Binafsi miaka miwili iliyopita nilikuwa simkubali Aishi Manula kutokana na mapungufu yake ktk kulilinda lango,
Lakini kiukweli ameimprove sana hivi karibuni, amekuwa nguzo muhimu ktk idara ya goalkeeping kuanzia Simba mpaka Starz.
Yale mapungufu yake hasa katika udakaji mipira ya juu, kuzicheza krosi, kona na fouls yamepungua kwa kiasi kikubwa sana
Na katika michuano ya CAF-CL mpaka mzunguko wa mechi nne unaisha ni magolikipa wawili tu waliocheza dakika nyingi zenye clean sheet, Ahmed Reda Tagnaouti wa Wydad Casablanca ya Morroco alipo Msuva na Aishi Salum Manula.
Kongole sana AirManula