Catherine Ruge: Kakoko alinitishia kuniua baada ya kuibua madudu mengi TPA

Catherine Ruge: Kakoko alinitishia kuniua baada ya kuibua madudu mengi TPA

Ndugai atakuwa pressure ilimpanda baada ya kulazimishwa kujiuzulu, na huo ulinzi wanaompa huko India serikali wanaogopa asije kutoa siri ya waliomuandikia barua ya kujiuzulu.
Ndugai alimkana JPM. Akaamua kuanzisha Bandari yao ile. Na yeye akaishia kukanwa mbele ya kadamnasi. Mambo ta Tit for Tat. Apambane na hali yake
 
Aliyekuwa mbunge wa viti maalum CHADEMA na Katibu mkuu BAWACHA ndugu Catherine Ruge amedai kwamba wakati akiwa mbunge akifanyia kazi kamati ya PAC alitishiwa kifo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA ndugu Kakoko ambaye alikuja kutumbuliwa kwa tuhuma za ufisadi na kushtakiwa mahakamani.

Hali hiyo ilikuja baada ya yeye kuibua Madudu mengi ya ufujaji wa pesa katika Mamlaka hiyo na kubainisha kuwa kulikuwa na baadhi ya watumishi wazalendo wa kutoka mamlaka hiyo walikuwa wakimpa nyaraka za ndani za matumizi mabaya ya pesa ambazo Bwana Kakoko alikuwa akizificha.

Akiongea kwa njia ya mtandao kupitia mjadala unaoendeshwa kupitia mtandao wa Clubhouse, Pia ndugu Catherine Ruge alisema amedokeza anashangaa watu wakihoji alipo aliyekuwa Spika wa bunge ndugu Job Yustino Ndugai wakati yeye anafahamu kuwa yupo Katika matibabu hospitali ya Apollo nchini India na Kuna ulinzi mkali umeimarishwa katika mahali alipo mgonjwa.

Taarifa za kuugua kwa Ndugai, Catherine Ruge amedai kuwa amezipata kutoka kwa mdogo wake ambaye walikuwa wakitibiwa pamoja katika hospitali hiyo.
Sasa aweke huo ushahidi sio unafiki
 
Ndugai atakuwa pressure ilimpanda baada ya kulazimishwa kujiuzulu, na huo ulinzi wanaompa huko India serikali wanaogopa asije kutoa siri ya waliomuandikia barua ya kujiuzulu.
Hivi kumbe hakuandika mwenyewe hiyo barua?
 
Nchi zetu ni bora tu zingeendelea kuwa chini ya wakoloni japo nao wangelikuwa na matatizo yao.
Omujubi, mtu anaweza kusoma hii comment yako kwa haraka asikuelewe lakini ninahisi tungekuwa tumeendelea zaidi. Kuna viongozi wanaihujumu hii nchi utafikiri wao siyo watanzania, kwamba kuna nchi nyingine wanapeleka wanavovipora TZ. Hata aliyeazimwa koti hawezi kulitumia vibaya namna tunavyoona. Haiingii akilini, najiuliza inakuwa je kila mahali ni madudu?
 
Nchi zetu ni bora tu zingeendelea kuwa chini ya wakoloni japo nao wangelikuwa na matatizo yao.
Jisemee mwenyewe, ukitaka utumwa ni wewe tu nenda Ulaya au Uarabuni ukatumikishwe kama mtumwa.
Hela nzuri tu.
 
Kakoko kaiba sana.

Nenda Kigoma kuna taarifa zake.
No kwa taarifa yako kakoko ni hakuwa kiongozi mzuri alikuwa mnoko mnoko kiasi kwamba wafanyakazi wake wa chini wakamzidi mbinu. Kulikuwa na vinara wa wizi hapo TPA ambao ndiyo walimchafulia na kibaya kulikuwa na michepuko ya wakubwa akawa anaogopa kuigusa (rejea Majaliwa).
 
Back
Top Bottom