Category ipi ya movie huipendi?

Me sizipendi sci-fi,romance na comedy comedy nilizipenda mbili tu ya Mr bean na ya Mr bone pekee basi
 
Hupendi kuchekeshwa mkuu?
Kwangu nyingi zinazoonekanaga za comedy hata sionagi kama zinachekeaha eti.
Kwangu mimi wachekeshaji ni hawa. Mr Ben na Charli champlin kidogo na Jack chan japo yeye huwa ni action lakini kuna ukomedui anawekaga.
 
Aisee kumbe Yuko wengi tusioelewa huo UJINGA wa sci-fi movies nilikuwa najiona mshamba kumbe washamba ni wale waangaliao hizo movie
 
Sci-Fi/Superheroes- siangalii, nishaona Chache kwa sababu maalamu- the amazing spiderman sababu ya actor wake,Black panther sababu ilivuma sana,Spiderman homecoming sababu ya bidada flani, The martian sababu ya actor wake huwa namfuatilia(huwa ni mmoja kati ya favorite actor wangu) Nilijaribu kuangalia Avator,captain america na guardian of the galaxy ila nikakomea robo tu.

Comedy za kizungu- hazinichekeshagi wala sizifurahiagi
 
Kwangu mm movies bora ni Sci-fi action historical na animation ila tu iwe imetoka Hollywood apo utanikamata ila nikikuta movie ya bollywood sijui Korea sijui wap Ata kwa dawa sioni nalala
 
Nilipoona tu neno Sci-Fi nikatafuta limao ili kukata kichefuchefu. Sina la kuongeza zaidi ya kusema pia Superhero movies kama spiderman, the great hulk na wenzake wa aina hio siwakubali in exception of Kingkong kitambo sana niliangaliaga kabla wengi hawajamiliki tv bongo enzi hio tv ni za "National"! Mwisho wangu wa Sci-Fi ni terminator tu.

Pia movie za wanasayansi wanaenda angani sijui mwezini mara madege yanatunguana huko juu. Watu wamejifungia kwenye chumba kina mikompyuta kama dashboard ya ndege hizo hapana, au ndani ya meli hizo pia hapana.

Movie ikianza na wa UK wamepanda ma farasi farasi jangwani ile ki cowboy mara sijui kijiji cha king na queen ki long time pia nabonyeza next button.
 
Hata mimi sipendi za mazombi
 
Ukitaka nisibanduke kwenye TV tupia vitu kama:
1.The Mummy
2.Wrong Turn
3.Piranha
4.Shark night
5.Timberwoods
6.Hills have eyes
7.Texas chainsaw
8.Final destination

Hizi ni thrillers/horrors ila pia adventure flani kama watu wameenda picnic mara majanga yanaanza kutokea huko porini huwa tamu sana.

Nyingine nazopenda ni romantic movies/comedies ila za ki black americans.

Movie za mkono pia nazikubali ila sio ishu sana kama hilo kundi la kwanzau
 
Za kahindi kwa asilimia 90 hapana exception zipo chache kama 3 idiots, my name is khan etc category nyingine kama movie imetumia akili nyingi na story inaeleweka haina shida ilimradi niwe enterteined

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Za kahindi kwa asilimia 90 hapana exception zipo chache kama 3 idiots, my name is khan etc category nyingine kama movie imetumia akili nyingi na story inaeleweka haina shida ilimradi niwe enterteined

Sent using Jamii Forums mobile app
Angalia Drishyam na Andhadhoon, zipo vizuri sana.
 
Horror nzuri sana, raha yake uangalie usiku. πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…