Car diagnostic solutions

Car diagnostic solutions

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Hii thread ni maalumu kwa ajili ya results zote ambazo nitakuwa nazipata baada ya kufanya diagnosis kwenye magari. Nitakuwa napost screenshots za hizo codes pamoja na hatua mbalimbali nilizozipitia katika kutatua natatizo hayo.

MUHIMU: Kama tatizo limetatuliwa kwa njia fulani, haimaanishi kwamba kila siku litatatuliwa kwa njia hiyo. Unaweza ukakutana na matatizo matano ya aina tofauti na ukayatatua kwa njia 5 tofauti. Tumia akili.

Kama utakuwa Impressed na njia ambazo tunatumia kudiagnose na kurekebisha matatizo, basi tuwasiliane 0621 221 606 Nipo Dar Magomeni, Mwembechai.
 
Hii ilikuwa ni Range Rover Vogue L322 ambayo ina engine ya BMW 4.4L V8.

images (3).jpeg


Gari iligoma kuwaka ghafla, inakaa switch on ila ukiwasha ni kama starter motor imeungua au relay yake imekufa, yaani hata husikii chochote.

Fundi wa Kwanza alibadilisha Neutral safety switch au wengine wanaita selector switch. Ambayo ni kama hii hapa chini.

images (1).jpeg


Hiyo switch ilibadilishwa na tatizo likawa bado lipo.

Wakaamua kuunga waya kwenye negative terminal ya Starter motor, halafu wakawa wanawasha kwa kugusisha ule waya kwenye bodi la gari. Na wameitumia hivyo mpaka baadae ilipokuja kugoma kuwaka kwa njia hiyo tena.

Nilipoenda kuipima haikuonesha code yoyote kwenye engine lakini Transmission Control Unit ilikuwa hairespond kabisa. Kama vile haijachomekwa tu.

Nilijaribu kuangalia data za mifumo miwili ambayo ni immobilizer na Transfer case(TCCM) na nilichokikuta kilikuwa kama ifuatavyo.

Kwenye Immobilizer ilikuwa hivi

Screenshot_2021-06-15-09-12-56-151_com.us.thinkdiag.plus.png


1. Key status ilikuwa valid.

2. Gear status ikawa inaonesha ipo kwenye gear ( japo gear lever position ilikuwa ni parking).

3. Ukiangalia pale mwisho Starter motor inaonesha ipo Blocked(Disabled).

Kwenye Transfer case ilikuwa hivi

Screenshot_2021-06-15-09-14-19-345_com.us.thinkdiag.plus.png



Ukiangalia hapo kwenye gear lever position inaonesha ipo Reverse. Kwa maana gari isingeweza kuwaka as gari huwakia kwenye Parking au Neutral tu.

From there nikapima fuses na Relays na kila kitu kikawa poa, Nikapima nyaya za Control ya Gearbox nazo zikawa poa.

So kilichofuata ikawa kubadili control unit ya transmission na kununua starter motor mpya ambapo ile ya mwanzo iliungua kama matokeo ya ule waya waliounga kwenye negative terminal wakawa wanawashia gari kienyeji.

CASE CLOSED.
 
Sasa gari za miaka ya kina mzee Mwiru hii njia ni rafiki kweli

Kila kitu kina upside na downside.

Gari za zamani hazina majanga majanga mengi. Ila kwa mfano likitokea tatizo kama la hapo juu kwenye hiyo Range unaweza kuhangaika sababu hautokuwa na namna ya kupima.
 
images%20(6).jpg


Hii nimeidiagnose week iliyopita. Ni Toyota IST ya mwaka 2002. Gari haikuwasha taa yoyote kwenye Dashboard ila ilikuwa na Dalili zifuatazo.

1. Kuwaka huku idle speed(sailensa) iko juu sana. Mshale unaweza kuwakia hata kwenye 3 au zaidi.

2. Kukosa nguvu.

3. Gari ilikuwa haivuki speed 80Km/h.

Tulipopima tu ikaja hiyo code P1656 - OCV circuit(Bank 1).

Screenshot_2021-06-28-16-30-32-297_com.us.thinkdiag.plus.jpg


OCV ni kufupisho cha Oil Control Valve, kwa majina mengine unaweza kuiita VVT solenoid (Haiitwi VVTi sensor kama watu wengi waljvyoibatiza.)

Straight forward hiyo code inamaanisha hiki kitu kimeharibika au nyaya zake zimekatika au kuna waya wake umegusa bodi. [emoji116][emoji116][emoji116]

images%20(5).jpg


So tulifungua hiyo solenoid, Tukaitest na ikaonekana haifanyi kazi tena. Pia sehemu yake ambayo ndio inaingia connector ya umeme palikuwa pameugwa na paliachia wakati bado tunaendelea kuhangaika nayo. Wire zilikuwa fresh hiyo ikawa inahitajika inunuliwe hiyo VVT solenoid nyingine.

So tulibadilisha ishu zote zikawa solved.

Mwenye hiyo gari ndio kwanza alikuwa ametoka kuinunua mkononi na hakuweza kujua kama taa ya check engine wameshaichezea.

Ingawa ilikuwa ukiweka Switch ON taa ya check engine inawaka lakini ukishawasha gari hata uchomoe sensor yoyote ile taa haiwaki. Hiyo hiyo taa walishaichezea na probably waliiungia kwenye taa ya Oil kama wengi wanavyofanya.

Anyway

Kama una tatizo na gari lako au unahitaji gari lako lifanyiwe Diagnosis au Check up kiujumla nicheck 0621 221 606. Nipo Dar Magomeni, Mwembechai.
 
Chief kwa laki tano naweza pata diagnosis mashine nzuri kwa matumizi ya nyumbani, gari jamii ya Toyota corolla hizi.. ist, spacio, Raum etc


US $187.44 34%OFF | THINKCAR Thinkscan Plus S7 Lifetime Free Optional 5 Resets Car Diagnostic Tool ECM/TCM/ABS/SRS/BCM/IC System OBD2 Auto Scanner

Try this
 
images%20(12).jpg


Leo tupo kwenye Toyota Corolla Axio ya mwaka 2006 ikiwa na engine ya 1nz na gearbox ya 5 speed CVT.

Tulireset CVT gearbox na kucalibrate CVT oil pressure.

Ile kuanza tu kuendesha ikawa imewasha check engine na ikaleta code hii hapa.[emoji116][emoji116][emoji116]

Screenshot_2021-07-04-13-41-14-528_com.us.thinkdiag.plus.jpg


P1589 Acceleration sensor learning Value.

Hata ukiangalia mtandaoni sababu ni hizi. [emoji116][emoji116][emoji116]


Screenshot_2021-07-04-15-11-45-884_com.android.chrome.jpg



Gari za kisasa nyingi, Sensor zake huwa zinakuwa na learned values ambazo kama ukifanya baadhi ya vitu kwenye gari huwa zinafutika hivyo mpaka uziset na upya.

To cut the story nmecalibrate acceleration sensor na taa ya check engine ikazima.

CASE CLOSED.
 

Attachments

  • Screenshot_2021-07-04-15-11-45-884_com.android.chrome.jpg
    Screenshot_2021-07-04-15-11-45-884_com.android.chrome.jpg
    42.9 KB · Views: 26
Toyota IST ncp61 (1490 CC)

Iliwahi kukosa kabisa nguvu kwenye kilima chochote kile.

Nikapeleka kwenye diagnosis machine. Haikuona any diffect. Yaani mashine ikatoa majibu kuwa mifumo yote ya gari ipo OKAY!

Nikaenda kwa fundi wa chini ya mwembe. Akaendesha gari kuicheki kwenye kilima kidogo.

Fasta jamaa akasema hiyo ni eksozi imejaa/imeziba masega. Na kweli baada ya kuyaondoa masega kwenye eksozi, gari ilirudi kama mpyaaa, full power.

Swali: Je, hizi diagnosis machines hazina uwezo wa kudect tatizo kwenye mfumo wa eksozi?

Mkuu JituMirabaMinne .
 
Hii thread ni maalumu kwa ajili ya results zote ambazo nitakuwa nazipata baada ya kufanya diagnosis kwenye magari. Nitakuwa napost screenshots za hizo codes pamoja na hatua mbalimbali nilizozipitia katika kutatua natatizo hayo.

MUHIMU: Kama tatizo limetatuliwa kwa njia fulani, haimaanishi kwamba kila siku litatatuliwa kwa njia hiyo. Unaweza ukakutana na matatizo matano ya aina tofauti na ukayatatua kwa njia 5 tofauti. Tumia akili.

Kama utakuwa Impressed na njia ambazo tunatumia kudiagnose na kurekebisha matatizo, basi tuwasiliane 0621 221 606 Nipo Dar Magomeni, Mwembechai.


UPDATES

☆ Baada ya week ijayo tutakuwa na material special kwa ajili ya kucover wires za gari. Hivyo kupunguza madhara ya moto ambayo mara nyingi husababishwa na wire ambazo zipo uchi (naked).

View attachment 1886159
 
Back
Top Bottom