Catherine Ruge: Kakoko alinitishia kuniua baada ya kuibua madudu mengi TPA

Aliyekuwa mbunge wa viti maalum CHADEMA na Katibu mkuu BAWACHA ndugu Catherine Ruge amedai kwamba wakati akiwa mbunge akifanyia kazi kamati ya PAC alitishiwa kifo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA ndugu Kakoko ambaye alikuja kutumbuliwa kwa tuhuma za ufisadi na kushtakiwa mahakamani.

Hali hiyo ilikuja baada ya yeye kuibua Madudu mengi ya ufujaji wa pesa katika Mamlaka hiyo na kubainisha kuwa kulikuwa na baadhi ya watumishi wazalendo wa kutoka mamlaka hiyo walikuwa wakimpa nyaraka za ndani za matumizi mabaya ya pesa ambazo Bwana Kakoko alikuwa akizificha.

Akiongea kwa njia ya mtandao kupitia mjadala unaoendeshwa kupitia mtandao wa Clubhouse, Pia ndugu Catherine Ruge alisema amedokeza anashangaa watu wakihoji alipo aliyekuwa Spika wa bunge ndugu Job Yustino Ndugai wakati yeye anafahamu kuwa yupo Katika matibabu hospitali ya Apollo nchini India na Kuna ulinzi mkali umeimarishwa katika mahali alipo mgonjwa.

Taarifa za kuugua kwa Ndugai, Catherine Ruge amedai kuwa amezipata kutoka kwa mdogo wake ambaye walikuwa wakitibiwa pamoja katika hospitali hiyo.
Kupoteza Uspika tu tayari anaumwa?🤣🤣
 
Yaani kutoka Ikulu kukutana na Mheshimiwa mpaka kurudi Apollo.... Hii inafikirisha.
 
Kama kwenye foma spika anatibiwa chini ya "Ulinzi Mkali".... maisha kama gwaride, nyuma geuka moja, wa kwanza amekuwa wa mwisho... mkaa ule ule ulikuwa unachomea nyama choma, leo unakuchoma mwenyewe.
 
Ndugai atakuwa pressure ilimpanda baada ya kulazimishwa kujiuzulu, na huo ulinzi wanaompa huko India serikali wanaogopa asije kutoa siri ya waliomuandikia barua ya kujiuzulu.
mwache avune alichopanda
 
Mbona unazungumzia Ndugai kama sub stori wakati inaonekana ni habari iliyokamilika?

Nini kinaendelea kwa Ndugai?
Ndugai anaumwa kalazwa Appolo anasumbuliwa na maradhi lukuki ikiwemo alipandikizwa Figo na wanadai ana yale mambo ya Gridi ya taifa sasa unajua grid ya taifa ina tabia ya kupunguza akili akaropoka.
 
Ndugai atakuwa pressure ilimpanda baada ya kulazimishwa kujiuzulu, na huo ulinzi wanaompa huko India serikali wanaogopa asije kutoa siri ya waliomuandikia barua ya kujiuzulu.
Mkuu kisukari na hasira ni sumu, ukimkwaza mwenye sukari ni nusu kifo kwake
 
Back
Top Bottom