Kama Watanzania Taifa la watu wenye UTU(humanity) tumefikia mahali hapa kufurahia kifo cha mtu na kushangilia basi ninasikitika sana KWELI ninasikitika sana, Marehemu Captain John Komba ni mwanadamu kama sisi na kama wanadamu wengine ana mazuri yake na mabaya yake ana mema na mapungufu siyo VEMA hata kidogo kumtukana Marehemu na kufurahia kifo chake! Hebu jiulize mwenyewe kama Captain Komba angekuwa mzazi wako au ndugu yako watu wakawa wanafurahia kifo chake ungejisikiaje? Kuingia msituni kupinga serikali tatu ni mtazamo wake maana anaona mapungufu ya serikali tatu na madhara yake na ninyi mnaopinga serikali mbili mna mitazamo yenu na mnaona mapungufu ya serikali mbili na madhara yake(hiyo ni mitazamo) na inatakiwa kupingana kwa hoja na tofauti zenu za mitazamo iwe ndiyo umoja wenu kama taifa la watu wenye utu na hoja siyo kutukana na kujengeana uadui, hakuna anayejua salio halisi la maisha yake! Komba amefariki but who's next? Labda mimi au wewe! Hivyo tuepuke kutoa majibu emotional maana si VEMA kwa kiongozi kuongozwa na hisia, wengi mmeonyesha hisia za chuki huku mkijinadi kama mbadala wa utawala uliopo I can tell you that the situation will worsen than now because you guys don't think like actual leaders! Act and live like a righteous leader even though you're not in the system, Nimesikitishwa sana na kifo cha ndugu yetu Captain John Komba alikuwa mwimbaji mzuri na mhamasishaji mzuri sana wa yale anayoyaamini, Mungu amrehemu na kumpumzisha, AMEN