Category ipi ya movie huipendi?

Category ipi ya movie huipendi?

Forgotten

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,518
Reaction score
10,839
Mimi nitaangalia movie categories zote ila category ya Science Fiction (Sci-Fi) inanipa tabu sana kuangalia movie zake. Nilianza kuangalia movie za Sci-Fi za Spider-Man, miaka hiyo Spider-Man ni movie ambayo lazima uitazame, hii ndio ilinifanya nikawa nafatilia Sci-Fi. Kwenye Spider-Man Marvel wametisha sana, ndio movie pekee ya Sci-Fi ninayoifuatilia kila ikitoka japokuwa sipendi Sci-Fi kwa 99%. Nimetazama zote 1, 2, 3, Spider-Man Homecoming, Spider-Man Far From Home, Spider-Man Into The Spider-Verse.

Movie za mwisho za Sci-Fi kucheki tofauti na Spider-Man ni Black Panther, Venom, Terminator: Dark Fate, tena hizi ni baada ya kuongelewa sana nikaona nisipitwe ila hakuna kitu nili-enjoy kuziangalia.

Kuna siku nlimkuta jamaa anacheki movie ya Sci-Fi nimeisahau jina, akaisifia sana niichukue nikaangalie. Nikakaa nae niangalie kidogo nikashangaa kwenye movie jamaa kapiga kengele kichwa alaf bado mzima hana hata jeraha, nilicheka sana nikajiuliza kwanini movie kama hizi wasiziweke tu kwenye category ya comedy. 😂😂😂 Maana jamaa alipiga diving header moja hatari kama Ronaldo.
 
Hata mimi sipendi sci-fi naonaga ni utoto sana, siwezi kabisa kukaa naangalia maroboti ya ajabu ajabu au viumbe vya ma chuma chuma. Ninapenda love stories na zile movies zilizo base kwenye true events kwa mfano Bunnyman, Texas Chainsaw, yan movies za hivo.
 
Romance huwa hata sizifikirii zinakela ngumi eti ndo kofi halafu Kofi moja tu mtu atalia mpk anakuwa mwekundu! Sijui hawaonagi yale mateke ya kina vandame au ngumi za kina boyker..
U kenge kenge tu.
 
Mkuu wewe uko kama mimi na movie hizo sa sci-fi ulizoangalia ni kama mimi..
Nimeanza kuangalia spiderman tangu utotoni mpaka sasa hivi naangalia spider.. lakini hizi nyingine sijui avengers sijawahi na sina mpango kabisa.. naona kama uongo umezidi.

Napenda movie za magaidi na wizi kama italian job n.k
 
Hizi binafsi sina mzuka nazo
1.science-fiction
2.Historical movies (mamovie ya zamani kama (G.O.T) game of thrones na wenzake.
3.Romance movies.(story za mapenzi mwanzo mwisho)
4.Comedy movies
 
Hata mimi sipendi sci-fi naonaga ni utoto sana, siwezi kabisa kukaa naangalia maroboti ya ajabu ajabu au viumbe vya ma chuma chuma. Ninapenda love stories na zile movies zilizo base kwenye true events kwa mfano Bunnyman, Texas Chainsaw, yan movies za hivo.
Terminator, li-robot linalipuliwa ila linajiunga tena. Hahah!
 
Hizi binafsi sina mzuka nazo
1.science-fiction
2.Historical movies (mamovie ya zamani kama (G.O.T) game of thrones na wenzake.
3.Romance movies.(story za mapenzi mwanzo mwisho)
4.Comedy movies
Hizi historical zinanipaga utata sana pia, nina G.O.T full series ila kuianza ndio mtihani.
 
Back
Top Bottom