Catherine Ruge: Kakoko alinitishia kuniua baada ya kuibua madudu mengi TPA

Catherine Ruge: Kakoko alinitishia kuniua baada ya kuibua madudu mengi TPA

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Aliyekuwa mbunge wa viti maalum CHADEMA na Katibu mkuu BAWACHA ndugu Catherine Ruge amedai kwamba wakati akiwa mbunge akifanyia kazi kamati ya PAC alitishiwa kifo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA ndugu Kakoko ambaye alikuja kutumbuliwa kwa tuhuma za ufisadi na kushtakiwa mahakamani.

Hali hiyo ilikuja baada ya yeye kuibua Madudu mengi ya ufujaji wa pesa katika Mamlaka hiyo na kubainisha kuwa kulikuwa na baadhi ya watumishi wazalendo wa kutoka mamlaka hiyo walikuwa wakimpa nyaraka za ndani za matumizi mabaya ya pesa ambazo Bwana Kakoko alikuwa akizificha.

Akiongea kwa njia ya mtandao kupitia mjadala unaoendeshwa kupitia mtandao wa Clubhouse, Pia ndugu Catherine Ruge alisema amedokeza anashangaa watu wakihoji alipo aliyekuwa Spika wa bunge ndugu Job Yustino Ndugai wakati yeye anafahamu kuwa yupo Katika matibabu hospitali ya Apollo nchini India na Kuna ulinzi mkali umeimarishwa katika mahali alipo mgonjwa.

Taarifa za kuugua kwa Ndugai, Catherine Ruge amedai kuwa amezipata kutoka kwa mdogo wake ambaye walikuwa wakitibiwa pamoja katika hospitali hiyo.
 
Back
Top Bottom