Cassius Clay 1964

Cassius Clay 1964

Mm ni mdogo mno, ila nina wimbo wa Elvis naupenda mno, ninao had kwenye simu, unaitwa SUSPICIOUS MIND [emoji16]
We can't go on with suspicious minds
And we can't build our dreams with suspicious minds.

Nyimbo nzuri sana.
 
Kwa hadith unazo tupatia ni kama sasa maisha yamerudi nyuma sana
Kabisa. Japo hapakuwa na maendeleo makubwa na utandawazi uliopo sasa lakini ni kama vile zamani vilikuwa vinapatikana kirahisi mno. Ni kawaida kwa miaka ya zamani mtoto wa maskini akipata channel kwenda Ulaya tofauti na sasa imekuwa ni lazima uwe tajiri kuweza kupata fursa za kimaisha.
 
CASSIUS CLAY 1964

Hii picha ilikuwa maarufu sana miaka ya 1960. Ilipigwa siku Cassius Clay alipomshinda Sony Liston na kuchukua mkanda wa uzito wa juu wa masumbwi.

Kwangu mimi picha hii inaniletea kumbukumbu nyingi za miaka hiyo. Kwanza nakumbuka kupokea simu kanipigia baba yangu niko nyumbani ananifahamisha kuwa Cassius Clay amempiga Sony Liston.

Kwa nini baba anipigie simu kunipa taarifa hizi? Alikuwa anajua ni kwa kiasi gani nikimpenda Cassius Clay. Wakati huo bado hajawa Muhammad Ali. Nyakati hizi zilikuwa za kipekee sana kwangu na kwa hakika watoto wengi wa umri wangu.

Hizi zilikuwa nyakati za The Beatles, Elvis Presley, Cliff Richard, Helen Shapiro, Ray Charles, Sam Cooke na wengineo. Nyimbo za hawa wanamuziki zilituchukua sana. Lakini kadri umri ulivyozidi kusogea na fikra zangu za utoto zikawa naziacha nyuma pamoja na hawa watu maarufu.

Lakini mara moja moja ninaposikia miziki yao wa nyakati zao narejea udogoni inakuwa kama jana. Nakumbuka siku nilipoiona senema ya Elvis Presley, "Blue Hawaii," Empire Cinema. Ilikuwa siku ya Eid Fitr. Nyimbo zake hadi leo zinajaza moyo wangu kumbukumbu nyingi.

Nimemuona Helen Shapiro katika "Play it Cool," anaimba "I don't Care."

Katika senema hii alikuwapo Billy Fury. Kijana wa Kiingereza akipiga mitindo ya Rock and Roll.

Siku moja niko Liverpool Coach Station, London stesheni ya mabasi kwenda "bara" ya Uingereza ukipenda.

Natoka Cardiff nakwenda Glasgow. Cardiff ukifananisha na London ni shamba mfano unatoka Kilwa unakuja Dar-es-Salaam upande basi kwenda labda Arusha.

Ukifika Dar es Salaam kituo cha mabasi Mnazi Mmoja na wewe huijui Dar-es-Salaam bila shaka utanyoosha miguu kuangalia mji kabla ya kwenda Arusha angalau upate cha kuhadithia ukirejea Kilwa.

Basi nanyoosha miguu kuangalia mitaa jirani na hapo Liverpool Coach Station. Nikakuta tangazo limebandikwa nje kwenye kioo cha mgawa mmoja mdogo mfano wa AK Tea Room.

Tangazo lile linamtangaza Helen Shapiro kama Born Again Christian na kueleza wapi atahubiri Injili. Zaidi ya miaka 30 sasa imepita. Nilipangiwa kusomesha darasa moja la undergraduates University of Iowa.

Wamarekani wana utamaduni na mila za kipekee sana. Wanafunzi wamekaa darasani utadhani wako kijiweni wana barizi. Wenyeji wameniekeza kabla vipi naweza ku-connect na darasa langu siku ya kwanza wakanielewa. Nikaweka kwenye projector poster ya Blue Hawaii nikawauliza kama wanamjua huyo kwenye poster.

"That's Elvis..."

Nikawaeleza kwa kifupi historia yangu na Elvis Presley nikiwa na miaka 12. Nikaweka picha yangu nyuma yangu wanesimama vijana wa umri wangu. Hii iliwamaliza kabisa. Darasa lilichangamka na lecture ilimalizika vyema kabisa. Wamarekani wanaamini dunia yote iko kwao kwengine Afrika ni mwitu.

Muhammad Ali hakupata kuwa mbali na mimi hadi kifo chake.

Kitabu chake, "Muhammad Ali My Own Story," ni katika vitabu ninavyovipenda sana. Nilipofika New York nilifika Guy Madison Garden ambako Muhammad Ali alipigana na Joe Frazier 1971 katika pambano lililoitwa, "Fight of the Century." Nilifika pia Central Park kuangalia John Lennon Memorial. Lennon alikuwa mmoja wa The Beatles.

Katika wenyeji wangu New York alikuwa Spiegel ambaye alikuwa rafiki wa karibu sana wa John Lennon. Jana yake alikuwa nyumbani kwa Lennon jirani sana na Central Park na siku ya pili ndiyo Lennon akauliwa kwa kupigwa risasi nje ya nyumbani kwake.

Mimi nilishangaa aliponieleza hili na yeye alishangaa nilipomwimbia nyimbo ya The Beatles, "Things We Said Today," na nikamwambia nikiipiga nyimbo hii kwenye guitar langu Hoffner.

Wakati huo nilikuwa na miaka 16.

333891835_578639200866660_5519900118419920962_n.jpg

335456423_1262469191049945_5850042891668838095_n.jpg

Cassius Clay v Sonny Liston, MIami Beach 1964

334438316_223424066856035_3380240507058261617_n.jpg

Muhammad Ali v Joe Frazier, Guy Madison Garden New York 1971

334419667_600345668798834_8513452081450922321_n.jpg

John Lennon Memorial, Central Park New York
Nadhani picha unayoizungumzia ni ile aliyokuwa anampigia kelele liston aamke waendeleze pambano
 
Muhammad Ali i admire him so much

"On the last week i murdered a rock,
Injured a stone,
Hospitalized a brick,
Am so mean i make medicine sick."

January 17 1942 - June 3 2016.
 
Muhammad Ali i admire him so much

"On the last week i murdered a rock,
Injured a stone,
Hospitalized a brick,
Am so mean i make medicine sick."

January 17 1942 - June 3 2016.
Akhi...
Allah alimpa kipaji na akawa mwingi wa kushukuru.
 
Dagiii...
Mzee alikuwa pia na film projector tukiangalia senema.

Yeye ndiye aliyenifunza mimi kupiga picha.

Alinipa camera mbili aina ya Kodak nikiwa na miaka 12.

Babu yangu nyumba yake ilikuwa ya kwanza kuwa na umeme maji na shower bafuni.

Ziko stori nyingi sana nikiangalia nyuma hushangaa.

Siku moja baba yangu alichukua comic niliyokuwa nasoma akafungua kisha nikamsikia anasema, "Huyu Donald Duck bado yupo hadi leo?"

Sikuamini kuwa baba yangu katika udogo wake 1930s alikuwa akisoma comics.

Yako mengi.
Aliwezaje kupata maisha privileged Enzi za ukoloni ambako hata kununua bia Tu Kwa vibali??natamani utusimulie maisha ya Mzee wako kidogo
 
The Boss...
Iko siku In Shaa Allah nitaeleza hali ya wakati ule sisi tukiwa wadogo tukiwaona baba zetu na maisha yao.

Wakinunua magari mapya si yaliyotumika kama tufanyavyo sisi hivi sasa.

Ghafla maisha haya yakawatoka baada ya uhuru na wengine wakafa wakiwa katika umasikini mkubwa.
 
Watu wa awali kabisa nilioanza kuwafatilia katika jukwaa hili,
Tangu nikiwa sekondari.
Napenda uandishi wake, na mtiririko wake wa mawazo,
Kudos.
 
Ahsante kwa kumbukumbu, kuna binadamu watakuja kusema hiyo ni photoshop...
 
Back
Top Bottom