Bukwabi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 3,352
- 1,148
Muwaambie CCM waache kutupeleka mistuni na kutuacha huko nusu wafu! Hivi nikuulize swali; je yule mama muuza pombe aliyeuawa kule Ilula kwenye purukushani ya Polisi kusaka watu wanaokunywa pombe saa za kazi ili kumfurahisha mtoto wa mkulima angekuwa mzazi wako ungejisikiaje!? Halafu hiyo pombe saa za kazi kwani walianza kunywa siku ile ya purukushani na msako!? Siku zote mnawatafutiaga pesa ya kula nyie!? Polisi walitumwa na nani!? Walianzisha msako ili kumfurahisha pinda!? Wacheni huo upuuzi wenu!? Wengi tunaumizwa na dhuluma inayofanywa na CCM!
Swala hapa sio nani anatenda nini. Kifo cha mtu kinaleta masikitiko makubwa kwa anaowaacha, tunaposhangilia eti kwa kuwa fulani kafa, kwa upande wowote kwa hizi zinazokinzana, hapo ndipo tunapopotoka kwa kukiuka misingi ya utu kama jamii. Hakuna anayemtetea mtu ati kwa kuwa anatoka kwenye chama fulani au kundi fulani.
SUALA HAPA UTU UMEPOTEA MIONGONI MWETU!