Hii ilikuwa ni Range Rover Vogue L322 ambayo ina engine ya BMW 4.4L V8.
Gari iligoma kuwaka ghafla, inakaa switch on ila ukiwasha ni kama starter motor imeungua au relay yake imekufa, yaani hata husikii chochote.
Fundi wa Kwanza alibadilisha Neutral safety switch au wengine wanaita selector switch. Ambayo ni kama hii hapa chini.
Hiyo switch ilibadilishwa na tatizo likawa bado lipo.
Wakaamua kuunga waya kwenye negative terminal ya Starter motor, halafu wakawa wanawasha kwa kugusisha ule waya kwenye bodi la gari. Na wameitumia hivyo mpaka baadae ilipokuja kugoma kuwaka kwa njia hiyo tena.
Nilipoenda kuipima haikuonesha code yoyote kwenye engine lakini Transmission Control Unit ilikuwa hairespond kabisa. Kama vile haijachomekwa tu.
Nilijaribu kuangalia data za mifumo miwili ambayo ni immobilizer na Transfer case(TCCM) na nilichokikuta kilikuwa kama ifuatavyo.
Kwenye Immobilizer ilikuwa hivi
1. Key status ilikuwa valid.
2. Gear status ikawa inaonesha ipo kwenye gear ( japo gear lever position ilikuwa ni parking).
3. Ukiangalia pale mwisho Starter motor inaonesha ipo Blocked(Disabled).
Kwenye Transfer case ilikuwa hivi
Ukiangalia hapo kwenye gear lever position inaonesha ipo Reverse. Kwa maana gari isingeweza kuwaka as gari huwakia kwenye Parking au Neutral tu.
From there nikapima fuses na Relays na kila kitu kikawa poa, Nikapima nyaya za Control ya Gearbox nazo zikawa poa.
So kilichofuata ikawa kubadili control unit ya transmission na kununua starter motor mpya ambapo ile ya mwanzo iliungua kama matokeo ya ule waya waliounga kwenye negative terminal wakawa wanawashia gari kienyeji.
CASE CLOSED.