Case File 1: Mwanaume aliyekodi watu ili kumuua mkewe wakiwa Honeymoon (True Story) Part 1

jerrytz

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
5,975
Reaction score
4,266
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 maisha yalikuwa yakienda vizuri kwa dada aliyejulikana kama Ani Hindocha, mwenye asili ya India ambaye alizaliwa na kulelewa nchini Sweden.
Akiwa amemaliza shahada ya Engineering na alikuwa amepata kazi katika kampuni ya Erricson kama Mwandisi wa umeme katika kampuni hii kubwa ya vifaa vya umeme.
Mwaka 2009 shangazi yake na Ani anayeishi London akamtambulisha Ani kwa kijana wa kiume anayeitwa Shren Diwani aliyekuwa na miaka 29. Shren Diwan alikuwa anaisha Bristol nchini Uingereza, kama ilivyo kwa Ani, huyu kijana alizaliwa Uingereza lakini wazazi wake walikuwa na asili ya India.

Baada ya mawasiliano ya miezi kadhaa, Ani akiwa Sweden na Shren akiwa Uingereza ndipo Ani akaamua kwenda kutembea nchi Uingereza kwa shangazi yake lakini akiwa na matumaini ya kuonana na Shren.
Alipofika Uingereza ndipo wawili hao wakakutana kwa mara ya kwanza, baada ya siku kadhaa, Shren akaomuomba Ani kuwa awe mpenzi, mchumba na kuahidi kuwa anataka awe mke wake kabisa.
Ani alifurahia sana kukutana na Shren na ilionekana wazi kuwa vijana hawa wawili wanapendana kwa dhati.

Tarehe 10 June 2010, Shren alifika Sweden na kumpeleka Ani katika jiji la Paris na huko alimpatia zawadi kadhaa ikiwemo gauni ya thamani, pete almasi (diamond) yenye thamani Paundi 25000 na hereni za dhahabu. Wakiwa Paris Shren alimpeleka Ani kwenye hotel maarufu na ya gharama ya Ritz.
Mwaka 2010 mwezi Oktoba Shren na Ani wakafunga ndoa ya kifahari nchini India katika mji wa Mumbai, inakadiriwa kuwa familia zote mbili zilitumia kiasi cha Paundi 250,000 kwa ajili ya harusi hii.

Baada ya harusi, Shren akapanga honeymoon (Fungate) ikafanyike nchini Africa Kusini. Japokuwa Shren alipendelea honeymoo ikafanyike Dubai.
Hatimaye siku ya Jumanne tarehe 9 November 2010 wanandoa Ani na Shren,wakawasili katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya kusini. Shren alikuwa ameshafanya booking katika hotel inayojulikana kama Chiduachidua Safari Lodge yenye hadhi ya nyota tano, hii ipo ndani ya Hifadhi maarufu ya Krugger national Park. Wakatumia siku tatu kuona wanyama na kufanya utalii katika Hifadhi ya Klugger.

Ijumaa ya tarehe 12 November 2010 wanandoa hawa wakasafiri kutoka Johannesburg kwenda Cape Town kumalizia honeymoon. Capetown ni mji wa pili kwa ukubwa nchi Afrika Kusini ukiwa katika Peninsula Pwani ya Kusini Magharibi ya nchi hiyo.
Kivutio kikubwa ni milima ya Table Mountain ambayo watalii huwa wanpanda kwa kutumia Cable Cars.
Licha kwamba mji huu kuwa wenye kuvutia na kutembelewa na wageni wengi lakini historia yake sio nzuri.
Ni mji uliokuwa na ubaguzi sana kiasi cha watu weusi kuwa maskini sana na kuishi kwenye mabanda yasio na hadhi.
Baada ya sera ya kibaguzi ya Aprtheid kuisha mwazoni mwa miaka ya 1990, watu weusi nao wakaruhusiwa kuishi ndani ya mji wa Capetown.
Uwanja wa ndege wa Cape town upo katikati ya Cape Flat, hivyo wasafiri lazima wapite kwenye maeneo ya watu maskini kuingi katikati ya mji wa Capetown.
Walipowasili katika uwanja wa ndege wa Capetown, Ani na Shren wakatoka nje ya uwanja ili wapate Tax ya kuwapeleka Hotel ya Cape Grace Hotel.
Shren akamuita dereva Tax ambaye anaitwa Zola Tongo, akamueleza mahali anapotakiwa kwenda. Zola Tongo akapakia mabegi ya wanandoa hawa kwenye gari yake na safari kwenda hotelini ikaanza.
Safari kutoka uwanja wa ndege mpaka hotelini ilichukua dakika 20, walipofika gotelini Zola Tongo akawapa namba yake simu iwapo watahitaji huduma ya Tax waweze kumpigia. Zola Tongo akaondoka akiwaacha Ani na Shren mapokezi hotelini.
Baada ya hapo Ani na Shren wakapata chakula cha mchana katika mgahawa hapo hotelini.
Siku ya pili waliitumia muda kupumzika na kufurahi mandhari ya hoteli, huku wakiogelea hapo hapo hotelini.

Jioni ya siku hiyo wakaamua wakapete chakula cha usiku nje ya hoteli ili waujue vizuri mji wa Cape Town.
Shren akampigia simu Zola Tongo, yule dereva wa Tax ili awapeleke huko. Ani akavaa gauni nyeusi na viatu vya silver huku akiwa na mkoba, Shren alivaa mavazi meusi. Zola Tongo alifika na wanandoa hawa wakapanda gari tayari kwa safari.
Wakiwa njia wakaomba ushauri mahali ambapo wanaweza kupata chakula cha asili ya bara Asia. Zola Tonga akawapeleka katika mgawaha unauza vyakula ya asili ya Asia, Ani na Shren walifurahia mgahawa huo baada ya kula chakula kinachojulikana kama Sushi. Zola Toga aliwashusha na yeye kuendelea na kazi yake, lakini walikubaliana kuwa baadaye watampigia simu ili wakutane.
Saa 4.15 usiku, Shren akampigia simu Zola Tongo kuwa wamemaliza kula na wapo tayari kurudi hotelini. Zola Tongo alifika na kuwabeba wanandoa hawa ili kuwarudisha hotelini, safari hii Zola Tongo akaamua kupita kwenye barabara inayojulikana kama N2 road.

Saa 5 usiku, kijanamwenye umri wa miaka 32 anayeitwa Simbonile Madekazi, alikuwa anarudi nyumbani kwake eneo la Capetown Flats township, wakati anapaki gari yake akaona kuna mtu mwenye asili ya kihindi karibu na mlango wake wa kuingia ndani.
Shren akamkaribia Simbonile na akasema tafadhali je kuna kituo cha polisi eneo la karibu, ili nitoe taarifa ya kutekwa kwa mke wangu? Akajitambulisha kuwa yeye ni Shren Dowan na akasema kuwa yeye na mke wake walikuwa kwenye gari na walitekwa lakini yeye ameachiwa ila watekaji wameondoka na mke wake.
Simbonile akapiga simu polisi, lakini polisi walipohitaji kujua eneo walilotekwa na aina ya gari iliyotekwa, Shren hakuweza kutoa majibu yanayoeleweka.
Polisi walifika baada ya dakika 15 na ndipo wakaanza kumuuliza maswali Shren, moja ya majibu ya Shren ni kuwa, yeye na mke wake Ani, waliamua kutembelea eneo nje ya hotel ya Cape Grace ili wajionee maisha ya waafrika wa hali chini wanaoishi hapo Capetown.
Shren akaendelea kusema kuwa walipokaribia kona ya mwisho kuelekea hotelini, walivamiwa na vijana wawili wenye bunduki.
Walimtoa dereva na mmoja wao akawa anaendesha tax bila yeye na mkewe kujua wanapoelekea katika muda huo.
Wakiwa chini ya ulinzi watekaji hao wakachukua hela, mkoba wa mke wake, pete na simu zao. Wakati wote huo walikuwa wakitishwa na watekaji hao, kuwa wawe watulivu kwa sababu, wanaweza kuwaua kwa kutumia risasi.
Shren akasema, baaada ya gari kuendeshwa kwa muda wa dakika, dereva alisimama na kuamuru Shren ashuke kwenye gari.
Baada ya Shren kushushwa, gari ikaondoka kwa kasi huku mkewe Ani Hindocha akiwa ndani ya gari na watekaji.
Ikambidi atembee ili kupata msaada kutoka katika nyumba za karibu na barabara ndipo alipofika kwenye nyumba ya Simbonile Madekazi.
Polisi wakaondoka na Shren kumrudisha Cape Grace Hotel, na wakaanza kutafuta gari iliyotekwa.
Shren akapiga simu Uingereza na Sweden kuwaeleza wazazi wake na wazazi wa Anni kuwa walitekwa, yeye yupo salama lakini mke wake bado yupo kwenye mikono ya watekaji.
Baada ya muda, polisi walirudi hotelini wakiwa na dereva Tax, Zola Tongo. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi ni kuwa baada ya kushushwa na watekaji, Zola Tongo alienda kutoa taarifa polisi. Zola Tongo aliwaambia polisi kuwa hakumbuki majina ya wateja wake lakini anajua kuwa wamefikia katika hoteli ya Cape Grace Hotel ndio maana maafisa wa polisi wamefika hapo.

Nyumbani kwa akina Anni, hali ilikuwa ya masikitiko zaidi hasa kwa mama yake Nilam ambaye alikuwa akilia sana. Baba yake Anni, mzee Vinod Hindocha akaanza maandalizi ya kwenda Afrika kusini, wakati huo pia baba yake na Shren, mzee Diwan akafanikiwa kupata tiketi mbili kwenye ndege iliyokuwa inatoka Amsterdam, Uholanzi kwenda Capetown, Afrika kusini.
Hivyo wote wakasafiri, kwenda Amsterdam ili kupanda ndege kwenda Capetown.
Akiwa amefika Amsterdam ndipo anapata taarifa kuwa mwili wa mtoto wake Ani, umepatikana akiwa amkufa kwa kupigwa risasi ya shingo nje ya mji wa Capetown.
Hii ilikuwa taarifa mbaya sana kwa familia ya Vinod Hindocha.

Huko Capetown, polisi walipewa taarifa kuwa kuna gari imepakiwa pembeni ya barabara, ila cha kushangaza ni kuwa damu inatiririka kutoka upande wa nyuma ya gari hiyo.
Polisi walifika eneo la tukio saa 2 asubuhi na wakagundua gari iliyotolewa taarifa ndio Tax iliyotekwa.
Walipofungua ndani, wakakuta mwili wa Anni Hindocha, ukiwa umelala siti ya nyuma, ukiwa na jeraha la risasi upande shingoni. Kwa uchunguzi wa haraka ilionekana kuwa risasi imepigwa kwa karibu sana.
Pochi, pete na simu ya Anni vyote vilikutwa vikiwa pembeni ya mwili wa Anni Hindocha.

Kwa ukubwa tukio hili, Meya wa Mji wa Capetown aliagiza polisi kufanya uchunguzi na kuhakikisha kuwa wote waliohusika wanakamatwa.
Tukio hili liliathiri sana utalii wa Afrika kusini hasa katika mji wa Capetown.
Baba wa Anni, mzee Vinod akawasili katika mji wa Capetown na kupokelewa na maafisa wa polisi wa Afrika kusini pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Uingereza na Sweden.
Baada ya hapo akapelekwa katika hotel ya Grace Cape Hotel, ili kukutana na mkwe wake Shren.
Alipofika hotelini, alishangazwa na utulivu wa Shren kwa kuwa hakuwa anaonyesha huzuni, wakati yeye akiwa analia kutokana na kifo cha mtoto wake, Shren alikuwa yupo bize na simu yake akichati na kuongea. Jambo hili lilishangaza polisi pamoja na mzee Vinod, lakini walidhani kwa wakati huo labda Shren ndivyo anavyosononeka kwa msiba wa mkewe.

Jumatatu ya November 15, polisi wakamchukua mzazi wa Ani, mzee Vinod Hindocha akapelekwa hospitali ili kuona mwili wa binti yake.

Itaendelea................

Sehemu ya pili,
Baada ya kufika hospitali, mzee Vinodi akaonyeshwa mwili wa mtoto wake Anni, mzee alilia sana huku akibaki na majonzi sana.
Ubalozi wa Uingereza na Sweden ukishirikiana na mzee Vinod, wakapanga mwili wa Anni usafirishwe kurudi London kwa ajili ya mazishi.
Novemba 16 mwaka 2010 ikawa ndio siku ya kusafirisha mwili, wakiwa hotelini Cape Grace, mume wa Anni, Shren alionekana yupo bize sana na simu yake, lakini pia kuna nyakati alitoka nje ya hoteli akiwa na bahasha ya khaki na akampatia kijana mmoja mwafrika.
Hatimaye safari ya kurudi Uingereza ikaanza kutoka uwanja wa ndege wa Cape Town, kwa mujibu wa mzee Vinod, Shren alipokaa kwenye siti yake akajilaza na kufunga macho, kiujumla alitumia muda mrefu wa safari akiwa amelala.

Huko Capetown

Polisi wa Capetown wakaanza kumhoji dereva Tax Zola Tongo, kwanini aliwapeleka wageni katika mitaa ambayo inajulikana kwa ujmbazi na utekaji?
Zola Tonga akawa na majibu ambayo hayakuwaridhisha polisi. Kiujumla katika uchunguzi alama za vidole (Fingerprint) 25 zilikutwa kwenye Taxi ya Zola Tongo, polisi wakaanza kumsaka kila mtu ambaye alama zake za vidole zilikuwa kwenye Taxi. Alama hizi zikapelekwa kwenye database ya alama za vidole za watu nchini Afrika kusini kwa ajili ya utambuzi. Moja kati ya alama iliyojirudia mara nyingi ilikuwa ya kijana mmoja anayeitwa Kolile Mungeni.
Kolile Mungeni ni nani? Huyu kijana miaka mitano nyuma aliwahi kukamatwa na kufungwa kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kuhusika katika tukio la mauaji katika baa moja hapo Cape Town, hivyo taarifa zake zilikuwa kwenye database ya polisi nchini Afrika kusini. Alikaa miaka miwili jela kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa kutosha hivyo kesi ikawa imemalizwa.
Asubuhi ya tarehe 16 Novemba,2010 polisi wa Afrika kusini, wakamtaka Kolile Mungeni kwenye kibanda karibu kabisa na mahali ilipotelekezwa Taxi ya Zola Tonga. Siku moja kabla Kolile Mungeni alikuwa na marafiki zake wakifurahi maisha na kunywa pombe, hivyo alikutwa akiwa amelala huku akiwa amelewa, kwenye kibanda hiki walikutwa pia vijana wengine wawili.
Polisi wakawatoa nje wakiwa wameshafungwa pingu na baadhi ya polisi wakafanya upekuzi. Katika zoezi la upekuzi polisi walikuta simu moja aina ya Nokia, wakamuuliza Kolile Mungeni, hii simu ni ya nani?
Kolile Mungeni akajibu kuwa simu ni ya dereva Tax, wakati polisi wanaendelea na upekuzi wakakuta Mkoba na saa, na bangili ya dhahabu, vitu vyote hivi vilitambuliwa kuwa mali ya Ani Hindocha ambaye kwa sasa alikuwa marehemu.

Kolile Mungeni na vijana wale wawili wakapelekwa polisi kwa ajili ya mahojiano. Baada ya maswali machache, Kolile Mungeni akakiri kuhusika katika tukio la kuteka Taxi na kupora, alipoulizwa kuhusu kifo cha Ani, akasema yeye hahusiki na mauaji hayo. Polisi walipomuuliza anajua kuwa kuna mtu alikufa katika tukio hilo? Akajibu, ndio ninajua lakini aliyemuua huyo mwanamke ni mtu anayejulikana kwa jina la Umzi Wamadodo Kwabe.
Kufikia hapo polisi wakaanza jitihada za kumkamta Umzi Wamadodo Kwabe. Kolile Mungeni alikuwa akitoa ushirikiano wa karibu sana kwa polisi, kwa kuwapeleka mpaka eneo ambalo utekaji wa gari ulitokea. Akawapeleka mpaka mahali ambapo mume wa Ani, yaani Shren aliposhushwa kwenye gari na hata mahali ambapo Umzi Wamadodo Kwabe alifyatua risasi na kumuua Ani.

Baada ya hapo akawapeleka polisi katika mitaa ambayo Umzi Wamadodo anaishi lakini hawakuweza kumpata.
Huku jitihada za kumpata Umzi Wamadodo zikiendelea, Kolile Mungeni akawekwa rumande huku taratibu nyingine zikiendelea.
Siku mbili baadaye, yaani Novemba 18 mwaka 2010 polisi wakafanikiwa kumkamata Umzi Wamadodo. Umzi Wamadodo alikuwa na miaka 27 akiwa na mke na watoto watatu.
Mpaka wakati huo Umzi Wamadodo hakuwa na rekodi yoyote ya kiuhalifu, hii ilishangaza polisi. Lakini baada ya uchunguzi, ikajulikana kuwa Umzi Wamadodo anajishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Polisi wakampeleka Umzi Wamadodo kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano, cha kushangaza, Wamadodo alikiri haraka sana kuhusika kwake kwenye tukio la utekaji, lakini pia akawapa polisi eneo aliloficha silaha iliyotumika kumuua Ani Hindocha. Polisi wakafanikiwa kuipata silaha kwa maelekezo ya Umzi Wamadodo, na wakathibisha kuwa ni kweli silaha hiyo ndio ilitumika katika tukio la mauaji.
Licha ya kuonyesha ushirikiano wote na kuwapa polisi taarifa muhimu lakini alikataa kuwa sio yeye aliyefyatua risasi iliyomuua Ani, yeye akasema wakati wa tukio yeye alikuwa dereva tu, aliyeua ni Kolile Mungeni. Polisi wakawa na watuhumiwa wawili ambao wanakubali kuhusika kwenye tukio ila wote wanakataa kuwa walifyatua risasi, kila mmoja akimtuhumu mwingine.
Wakati polisi wakiwa na mshangao kwa watuhumiwa hawa ndipo Umzi Wamadodo akawaambia polisi kuwa yeye na mwenzake Kolile Mungeni walipewa kazi ya kuteka na kuua na mtu mwingine anayeitwa Mondei Mbombo lakini pia dereva wa Taxi anayeitwa Zola Tongo.
Kufikia hapo polisi wakajua kuwa hii sio kesi ya kawaida ya kutekwa kwa magari ama uporaji, ikaonekana kuwa ni tukio lililopangwa.

Turudi kwa Mondei Mbombo, huyu ni nani?
Mondei Mbombo kijana wa miaka 31, huyu alikuwa mfanyakazi upande wa mapokezi wa hotel ya kifahari Protea Colosseum Hotel, yeye na Umzi Wamadodo walifahamamiana miaka 10 iliyopita wakti huo wakiwa wanafanya kazi katika kampeni ya kuhamasisha elimu kwa vijana weusi wa Afrika kusini katika mji wa Cape Town. Wakapotezana kwa miaka kadhaa mpaka walipokutana tena Novemba mwaka 2010, wakazungumza na kupeana namba.
Tarehe 21 November mwaka 2010, polisi wakafanikiwa kumkamata Mondei Mbombo, hivyo polisi wakawa na watuhumiwa wote wa kesi hii pamoja na dereva Taxi Zola Tongo ambaye hapo awali polisi waliamini kuwa hana hatia na hahusiki na utekaji wala kuuawa kwa dada Ani.

Wakati huo, mipango ya mazishi ya marehemu Ani ilikuwa ikiendelea katika jiji la London, nchi Uingereza.
Kwenye msiba, ndugu jamaa na marafiki wakaanza kushangazwa na tabia za mume wa marehemu Shren, muda mwingi alikuwa akiongea na simu na kuchati kwenye kompyuta yake, hakuonyesha simanzi ya mtu aliyefiwa na mke tena kwa kifo cha kupigwa risasi.

Wakati wa maandalizi ya mazishi, Shren akajikuta katika majibizano na ndugu wa Ani, huyu anaitwa Shinea, huyu na Ani walikuwa pamoja na waliishi pamoja kwa muda mrefu. Huyu hakupenda tabia za shemeji yake za kuonyesha kwamba hajaguswa na msiba na wala hana masikitiko. Shinea aliwahi kupata meseji kadhaa kutoka kwa Ani kuwa hana furaha kwenye mahusiano yake na Shren. Kwa kumbumbuku hii, akawa anaona kabisa kuwa ndugu yake hakuwahi kupendwa na Shren.

Siku ya tarehe 21 Novemba mwaka 2010 polisi ikawajulisha familia ya Ani kuwa kutokana na upelekezi unaoendelea, polisi imemkamata pia dereva Taxi - Zola Tongo.
Siku hiyo hiyo kaka wa Shren anayeitwa Prayan akampigia simu mzee Vinodi Hindocha (baba wa Ani) kuwa si vyema wao kama familia kuzingatia meseji za malamiko ambazo Ani alimtumia dada yake Shinea. Mpaka wakati huo mzee Vinod Hindocha alikuwa hajui chochote kuhusiana na malalamiko ya mtoto wake kuhusiana na mahusiano yake na Shren. Alipomuuliza Shinea, ndipo alipoonyeshwa meseji za malalamiko za mtoto wake kuwa hana furaha kwenye mahusiano na Shren na hata hiyo ndio ni kwa ajili ya heshima tu. Mzee akabaki ameshangaa sana.
Tarehe 22 Novemba mwaka 2010 polisi wa Afrika Kusini ikaijulisha Idara ya Usalama ya Uingereza kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na watuhumiwa, mume wa Ani bwana Shren ndiye aliyepanga utekaji na mauaji ya mke wake Ani, kwa kuwatumia watu wanaofahamika kama Kolile Mungeni, Umzi Wamadodo, Mondei Mbombo na dereva taxi Zola Tongo.
Polisi wa Uingereza nao wakawapa taarifa familia ya marehemu Ani, kupitia kwa baba yake Mzee Vinodi Hindocha. Kufikia hapo kila kitu kikawa kimebadilika kabisa, taswira nzima ya msiba ikawa imebadilika. Familia ya Vinodi Hindocha na ile ya Shren Diwan ikawa ni ya uadui.
Baada ya taarifa hii kutoka, Shren akahojiwa na gazeti la Daily Mirror na kukana kuhusika kwako kwenye kifo cha Ani, huku akisema kuwa alimpenda Ani, kuliko kitu chochote hapa duniani na kuwa hawezi hata kufikiri kumdhuru mwanamke huyo ambaye kwa sasa ni marehemu. Akaongeza kuwa watu wanaomshuku katika hili ni wale ambao hawajui na hawakuona namna walivyokuwa wanapendana na Ani.Lakini akaongeza kuwa hana sababu ya kumuua Ani, maana hawana mali walizochuma pamoja, na hakuna ambacho atapata kwa kumuua mwanamke huyu siku za mwanzoni kabisa za ndoa yao, nilimpenda na nitampenda zaidi.
Katika mahojiano hayo Shren akajichanganya mahali, kwa kusema kuwa ilikuwa ni wazo la dereva Zola Tongo kuwapeleka wanandoa hao kwenye ule mgahawa wenye vyakula vya Kiasia. Hilo likawa kosa la kwanza.

Lakini pia akajichanganya tena kwa kusema kuwa watekaji walimshusha kwa nguvu kutoka kwenye gari, na alikuwa anapambana nao. Kwenye ripoti aliyotoa kwa polisi wa Afrika kusini hakusema kuwa alipambana na watekaji. Pia hata alipokutwa na polisi, muonekano wake haukuwa mtu aliyekuwa kwenye kupambana.
Hisia zikaanza kwenye familia ya Ani, wakati huu sasa ndipo Shinea akawapa taarifa familia kuwa Ani aliwahi kumwambia kuwa licha ya ndoa kuwa imefanyika lakini yeye na Shren hawajawahi kufanya tendo la ndoa, hii ilishangaza kiasi na kupelekea kuibuka kwa maswali zaidi. Je Shren ni mwanamume kamili? Hapo sasa ukweli mwingine ukaibuka kuhusu Shren, mume wa Ani.

Ani alipogundua kuwa Shren amepanga kumpeleka honeymoon nchini Afrika Kusini, Ani aliandika meseji kwa ndugu yake Shinea kuwa hataki kwenda Afrika kusini, sababu ikiwa ni kutoridhishwa kwake na kuwa na mume ambaye hawajakutana kimwili na inaonekana kuwa ana matatizo.
Shinea akamuomba Ani aende honeymoon ili kuepuka fedhea kwa familia yao. Kufikia muda huu familia ikaamini kuwa safari ya Afrika kusini ilikuwa mpango maalum wa kumuua mtoto wao Ani, kwa sababu afrika kusini ilikuwa inasifika kwa uporaji na mauaji, hivyo tukio la Ani kufa akiwa Afrika kusini lisingezua maswali mengi.

Turudi Afrika Kusini sasa;
Mwezi Desemba mwaka 2010 Idara ya upelezi ya Afrika Kusini ikamtaarifu mzee Vinod Hindocha kuwa anatakiwa kwenda Afrika Kusini.
Mzee Vinodi akasafiri mpaka Afrika Kusini, alipofika akataarifiwa na Idara ya Upelelezi ya Afrika Kusini kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na dereva Taxi Zola Tongo, wamepata sababu ya kutosha kuamini kuwa tukio la kutekwa na kuuawa kwa mtoto wake Ani, lilipangwa na mume wake Shren.
Ushahidi dereva Taxi- Zola Tongo ulikuwa kama ifuatavyo; alisema; baada ya kuwabeba kutoka Uwanja wa ndege Shren na mkewe Ani, aliwapeleka kwenye hoteli ya Cape Grace Hotel, aliendelea kusema kuwa walipofika Ani, aliingia hotelini Shren alibaki nje akiongea naye na ndipo katika hali ya kushangaza akamuuliza, je unamjua mtu anayeweza kuua mtu?

Zola Tongo anasema baada ya mazungumzo mafupi ndipo akagundua kuwa Shren anataka mtu wa wa kumuua mke wake Ani.
Na kuwa Shren alikuwa tayari kulipa kiasi Rand 15,000/- (Elfu kumi na tano) na kumlipa Zola Tongo kiasi cha Rand 2,000/- (Elfu mbili) iwapo atapata mtu wa kufanya kazi hiyo.
Licha ya kuwa Zola Tongo hakuwa na rekodi za kihalifu lakini alikubali kumtafutia mtu anayeweza kufanya kazi hiyo ya kuua.
Polisi waliangalia camera za usalama na kuona kuwa ni kweli Shren na Zola Tongo walisimama na kuzungumza kwa dakika kadhaa nje ya Hotel ya Cape Grace.

Camera pia zilimnasa Shren akiingia ndani ya hotel lakini akatoka dakika tano baadaye na kuzungumza na Zola Tongo kwa dakika tisa.
Zola Tongo akaendelea kusema kuwa baada ya kutoka hapo Hotelini ndipo alipompigia simu rafiki yake Mondei Mbombo aliyekuwa anafanya kazi Protea Colosseum Hotel. Rekodi za simu zilionyesha ni kweli kuwa Zola Tongo alimpigia simu Mondei Mbombo na walizungumza kwa dakika kadhaa.

Polisi walipofuatilia kamera za usalama za Hotel ya Protea waligundua kuwa siku hyo Zola Tongo na Mondei Mbombo walikutana na kuzungumza nje ya hotel ya Protea Colloseum, kuthibitisha maneno ya Zola Tongo.

Kwa maelezo ya Zola Tongo ni kuwa alipofika kazini kwa Mondei Mbombo alimueleza juu ya mtu anayetaka mke wake auawe, ndipo Mondei Mbombo akamwambia Zola kuwa yeye ana sahihi mtu anayeweza kufanya kazi hiyo. Mazungumzo yao kwa mujibu wa video za CCTV yalidumu kwa dakika mbili.

Zola Tonga akaondoka huku akiwa amehaidiwa kuwa atapatiwa mtu sahihi kwa shughuli ya kuua.

Jioni ya siku hiyo Mondei Mbombo akampigia simu Umzi Wamadodo kuwa kuna kazi ya kuua mtu kwa malipo ya Randi 15,000/- na akamuuliza kama anaweza kufanya kazi hiyo, wakati simu inapigwa Umzi Wamadodo alikuwa yupo na rafiki yake Kolile Mungeni. Watu hao wawili wakakubali kuifanya hiyo kazi kwa pamoja.
Usiku huo Zola Tongo akawapa taarifa kuwa Shren na mkewe Ani, wanapata chakula cha usiku kwenye mgahawa, akawapa eneo na muda atakaokuwa anawarudisha hotelini na njia atakayopita.

Polisi pia waligundua kuwa kabla ya Shren na mkewe Ani kuondoka mgahawani kurudi hotelini, alipokea meseji kutoka kwa dereva Taxi- Zola Tongo, japokuwa hawakuweza kujua ni nini kiliandikwa kwenye mesehi hiyo…..

Safari ya kurudi hotelini ikaanza……………………..

Sehemu ya Tatu

Baada ya kesi kuendeshwa kwa muda nchi Afrika kusini mwendesha Mashtaka akawaahidi Umzi Wamamdodo na dereva taxi Zola Tongo kuwa iwapo watakiri kosa na kutoa ushahidi dhidi ya Shren Dewani basi watapunguziwa adhabu.
Kwa upande mwingine Monde Mbombo yeye akahaidiwa msamaha kamili iwapo pia atatoa ushahidi wa kutia hatiani Shren Diwani. Kiufupi ni kwamba mwendesha mashtaka alitaka kutumia kila mbinu kumtia hatiani Shren Diwani.

Tarehe 7 Desemba 2010, dereva tax Zola Tongo akafikifishwa katika mahakama kuu ya Western Cape, akakiri makosa ya kuiba kwa kutumia silaha, kuteka na kuhusika katika mauaji ya Ani Hindocha lakini akaongeza kwa kusema alifanya yote haya akishirikiana na mume wa Ani anayeitwa Shren Diwani. Mahakama ikampa Zola Tongo adhabu ya kifungo cha miaka 18 jela na akapelekwa katika gereza la Malmesbury.

Tarehe 18 February 2011 Umzi Wamadodo akahukumiwa kifungo cha miaka 25 kwenda jela kwa kosa la kuteka, kupora na kuua.

Tarehe 19 February 2012 baada ya kesi kuendeshwa kwa muda mrefu mtuhumiwa mwingie Kolile Mngeni naye akatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Tarehe 14 Julai mwaka 2014 Kolile Mungeni akiwa anatumikia kifungo cha maisha jela ikagundulika kuwa anaugua kansa ya ubongo, wamasheria kadhaa wakaomba apatiwe msamaha lakini mahakama ikakataa ombi la hilo.
Tarehe 18 Oktoba mwaka 2014 Kolile Mungeni akafariki katika gereza la Goodwood.​

Turudi kwa Shren akiwa London, Uingereza

Tarehe 12 Agosti 2013 kijana mmoja wa kiume amwenye umri wa miaka 25 akajitokeza na kudai kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Shren Diwani, baada ya taarifa hizi kuandikwa gazetini, Shren na familia yake walikana lakini baadaye yule kijana akaachia meseji na picha zilizothibitisha kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.
Baada ya taarifa hizi ikawa wazi kwamba Shren alioa kwa sababu ya shinikizo la wazazi na ndugu zake lakini alikuwa ni tu wa mapenzi ya jinsia moja yaani jamaa alikuwa Gay (shoga).
Hii ikawa taarifa mbaya zaidi kwa familia ya Diwani na familia ya mzee Vinod Hindocha, maana sasa ilikuwa wazi kuwa mauaji yalipangwa ili kuficha ukweli huu wa Shren kuwa shoga na hakuwa mwanamume kamili.

Hili halikuwa tatizo kwa Shren kwa sababu nchini Uingereza kuwa shoga au kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja sio kosa kisheria.

Tarehe 1 Mei mwaka 2014 Mahakama ya Afrika kusini ikatuma ombi kwa idara ya usalama ya Uingereza kuomba Shren Diwani, apelekwe Afrika kusini kujibu tuhuma za kupanga mauaji ya mke wake Ani Hindocha.
Baada ya majadiliano na maombi kadhaa ya Shren kuomba asipelekwe Afrika Kusini hatimaye tarehe 7 April 2014 Shren Diwani akapandishwa ndege na maafisa wa Uingereza kupelekwa Afrika kusini kujibu tuhuma zake.
Alipofika tu uwanja wa ndege wa Cape Town, alikamatwa na maafisa wa Afrika kusini na kuweka rumande kwa tuhuma za makosa ya kupanga njama za kumuua mkewe, unyanganyi na kuzuia ushahidi muhimu katika kesi.

Shren Diwan kwa ujasiri kabisa akakataa makosa yote licha ya kuonyeshwa ushahid kutoka kwa dereva tax na Umzi Wamadodo.

Kesi ya Shren Diwani ikaanza kusikilizwa tarehe 6 Oktoba 2014 katika mahakama kuu ya Cape Town chini ya Jaji maarufu Traverso, Shren alikuwa anatetewa na wanasheria wa kimataifa katika kesi hiyo.
Wakati kwa maswali kwa mashahidi ambao ni Umzi Wamadodo, dereva Tax Zola Tongo, wakajichanganya katika mpangilio wa tukio. Wakati Zola Tongo akidai kuwa aliambiwa na Shren kutafuta mtu wa kumuua mkewe, Umzi Wamadodo alisema yeye alipewa taarifa za kumteka tu Ani na sio kuua. Hilo likawa kosa kubwa sana lilioathiri mwenendo mzima wa kesi. Mawakili wa kimataifa kutoka Uingereza wakapeleka ombi kwa Hakimu Traverso.
Tarehe 24 Novemba mwaka 2014 Jaji Traverso akaiambia mahakama kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unaomhusisha moja kwa moja Shren Diwani katika utekwaji wa gari na kifo cha mkewe Ani Hindocha. Kufikia hapo Mahakama kuu ya Cape Town ilikuwa imeamua kuwa Shren Diwani hana kesi ya kujibu, hivyo yupo huru.

Baada ya maamuzi haya watu wengi na mashirika kadhaa yalilaumu uamuzi wa Jaji Traverso wakidai kuwa Jaji ameamua kwa makusudi kumuachia mtu aliyepanga mauaji ya mke wake katika ardhi ya Afrika Kusini.

Familia ya Ani Hindocha, ilijaribu mara kadhaa kufungua shauri na mashtaka kwa Shren Diwani lakini polisi na mwendesha mashtaka walikataa kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani Shren Diwani.

Shren alirudi London Uingereza kuendelea na maisha yake akiwa mtu huru kabisa, japo kwa sasa sio mtu anayeonekana kila mahali na inadhaniwa kuwa amehama kabisa nchi Uingereza.

Kauli ya mwisho kutoka kwa familia ya Ani Hindocha

Tarehe 4 Agosti 2018 familia ya Ani Hindocha kupitia kwa msemaji wa familia ikasema ‘’ tunakubali kuwa binti yetu ameshafariki, hakuna tunachoweza kufanya kwa sasa, tunajua kuwa Shren alihusika kwa namna moja ama nyingine, hii inatuumiza sana. Inasikitisha kwamba tulikubali binti yetu kuolewa na mtu ambaye alikuwa na maisha ya siri katika ushoga, ni maisha yake lakini hakupaswa hata kuja kuomba kumuoa binti yetu, tumeumia sana na tunastahili kuombwa japo samahani kutoka kwa Shren.’’

Mwisho.

.

Sehemu ya pili,
Baada ya kufika hospitali, mzee Vinodi akaonyeshwa mwili wa mtoto wake Anni, mzee alilia sana huku akibaki na majonzi sana.
Ubalozi wa Uingereza na Sweden ukishirikiana na mzee Vinod, wakapanga mwili wa Anni usafirishwe kurudi London kwa ajili ya mazishi.
Novemba 16 mwaka 2010 ikawa ndio siku ya kusafirisha mwili, wakiwa hotelini Cape Grace, mume wa Anni, Shren alionekana yupo bize sana na simu yake, lakini pia kuna nyakati alitoka nje ya hoteli akiwa na bahasha ya khaki na akampatia kijana mmoja mwafrika.
Hatimaye safari ya kurudi Uingereza ikaanza kutoka uwanja wa ndege wa Cape Town, kwa mujibu wa mzee Vinod, Shren alipokaa kwenye siti yake akajilaza na kufunga macho, kiujumla alitumia muda mrefu wa safari akiwa amelala.

Huko Capetown

Polisi wa Capetown wakaanza kumhoji dereva Tax Zola Tongo, kwanini aliwapeleka wageni katika mitaa ambayo inajulikana kwa ujambazi na utekaji?
Zola Tonga akawa na majibu ambayo hayakuwaridhisha polisi. Kiujumla katika uchunguzi alama za vidole (Fingerprint) 25 zilikutwa kwenye Taxi ya Zola Tongo, polisi wakaanza kumsaka kila mtu ambaye alama zake za vidole zilikuwa kwenye Taxi. Alama hizi zikapelekwa kwenye database ya alama za vidole za watu nchini Afrika kusini kwa ajili ya utambuzi. Moja kati ya alama iliyojirudia mara nyingi ilikuwa ya kijana mmoja anayeitwa Kolile Mungeni.
Kolile Mungeni ni nani? Huyu kijana miaka mitano nyuma aliwahi kukamatwa na kufungwa kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kuhusika katika tukio la mauaji katika baa moja hapo Cape Town, hivyo taarifa zake zilikuwa kwenye database ya polisi nchini Afrika kusini. Alikaa miaka miwili jela kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa kutosha hivyo kesi ikawa imemalizwa.
Asubuhi ya tarehe 16 Novemba,2010 polisi wa Afrika kusini, wakamtaka Kolile Mungeni kwenye kibanda karibu kabisa na mahali ilipotelekezwa Taxi ya Zola Tonga. Siku moja kabla Kolile Mungeni alikuwa na marafiki zake wakifurahi maisha na kunywa pombe, hivyo alikutwa akiwa amelala huku akiwa amelewa, kwenye kibanda hiki walikutwa pia vijana wengine wawili.
Polisi wakawatoa nje wakiwa wameshafungwa pingu na baadhi ya polisi wakafanya upekuzi. Katika zoezi la upekuzi polisi walikuta simu moja aina ya Nokia, wakamuuliza Kolile Mungeni, hii simu ni ya nani?
Kolile Mungeni akajibu kuwa simu ni ya dereva Tax, wakati polisi wanaendelea na upekuzi wakakuta Mkoba na saa, na bangili ya dhahabu, vitu vyote hivi vilitambuliwa kuwa mali ya Ani Hindocha ambaye kwa sasa alikuwa marehemu.

Kolile Mungeni na vijana wale wawili wakapelekwa polisi kwa ajili ya mahojiano. Baada ya maswali machache, Kolile Mungeni akakiri kuhusika katika tukio la kuteka Taxi na kupora, alipoulizwa kuhusu kifo cha Ani, akasema yeye hahusiki na mauaji hayo. Polisi walipomuuliza anajua kuwa kuna mtu alikufa katika tukio hilo? Akajibu, ndio ninajua lakini aliyemuua huyo mwanamke ni mtu anayejulikana kwa jina la Umzi Wamadodo Kwabe.
Kufikia hapo polisi wakaanza jitihada za kumkamta Umzi Wamadodo Kwabe. Kolile Mungeni alikuwa akitoa ushirikiano wa karibu sana kwa polisi, kwa kuwapeleka mpaka eneo ambalo utekaji wa gari ulitokea. Akawapeleka mpaka mahali ambapo mume wa Ani, yaani Shren aliposhushwa kwenye gari na hata mahali ambapo Umzi Wamadodo Kwabe alifyatua risasi na kumuua Ani.

Baada ya hapo akawapeleka polisi katika mitaa ambayo Umzi Wamadodo anaishi lakini hawakuweza kumpata.
Huku jitihada za kumpata Umzi Wamadodo zikiendelea, Kolile Mungeni akawekwa rumande huku taratibu nyingine zikiendelea.
Siku mbili baadaye, yaani Novemba 18 mwaka 2010 polisi wakafanikiwa kumkamata Umzi Wamadodo. Umzi Wamadodo alikuwa na miaka 27 akiwa na mke na watoto watatu.
Mpaka wakati huo Umzi Wamadodo hakuwa na rekodi yoyote ya kiuhalifu, hii ilishangaza polisi. Lakini baada ya uchunguzi, ikajulikana kuwa Umzi Wamadodo anajishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Polisi wakampeleka Umzi Wamadodo kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano, cha kushangaza, Wamadodo alikiri haraka sana kuhusika kwake kwenye tukio la utekaji, lakini pia akawapa polisi eneo aliloficha silaha iliyotumika kumuua Ani Hindocha. Polisi wakafanikiwa kuipata silaha kwa maelekezo ya Umzi Wamadodo, na wakathibisha kuwa ni kweli silaha hiyo ndio ilitumika katika tukio la mauaji.
Licha ya kuonyesha ushirikiano wote na kuwapa polisi taarifa muhimu lakini alikataa kuwa sio yeye aliyefyatua risasi iliyomuua Ani, yeye akasema wakati wa tukio yeye alikuwa dereva tu, aliyeua ni Kolile Mungeni. Polisi wakawa na watuhumiwa wawili ambao wanakubali kuhusika kwenye tukio ila wote wanakataa kuwa walifyatua risasi, kila mmoja akimtuhumu mwingine.
Wakati polisi wakiwa na mshangao kwa watuhumiwa hawa ndipo Umzi Wamadodo akawaambia polisi kuwa yeye na mwenzake Kolile Mungeni walipewa kazi ya kuteka na kuua na mtu mwingine anayeitwa Mondei Mbombo lakini pia dereva wa Taxi anayeitwa Zola Tongo.
Kufikia hapo polisi wakajua kuwa hii sio kesi ya kawaida ya kutekwa kwa magari ama uporaji, ikaonekana kuwa ni tukio lililopangwa.

Turudi kwa Mondei Mbombo, huyu ni nani?
Mondei Mbombo kijana wa miaka 31, huyu alikuwa mfanyakazi upande wa mapokezi wa hotel ya kifahari Protea Colosseum Hotel, yeye na Umzi Wamadodo walifahamamiana miaka 10 iliyopita wakti huo wakiwa wanafanya kazi katika kampeni ya kuhamasisha elimu kwa vijana weusi wa Afrika kusini katika mji wa Cape Town. Wakapotezana kwa miaka kadhaa mpaka walipokutana tena Novemba mwaka 2010, wakazungumza na kupeana namba.
Tarehe 21 November mwaka 2010, polisi wakafanikiwa kumkamata Mondei Mbombo, hivyo polisi wakawa na watuhumiwa wote wa kesi hii pamoja na dereva Taxi Zola Tongo ambaye hapo awali polisi waliamini kuwa hana hatia na hahusiki na utekaji wala kuuawa kwa dada Ani.

Wakati huo, mipango ya mazishi ya marehemu Ani ilikuwa ikiendelea katika jiji la London, nchi Uingereza.
Kwenye msiba, ndugu jamaa na marafiki wakaanza kushangazwa na tabia za mume wa marehemu Shren, muda mwingi alikuwa akiongea na simu na kuchati kwenye kompyuta yake, hakuonyesha simanzi ya mtu aliyefiwa na mke tena kwa kifo cha kupigwa risasi.

Wakati wa maandalizi ya mazishi, Shren akajikuta katika majibizano na ndugu wa Ani, huyu anaitwa Shinea, huyu na Ani walikuwa pamoja na waliishi pamoja kwa muda mrefu. Huyu hakupenda tabia za shemeji yake za kuonyesha kwamba hajaguswa na msiba na wala hana masikitiko. Shinea aliwahi kupata meseji kadhaa kutoka kwa Ani kuwa hana furaha kwenye mahusiano yake na Shren. Kwa kumbumbuku hii, akawa anaona kabisa kuwa ndugu yake hakuwahi kupendwa na Shren.

Siku ya tarehe 21 Novemba mwaka 2010 polisi ikawajulisha familia ya Ani kuwa kutokana na upelekezi unaoendelea, polisi imemkamata pia dereva Taxi - Zola Tongo.
Siku hiyo hiyo kaka wa Shren anayeitwa Prayan akampigia simu mzee Vinodi Hindocha (baba wa Ani) kuwa si vyema wao kama familia kuzingatia meseji za malamiko ambazo Ani alimtumia dada yake Shinea. Mpaka wakati huo mzee Vinod Hindocha alikuwa hajui chochote kuhusiana na malalamiko ya mtoto wake kuhusiana na mahusiano yake na Shren. Alipomuuliza Shinea, ndipo alipoonyeshwa meseji za malalamiko za mtoto wake kuwa hana furaha kwenye mahusiano na Shren na hata hiyo ndio ni kwa ajili ya heshima tu. Mzee akabaki ameshangaa sana.
Tarehe 22 Novemba mwaka 2010 polisi wa Afrika Kusini ikaijulisha Idara ya Usalama ya Uingereza kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na watuhumiwa, mume wa Ani bwana Shren ndiye aliyepanga utekaji na mauaji ya mke wake Ani, kwa kuwatumia watu wanaofahamika kama Kolile Mungeni, Umzi Wamadodo, Mondei Mbombo na dereva taxi Zola Tongo.
Polisi wa Uingereza nao wakawapa taarifa familia ya marehemu Ani, kupitia kwa baba yake Mzee Vinodi Hindocha. Kufikia hapo kila kitu kikawa kimebadilika kabisa, taswira nzima ya msiba ikawa imebadilika. Familia ya Vinodi Hindocha na ile ya Shren Diwan ikawa ni ya uadui.
Baada ya taarifa hii kutoka, Shren akahojiwa na gazeti la Daily Mirror na kukana kuhusika kwako kwenye kifo cha Ani, huku akisema kuwa alimpenda Ani, kuliko kitu chochote hapa duniani na kuwa hawezi hata kufikiri kumdhuru mwanamke huyo ambaye kwa sasa ni marehemu. Akaongeza kuwa watu wanaomshuku katika hili ni wale ambao hawajui na hawakuona namna walivyokuwa wanapendana na Ani.Lakini akaongeza kuwa hana sababu ya kumuua Ani, maana hawana mali walizochuma pamoja, na hakuna ambacho atapata kwa kumuua mwanamke huyu siku za mwanzoni kabisa za ndoa yao, nilimpenda na nitampenda zaidi.
Katika mahojiano hayo Shren akajichanganya mahali, kwa kusema kuwa ilikuwa ni wazo la dereva Zola Tongo kuwapeleka wanandoa hao kwenye ule mgahawa wenye vyakula vya Kiasia. Hilo likawa kosa la kwanza.

Lakini pia akajichanganya tena kwa kusema kuwa watekaji walimshusha kwa nguvu kutoka kwenye gari, na alikuwa anapambana nao. Kwenye ripoti aliyotoa kwa polisi wa Afrika kusini hakusema kuwa alipambana na watekaji. Pia hata alipokutwa na polisi, muonekano wake haukuwa mtu aliyekuwa kwenye kupambana.
Hisia zikaanza kwenye familia ya Ani, wakati huu sasa ndipo Shinea akawapa taarifa familia kuwa Ani aliwahi kumwambia kuwa licha ya ndoa kuwa imefanyika lakini yeye na Shren hawajawahi kufanya tendo la ndoa, hii ilishangaza kiasi na kupelekea kuibuka kwa maswali zaidi. Je Shren ni mwanamume kamili? Hapo sasa ukweli mwingine ukaibuka kuhusu Shren, mume wa Ani.

Ani alipogundua kuwa Shren amepanga kumpeleka honeymoon nchini Afrika Kusini, Ani aliandika meseji kwa ndugu yake Shinea kuwa hataki kwenda Afrika kusini, sababu ikiwa ni kutoridhishwa kwake na kuwa na mume ambaye hawajakutana kimwili na inaonekana kuwa ana matatizo.
Shinea akamuomba Ani aende honeymoon ili kuepuka fedhea kwa familia yao. Kufikia muda huu familia ikaamini kuwa safari ya Afrika kusini ilikuwa mpango maalum wa kumuua mtoto wao Ani, kwa sababu afrika kusini ilikuwa inasifika kwa uporaji na mauaji, hivyo tukio la Ani kufa akiwa Afrika kusini lisingezua maswali mengi.

Turudi Afrika Kusini sasa;
Mwezi Desemba mwaka 2010 Idara ya upelezi ya Afrika Kusini ikamtaarifu mzee Vinod Hindocha kuwa anatakiwa kwenda Afrika Kusini.
Mzee Vinodi akasafiri mpaka Afrika Kusini, alipofika akataarifiwa na Idara ya Upelelezi ya Afrika Kusini kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa na dereva Taxi Zola Tongo, wamepata sababu ya kutosha kuamini kuwa tukio la kutekwa na kuuawa kwa mtoto wake Ani, lilipangwa na mume wake Shren.
Ushahidi dereva Taxi- Zola Tongo ulikuwa kama ifuatavyo; alisema; baada ya kuwabeba kutoka Uwanja wa ndege Shren na mkewe Ani, aliwapeleka kwenye hoteli ya Cape Grace Hotel, aliendelea kusema kuwa walipofika Ani, aliingia hotelini Shren alibaki nje akiongea naye na ndipo katika hali ya kushangaza akamuuliza, je unamjua mtu anayeweza kuua mtu?

Zola Tongo anasema baada ya mazungumzo mafupi ndipo akagundua kuwa Shren anataka mtu wa wa kumuua mke wake Ani.
Na kuwa Shren alikuwa tayari kulipa kiasi Rand 15,000/- (Elfu kumi na tano) na kumlipa Zola Tongo kiasi cha Rand 2,000/- (Elfu mbili) iwapo atapata mtu wa kufanya kazi hiyo.
Licha ya kuwa Zola Tongo hakuwa na rekodi za kihalifu lakini alikubali kumtafutia mtu anayeweza kufanya kazi hiyo ya kuua.
Polisi waliangalia camera za usalama na kuona kuwa ni kweli Shren na Zola Tongo walisimama na kuzungumza kwa dakika kadhaa nje ya Hotel ya Cape Grace.

Camera pia zilimnasa Shren akiingia ndani ya hotel lakini akatoka dakika tano baadaye na kuzungumza na Zola Tongo kwa dakika tisa.
Zola Tongo akaendelea kusema kuwa baada ya kutoka hapo Hotelini ndipo alipompigia simu rafiki yake Mondei Mbombo aliyekuwa anafanya kazi Protea Colosseum Hotel. Rekodi za simu zilionyesha ni kweli kuwa Zola Tongo alimpigia simu Mondei Mbombo na walizungumza kwa dakika kadhaa.

Polisi walipofuatilia kamera za usalama za Hotel ya Protea waligundua kuwa siku hyo Zola Tongo na Mondei Mbombo walikutana na kuzungumza nje ya hotel ya Protea Colloseum, kuthibitisha maneno ya Zola Tongo.

Kwa maelezo ya Zola Tongo ni kuwa alipofika kazini kwa Mondei Mbombo alimueleza juu ya mtu anayetaka mke wake auawe, ndipo Mondei Mbombo akamwambia Zola kuwa yeye ana sahihi mtu anayeweza kufanya kazi hiyo. Mazungumzo yao kwa mujibu wa video za CCTV yalidumu kwa dakika mbili.

Zola Tonga akaondoka huku akiwa amehaidiwa kuwa atapatiwa mtu sahihi kwa shughuli ya kuua.

Jioni ya siku hiyo Mondei Mbombo akampigia simu Umzi Wamadodo kuwa kuna kazi ya kuua mtu kwa malipo ya Randi 15,000/- na akamuuliza kama anaweza kufanya kazi hiyo, wakati simu inapigwa Umzi Wamadodo alikuwa yupo na rafiki yake Kolile Mungeni. Watu hao wawili wakakubali kuifanya hiyo kazi kwa pamoja.
Usiku huo Zola Tongo akawapa taarifa kuwa Shren na mkewe Ani, wanapata chakula cha usiku kwenye mgahawa, akawapa eneo na muda atakaokuwa anawarudisha hotelini na njia atakayopita.

Polisi pia waligundua kuwa kabla ya Shren na mkewe Ani kuondoka mgahawani kurudi hotelini, alipokea meseji kutoka kwa dereva Taxi- Zola Tongo, japokuwa hawakuweza kujua ni nini kiliandikwa kwenye mesehi hiyo…..

Safari ya kurudi hotelini ikaanza……………………..

Itaendelea sehemu ya Tatu

Nitakupa taarifa juu ya mwanamume aliyejitokeza nchi Uingereza na kudai kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Shren, hivyo kufanya kesi kuwa ngumu zaidi kwa Shren………

Na taarifa nzima ya utekelezaji wa kifo cha Ani

Shren kurudishwa Afrika kusini kujibu tuhuma
 
Back
Top Bottom