View attachment 1833694
Hii nimeidiagnose week iliyopita. Ni Toyota IST ya mwaka 2002. Gari haikuwasha taa yoyote kwenye Dashboard ila ilikuwa na Dalili zifuatazo.
1. Kuwaka huku idle speed(sailensa) iko juu sana. Mshale unaweza kuwakia hata kwenye 3 au zaidi.
2. Kukosa nguvu.
3. Gari ilikuwa haivuki speed 80Km/h.
Tulipopima tu ikaja hiyo code P1656 - OCV circuit(Bank 1).
View attachment 1833697
OCV ni kufupisho cha Oil Control Valve, kwa majina mengine unaweza kuiita VVT solenoid (Haiitwi VVTi sensor kama watu wengi waljvyoibatiza.)
Straight forward hiyo code inamaanisha hiki kitu kimeharibika au nyaya zake zimekatika au kuna waya wake umegusa bodi. [emoji116][emoji116][emoji116]
View attachment 1833696
So tulifungua hiyo solenoid, Tukaitest na ikaonekana haifanyi kazi tena. Pia sehemu yake ambayo ndio inaingia connector ya umeme palikuwa pameugwa na paliachia wakati bado tunaendelea kuhangaika nayo. Wire zilikuwa fresh hiyo ikawa inahitajika inunuliwe hiyo VVT solenoid nyingine.
So tulibadilisha ishu zote zikawa solved.
Mwenye hiyo gari ndio kwanza alikuwa ametoka kuinunua mkononi na hakuweza kujua kama taa ya check engine wameshaichezea.
Ingawa ilikuwa ukiweka Switch ON taa ya check engine inawaka lakini ukishawasha gari hata uchomoe sensor yoyote ile taa haiwaki. Hiyo hiyo taa walishaichezea na probably waliiungia kwenye taa ya Oil kama wengi wanavyofanya.
Anyway
Kama una tatizo na gari lako au unahitaji gari lako lifanyiwe Diagnosis au Check up kiujumla nicheck 0621 221 606. Nipo Dar Magomeni, Mwembechai.