Sio ulimbukeni ndugu yangu na wala sina majivuno. Ukiona mtu anaona anabaguliwa juwa hajitumi. Lazima ujitume ndio usaidiwe. Mtu akiona una potential atakusaidia, wapalestina ni rahisi kuwa raia wa EU wanaishia kuendesha taksi na mabasi. Hebu fikiria kama kila mtanzania angepewa nafasi ya kuwa raia katika ncho za U.S.A, Canada na E.U naomba nikuulize wangekataa shule kweli ? Na mimi siongelei leo maana walianza kuwa wakimbizi zaidi ya miaka 60 iliyopita.
Usiseme kila mtu mwenye akiili anatakiwa kutoa msaada . Maisha ni kitendawili kuitengeneza jamii bora anza na familia yako na nyumbani kwako. Kumsaidia mtu yeyote duniani ni pesa na sio kitu kingine. Hauwezi kusaidiwa kama hauna kitu unaweza kutoa kwa Jamii. Ninatoka nje ya mada kidogo lakini unajua kwa nini Kagame anajipambania na minerals za Eastern DRC ?
Kama unaamini duniani ni kusaidiana naomba ufanye kazi bure na usilipwe mshahara. Mtu una akili kama Raia wa uswisi ambaye hata kama hana kazi analipwa na serikali. Misaada ya Marekani inatolewa strategically na sio kwa faida yenu kwa asilimia mia moja. Dunia ndio ilivyo mimi ninapofanya kazi najua boss sio rafiki yangu wala HR sio ndugu yangu ndio maana kila siku saa kumi na moja alfajiri nishatupa shuka. Huku Ujerumani sikuja kwa scholarship wala kwa kuomba omba. Hakuna mtu anejua aibu ya kuomba kama mimi. Niliacha kuomba mwaka 98, ndio maana huko juu nilikuambia ukatembelee Kenya uone nini maana na kupambana. Watu wanapambana aisee. Huku ujerumani vijana wadogo chini ya miaka 26 wana P.H.D.Sisi tumekazana kuruhusu Taasisi zitulipie mahari.