Car diagnostic solutions




Toyota Allex yenye engine ya 1NZ-FE inaenda 6Km/L.

Haijawasha Check engine ila tulivopima imekuja P0100 na P0110. 90% hiyo P0100 inaweza kuwa sababu.

Japo zimetajwa sensor mbili hapo ila zote mbili zinakaa kwenye Housing moja.
 
Nissan Note mkuu
Basi mkuu, nilikuwa nina wasiwasi inafanana na mbili hivi niko nazo za xtrail qr20, jamaa alikuwa nazo mpya akanipa gari yangu(xtrail yd22) haziingiliani.
Nimeicheki haifanani, ila kwa mbaali inafanana na ya kwangu, ila yangu chini ina kibati..

Hii yako meno mangapi?
 
Hii yangu ina pini tatu mkuu...haiingiliani na xtrail...tulishaangalia ya xtrail
 
Mkuu vipi mtu anaweza kukucheki ukaenda kukagua gari ikiwa kwa mfano nainunua kutoka mikononi mwa mtu kujua ikiwa ipo sawa au ina tatizo lolote JituMirabaMinne
 
Nissan Xtrail Toleo la kwanza (NT30). Ukiiwasha inawasha Check engine inawaka kama hivyo...





Report Baada ya kuipimia ikaonesha P0340 CMP sensor circuit Bank 1 pamoja na P1123, ECT motor Relay/ Circuit.
Tukaziclear zote mbili na tukatry kuendesha kipande kirefu tu Check engine haijawaka tena.

Baada ya kurudi tukasema tuichomoe CMP sensor tuiangalie. Tumekuta Connector imejaa Oil.

Yaani Oil inatoka ndani kwenye engine inapita kwenye sensor inajaaa kwenye connector.

Japokuwa ukiiangalia connector kwa nje imejaa vumbi na haina dalili ya Oil.

Tumeisafisha tumeirudishia kwa matazamio. Kama Oil itaendelea kulick kuja kwenye connector basi sensor itakuwa ni ya kubadili.



Camshaft position sensor location.



Nissan QR20DE engine




Kama unahitaji Diagnosis na Repair ya gari lako. Tupigie 0621 221 606.
 
Mkuu JituMirabaMinne ,

Kwenye ajari Gari ikablast airbags zote mbili (ya kwenye steering na ya upande wa abiria). Airbags huwa zina replacement? ama zinarudishwa airbags zile zile zilizokuwepo?

If ni replaceable, je kuna vifaa vingine zaidi vya kureplace sambamba na hizo airbags?

Kuhusu mikanda je, nayo pia inakuwa replaced? mikanda imekuwa loose.
 

Kwa harakaharaka

1. Airbag zote mbili inabidi zije mpya

2. Seatbelt zote mbili zije zingine

3. Pretensioner za Seatbelt


Vipo na Vingine ila kwa uhakika ni mpaka kupima maana magari yanatofautiana. Kuna vitu kama Crash sensors n.k. nazo huwa sometimes za kununua, so inategemea na aina ya gari Boss.
 



Mfano hiyo ilikuwa Nissan Dualis niliipimaga mwezi wa 8, Jamaa alitaka ila tukanote ilipata ajali na jamaa wamezima Taa ya Airbag.

Hiyo screenshot ya diagnosis inaonesha baadhi tu ya vitu vya kubadili, ila vinaendelea hapo. Ndo maana nikasema uhakika zaidi hadi kupima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…