukufanya ukawa kamili ila yeye.
 
SnowBall, mapenzi ni upofu pale umpendapo mtu kwa dhati hivyo inakuwia vigumu kuona kwingine,
yaani hautaweza kuona kwingine zaidi, utabaki kumpenda yule umpendae na hivyo kuwa kama kipofu.

Upofu unaosemwa sio upofu wa kutokuana bali ni upofu wa kuto kupendapenda ovyo.
 
ukipenda unaona but unakubali kuona na kukubali unachokiona!
kwa mtu asiyependa huishia kutazama hawaoni!

ma dear love you mingi sanaa!

back to the topic, si kwamba macho ya mpendaji hayaoni mwali, ila huwa yanaona na yanakubali yanachokiona kisha macho ya rohoni yakaona upande wa tofauti na ule unaoona kwa jicho la nyama. hapo sasa ndipo maskio ya rohoni husemezeshwa na akili ya mpendaji juu ya kwann anampeda muhusika na atayakabili vipi.
 
ukipenda unaona but unakubali kuona na kukubali unachokiona!
kwa mtu asiyependa huishia kutazama hawaoni!

Nakubaliana na wewe,

Halafu kuna upofu wa muda pale mambo yanapoanza...ila baada ya hapo upofu unatoweka na mtu anakubali matokeo.....

Nafurahia kukubali matokeo kuliko kujidanganya au kuanza kuruka ruka bila hakika kama mtu anajua kweli anakotaka kwenda....!!

Babu DC!!
 
I love what l see!
But l choose what to see and what not to see, and it doesn't mean that l am blind!

Hapa umetuchanganya na lugha Kaunga,

Hebu tufanyie digestion kidogo ili tukupate....

Yaani unamaanisha kuwa macho yako yana control tower ambayo inayachagulia uelekeo na target??

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
kaka mkubwa heshima kwako.

kwanza kabisa when we say love eyes never see huwa tunamaanisha kwamba jicho la kuona huwa halion mapungufu ya apendwae.

it is true that if you see every thing by its color huwez kumpenda unayempenda manake waweza kukuta dosari ndogo sana na ikakurudisha nyuma but , kinachotokea ni kwamba jicho la nyama huona hata ubaya wa mwenza wako ila jicho la moyoni husema hii siyo big deal as utaweza kumanage upungufu huo.

labda nikupe mfano, mkeo sio mwanamke mzuri kuliko wanawake wote duniani hadi ukamuoa wala hakuwa mwanamke aliyekamili kuliko wote hadi ukamchumbia ila ni mwanamke pekee aliyeuteka moyo wako kiasi kwamba hukuona mwingine anayeweza kukufanya ukawa kamili ila yeye.

Hiyo concept ya mwanamke/mwanamume pekee inanipa taabu kidogo...

Sijui kama variables nyingine kama vile location, time, uchumi na kupigika vimeingizwa kwenye equation...lol!!

Babu DC!!
 
Hapa umetuchanganya na lugha Kaunga,

Hebu tufanyie digestion kidogo ili tukupate....

Yaani unamaanisha kuwa macho yako yana control tower ambayo inayachagulia uelekeo na target??

Babu DC!!
babu kama sikosei alichoandika fellow rev mother wangu hakina tofauti na nilichoandika mimi!
tukipenda tuona,tunachagua cha kuona na tunakubali kuona tunachokiona na mwisho tunapenda kile tunachokiona!
 
Hapa umetuchanganya na lugha Kaunga,

Hebu tufanyie digestion kidogo ili tukupate....

Yaani unamaanisha kuwa macho yako yana control tower ambayo inayachagulia uelekeo na target??

Babu DC!!

Mpaka kuwa naye maana yake nimempenda (I love what l see)
Pia nina machaguo ya kuamua nione sana nini au nisione nini, ninaweza nikaona SANA ucheshi wake na kuamua kuacha kuona ucareless wake. As binadamu ukichagua kuONA kitu chochote utakiona kwani unakikuza (magnify) kwa lenzi. Kuwa na machaguo ya nini unataka kuona si upofu bali ni degree kubwa sana ya VISIBILITY in my opinion.
 
huko mtaani utasikia "huyu naye kampendea nini huyu dada/kaka?"
wewe mwenyewe unaona umejiibulia gold yako.........
ukweli ni kwamba siyo unakuwa kipofu kipofu...... unakubaliana na yaliyopo na kuyachukulia kwa muonekano chanya.
 
babu kama sikosei alichoandika fellow rev mother wangu hakina tofauti na nilichoandika mimi!
tukipenda tuona,tunachagua cha kuona na tunakubali kuona tunachokiona na mwisho tunapenda kile tunachokiona!

Mpaka kuwa naye maana yake nimempenda (I love what l see)
Pia nina machaguo ya kuamua nione sana nini au nisione nini, ninaweza nikaona SANA ucheshi wake na kuamua kuacha kuona ucareless wake. As binadamu ukichagua kuONA kitu chochote utakiona kwani unakikuza (magnify) kwa lenzi. Kuwa na machaguo ya nini unataka kuona si upofu bali ni degree kubwa sana ya VISIBILITY.

Nimewakubali wadogo zangu.....

May be week end ilikuwa bado inanishupalia....

Haya twende kazi.....

Babu DC!!
 
Mpaka kuwa naye maana yake nimempenda (I love what l see)
Pia nina machaguo ya kuamua nione sana nini au nisione nini, ninaweza nikaona SANA ucheshi wake na kuamua kuacha kuona ucareless wake. As binadamu ukichagua kuONA kitu chochote utakiona kwani unakikuza (magnify) kwa lenzi. Kuwa na machaguo ya nini unataka kuona si upofu bali ni degree kubwa sana ya VISIBILITY.
SnowBall kuja uone hapa thread ako klozed! Kaunga enh!sasa mi naachaje kukupa bichwa sasa!?
 
Last edited by a moderator:
Umesema maneno mazito sana mamaangu...
Na hapa ndipo wakati mwingine tunashindwa kutambua yanayoonekana...kwa sababu 'udhaifu' wa mweznio unaonekana kama 'strength'...nakubali kuwa mapenzi yana kawaida ya kuficha usione udhaifu lakini je? kuishi kwa kujilisha upepo hakuwezi kuwa kubaya zaidi?..kwanni hata ukimpenda mtu usione mapungufu yake na kujaribu kuyaishi au kuyarekebisha ikibidi??

....it is true that if you see every thing by its color huwez kumpenda unayempenda manake waweza kukuta dosari ndogo sana na ikakurudisha nyuma but , kinachotokea ni kwamba jicho la nyama huona hata ubaya wa mwenza wako ila jicho la moyoni husema hii siyo big deal as utaweza kumanage upungufu huo.

labda nikupe mfano, mkeo sio mwanamke mzuri kuliko wanawake wote duniani hadi ukamuoa wala hakuwa mwanamke aliyekamili kuliko wote hadi ukamchumbia ila ni mwanamke pekee aliyeuteka moyo wako kiasi kwamba hukuona mwingine anayeweza kukufanya ukawa kamili ila yeye.
 
Mkuu saudari hapa ungefafanua zaidi bwana..
Manake kuna upofu wa kutokuona mabaya ya mwenzio na siku zote unakuwa unaona mazuri tu...japo siku ukiachana naye unagundua 'how worse she was'...

SnowBall, mapenzi ni upofu pale umpendapo mtu kwa dhati hivyo inakuwia vigumu kuona kwingine,
yaani hautaweza kuona kwingine zaidi, utabaki kumpenda yule umpendae na hivyo kuwa kama kipofu.

Upofu unaosemwa sio upofu wa kutokuana bali ni upofu wa kuto kupendapenda ovyo.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo concept ya mwanamke/mwanamume pekee inanipa taabu kidogo...

Sijui kama variables nyingine kama vile location, time, uchumi na kupigika vimeingizwa kwenye equation...lol!!

Babu DC!!

Babuuu variables nyingine zote zina remain constant as at first site what matters ni mapenzi.

kwani wewe ulipomuoa bibi alikuwa ndo mwanamke ama binti bora na mzuri kuliko wote uliopata kuwaona??
 
Ni Maoni yangu tu, naweza kuwa wrong; hivyo mjadala unafaa uendelee! You are always sweet, you know that; maana siku zote unachagua kuona vitu vizuri tu kwangu na kuyaignore madudu yangu kibao!
and thats a very high degree of my visibility sio!santeeee!
 
Back
Top Bottom