Mkuu, Ukijibu haya Maswali tunaweza kupata Strategy itayobakisha wateja na bei ukaongeza na bado ukauza.
1. Hao wateja ulionao ni wale wananunua ili nao wakauze(WAUZAJI) au wale wananunua ili watumie (WATUMIAJI au final users)?
2. Hizo bidhaa unazouza ni Unazitengeneza mwenyewe, Unaziingiza Nchini mwenyewe au Unazinunua hapahapa na kuongeza bei kidogo kisha unauza?
3. Bidhaa/huduma mnayotoa ni Mpya Sokoni au tayari ipo siku nyingi? Endapo tayari ilikuwepo, Je, Strategy mliyowapata hao wateja mlionao, mlitumia UBORA WA BIDHAA YENU(quality) au MLISHUSHA BEI ILIYOKUWEPO SOKONI(Price)?
USHAURI GENERAL.
Watanzania wengi hatuna mbinu mpya ya kuingia sokoni tofauti na kushusha bei. so kama na nyie mlitumia hio mbinu ya kitanzania kujipatia wateja mlionao, basi MKIONGEZA bei ni LAZIMA mtawapoteza WOTE. Na mkipandisha bei, atatokea Mtanzania mwingine atashusha bei kama kawaida na atawachukua wateja wenu. Unless kama mlitumia QUALITY ili muuze ndio mnaweza jadili kupandisha bei. Otherwise FALSE.
Asante.