Caught kissing on camera! do I need to bribe the IT guy?

Caught kissing on camera! do I need to bribe the IT guy?

Nadhani hiki kisa umekitoa somewhere, na haijakutokea
kwani haukusoma pale juu mwanzo wa maelezo? 'Nanukuu'

oooooh I see...

Posts: 8
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
 
Kaka kwani katika iyo record si utaonekana ukilazimishwa!!? Mwenye msala sasa utakuwa ni wewe au uyo binti!!? Mi sioni whats wory u??
 
Nadhani hiki kisa umekitoa somewhere, na haijakutokea
Does not matter......... unachotakiwa kufanya ni kutoa maelekezo....... what difference does it make iwe imemtokea yeye au mtu mwingine...???
 
Does not matter......... unachotakiwa kufanya ni kutoa maelekezo....... what difference does it make iwe imemtokea yeye au mtu mwingine...???
lakini vipi wewe mchangowako? unamtazamo gani juu ya hali ha huyu jamaa?
 
lakini vipi wewe mchangowako? unamtazamo gani juu ya hali ha huyu jamaa?
Jamaa ajieleze mapemaaa kwa mkewe.......maana akiacha wambeya wampelekee.......itamfikia ikiwa na chumvi nyingiiiiiii........... Na kuhusu kusemwa kwa bosi sidhani kama ni kitu cha kuogopa, labda kama kilichotokea kinavunja sehemu ya sera ya mahala anapofanyia kazi. Pamoja na hivyo........ kama ilivyokwisha semwa hapo juu..hiyo video si itaonyesha jinsi alivyokuwa analazimishwa...??? Hivyo hana haja ya kuhofu wala kuliwa hiyo 2.5m.
 
Kuna Mangungo wana fantasies hapa!

Avumaye Shigongo, kumbe wengine wamo.
 
Nanukuu...

Mimi ni mfanyakazi wa kampuni fulani hapa Dar. Ni muajiriwa yapata miezi mi 4 sasa. Tangu nianze kazi hapo kuna dada ambaye ameonyesha kila dalili ya kutaka kuwa na mimi kimapenzi! Ninafamilia na watoto kwahiyo sipendi kujihusisha katika mambo kama hayo. Siku moja wakati wa sherehe ya kuwapongeza baadhi ya wafanyakazi huyu dada alinibana katika kona akataka kunibusu (busu kubwa) lakini nilimzuia na hakufanikiwa!

Siku mbili baadae nilipokuwa nikiingia kazini asubuhi kwa kutumia 'elevator' mambo yalikuwa sivyo kwani dada huyo aliingia katika 'elevator' ambayo mimi nilikuwemo kupitia floor ya 2! Kwabahati mbaya tulikuwa wawili tu! Baada ya kuingia na kuanza kuelekea floor ya 6 hapo katikati alinikumbatia ghafla huku akinibusu kwa lazima! Kitendo hicho kilinihuzunisha kwani halikuwa lengo langu pia nilijua mule ndani ya 'elevator' kuna kamera za ulinzi!!

Ilipofika saa kumi jioni mtu wa IT wa kampuni yetu alinipigia simu kwamba anamazungumzo nami na aliniambia kwamba ameona vyoote 'tulivyofanya katika elevator'

Ameniomba nimpe Tshs. 2.5M haraka iwezekanavyo ili aweke kapuni hizo picha na kama sivyo basi atazipeleka kwa bosi!!!

Sasa mimi uwezo wangu ni mdogo kwani hizo pesa sina...

Je, nikambembeleze huyu IT amezee? Nikajikamatishe kwa bosi na kumueleza ukweli? Je, mke wangu akijua itakuwaje kwani nashindwa namna ya kumuelezea!!

Naomba msaada wenu...

Hii ni story ya kutunga. Tafadhali uweke hapa jambo ambalo halitapotezea wanachama muda wa kujibu. Unless uniambie kuwa wewe ni mwanamke na ni mwanaume anakulazimisha mahusiano ya kijinga.

Anyway, sehemu za kazi nyingine ni kama guest bubu!!! Baadhi ya watu wanatumia meza za maofisi kufanyia uharamia wao. Heshima iko wapi?? Na wewe unakubali kubusiwa au kufanya uzinzi ndani ya ofisi?? Na kama hutaki tabia hiyo mbona hukuripoti kwa utawala from the begining??? Nawe ulipendezewa na kadri siku zingeendelea vibrators zingezidi ungekubali. Sasa unahaha kwa kuwa umegundulika. Tafadhali uwe unaandika kwa font kubwa. Asante.
 
umejaribu kutunga stori nzuri ila ina mapungufu mengi,kaa chini ui edit acha kutuchanganya
 
... Ameniomba nimpe Tshs. 2.5M haraka iwezekanavyo ili aweke kapuni hizo picha na kama sivyo basi atazipeleka kwa bosi!!!
Na huyo dada je, yeye ameombwa atoe nini ili asipelekwe kwa boss?
 
kama umekuwa mwaminifu kwa mke wako kwa kipindi chote mweleze hali ilivyo,hilo huenda ni dili kati ya huyo mtu wa IT na huyo dada dunia haifai kwa sasa watu wanambinu nyingi sana za kujipatia kipato,huenda hata siku ya sherehe kuna mtu alibana mahali na kamera ungekisi nae picha inapigwa unaletewa na kutishiwa picha kufika kwa wakubwa,na kama bosi anajua utendaji wako huyo mtu wa IT acha afikishe hizo picha ukajitetee maana unaweza toa hizo siku nyingine akakuambia nipe laki 5 au nipeleke picha kwa mkeo.Mpe kubwa usitoe hata mia,labda kama ulishawishika na wewe ukaonyesha kuzama kwenye kisi la huyo dada
 
Mwambie huyo muomba rushwa wa IT/SECURITY hiyo hela akachukue kwa mwanamke aliyekuattack,kwani hata kwenye camera itaonyesha jinsi ulivyokuwa unahangaika kujinasua mikononi mwake vinginevyo ulitulia tu haukonyesha dalili za kutopenda jambo ulilokuwa unafanyiwa na huyo dada,kiongozi Stuka!!!
 
Pole sana ndugu yangu kwa Majaribu haya.Ninajua jambo moja,kweli itakuweka huru.Go tell truth and the peace of the Lord will be with you.
Aaaaamen! hii itasaidia kidogo(labda saana)
kumbuka une faute avouée est en moitié pardonnée
 
mjinga huona kila kitu ni ujinga! Nothing personal....


ni ujinga mtupu,
eti tanzania hii mwanaume utolewe milioni mbili
kwa sababu ya kum kiss mwanamke???????
Hivi vistory vyako havina kichwa wala miguu..
 
ujinga mtupu?

Mtu ameomba ushauri wewe unasema ujinga mtupu na nikiangalia hapo wewe ni 'Senior Expert member'.....Amazing!!Grow up!Sio lazima uchangie kila kitu ili kuosha kinywa tu.Be considerate!!!
 
Pole sana ndugu yangu kwa Majaribu haya.Ninajua jambo moja,kweli itakuweka huru.Go tell truth and the peace of the Lord will be with you.

mzee umedesa kwenye muvi ya obsessed nini? Kwani ulilainika ukala denda? Cha msingi hizo picha zinaonyesha kuwa mwanamke ndo anatumia nguvu, sasa unaogopa nini? Pia huyo IT mkamatishe takukuru
 
mtu ameomba ushauri wewe unasema ujinga mtupu na nikiangalia hapo wewe ni 'senior expert member'.....amazing!!grow up!sio lazima uchangie kila kitu ili kuosha kinywa tu.be considerate!!!

wewe humjui huyu pape...
Kila siku anakuja hapa na
story za aina hii.haziko sincere....
Zimejaa plots za kubuni.

Hakuna mlinzi wa kampuni atakae thubutu kukudai pesa
kwa sababu umem kiss mwanamke kwa hiari yake.
Halafu bosi wa kampuni inamuhusu nini kama
wewe umeoa na ume mkiss mwanamke mwingine?
 
Back
Top Bottom