Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilikuwa nimendika tusi nimelifuta, uwe mwerevu wa kufafanua badala kuandika as if layman. Nenda jifunze kwa JP Morgan na PPP ya railway. Usipende kudakia usivyovijua fisadi mkubwa. Tunamuunga mkono Mh. Kafulila, tumtie moyo na kumsapoti. Miradi mingi yenye PPP msimamizi anakuwa ni private, na private siku zote wanataka ku maximize profit at the same time public sector inataka ku maximize utoaji wa huduma unakuta mafanikio ya miradi ni makubwa. Hiyo ya kifisadi ka ulivyoninga inaharibiwa toka mwanzo yaani unakuta in fact aliyeingia ubia na serikali hana kabiss uwezo yaani ni dalali nadhani kosa hilo lilifanyika na Mzee Mkapa na Kigoda yaani watu waliuziana/kupeana viwanda wakiwa hawana ujuzi wala uwezo wa kuviendesha. PPP inataratibu zake. Mh. Kafulila yupo serious na utaratibu na taratibu ndiyo maana we expect no au few failures kwa sababu ya umakini.Bado unayo safari ndefu ya kujifunza.
Hahahaha nenda lecturer theatre utachoka, yaani facilities nyingi za madarasani ovyo sana, halafu mijitu imekomaa na eti mabweni 😂Maprofesa na watu wanapoteza muda kuongelea ujenzi wa mabweni.
Hahahahaha, hivi vyuo ndio maana hata elimu wanazotoa zimekuwa changamoto.
Karne ya 21 mnakaa kujadili ujenzi wa mabweni? na kujiona magenius.
dah aisee.
Nakubaliana na wewe haya mambo ya Serikali yanatupa gharama kubwa ambazo sio za msingiHakuna ufisadi kwa sababu KPI za PPP zinajulikana na kwa sababu muendeshaji ni private pia so unakuta kila kitu kipo safi
Kama asipoelewa hii basi amtafute Kafulila mwenyeweNilikuwa nimendika tusi nimelifuta, uwe mwerevu wa kufafanua badala kuandika as if layman. Nenda jifunze kwa JP Morgan na PPP ya railway. Usipende kudakia usivyovijua fisadi mkubwa. Tunamuunga mkono Mh. Kafulila, tumtie moyo na kumsapoti. Miradi mingi yenye PPP msimamizi anakuwa ni private, na private siku zote wanataka ku maximize profit at the same time public sector inataka ku maximize utoaji wa huduma unakuta mafanikio ya miradi ni makubwa. Hiyo ya kifisadi ka ulivyoninga inaharibiwa toka mwanzo yaani unakuta in fact aliyeingia ubia na serikali hana kabiss uwezo yaani ni dalali nadhani kosa hilo lilifanyika na Mzee Mkapa na Kigoda yaani watu waliuziana/kupeana viwanda wakiwa hawana ujuzi wala uwezo wa kuviendesha. PPP inataratibu zake. Mh. Kafulila yupo serious na utaratibu na taratibu ndiyo maana we expect no au few failures kwa sababu ya umakini.
Huyu nae ni chizi zile km2000 za PPP zipo wapi Hawa ndo wanao mwingiza madam kingMkurugenzi mkuu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na sekta Binafsi (PPP), Bwana David Kafulila amevitaka vyuo vya umma nchini kutumia sekta binafsi kujenga mabweni/Hosteli na miradi mingine mbalimbali kwa ubia na sekta binafsi jambo ambalo halihitaji fedha za Serikali.
Amesema miradi ya ubia inainufaisha zaidi serikali kwani inapata teknolojia mpya na za kisasa kutoka sekta binafsi na kusaidia uchumi wake kuendeshwa kisasa zaidi na kwa ufanisi.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa chuo hicho kilichojadili utekelezaji wa mradi wa ubia wa ujenzi wa mabweni yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 12,000.“CBE imeonyesha njia, imetengeneza template|andiko ambalo vyuo vingine vinapaswa kuiga kwa kujenga mabweni kwa ubia bila kuomba fedha Toka hazina ,” amesema Kafulila.
Amesema mamlaka zote za serikali zinazotekeleza miradi mbalimbali ziangalie uwezekano wa kuhusisha sekta binafsi kwenye utekelezaji wa miradi hiyo badala ya kusubiri fedha za serikali.
Amesema kila mradi ambao sekta binafsi inaweza kuutekeleza ni vyema taasisi za serikali zikaingia ubia nazo ili kuharakisha utekelezaji wake na kuokoa fedha za serikali ambazo zingetumika.
“Kila mradi ambao sekta binafsi inaweza kuutekeleza kwa teknolojia ya hali ya juu kuliko serikali basi apewe autekeleze ili tujenge uchumi wa kisasa ambao sekta binafsi ndiyo inanafasi kubwa ya kutengeneza ajira nyingi,” amesema
Ameipongeza menejimenti ya CBE kwa kuratibu mradi wa ujenzi wa mabweni hayo ambayo yatakapokamilika yataondoa uhaba wa makazi ya wanafunzi kwenye kampasi ya chuo hicho hapa jijini Dar es Salaam.
Kafulila amesema serikali iliamua kuweka utaratibu wa kuweka miradi kwa ubia ili kunufaika na mambo manne ikiwemo kutekeleza miradi yake bila kutumia fedha zake au mikopo kutoka mataifa ya nje.
“Utaratibu wa ubia unaleta unafuu kwa serikali kwasababu miradi inajengwa bila kutegemea fedha zake lakini utaratibu huu wa ubia unafanya serikali ivute teknolojia ya kujenga baadhi ya miradi, teknolojia ambayo kwa kiasi kikubwa inapatikana sekta binafsi,” amesema
Amesema kwa utaratibu wa ubia serikali inanufaika na teknolojia ya kisasa ambayo inapatikana kwenye sekta binafsi na kupata fursa ya kuleta weledi kwenye taasisi zake kama CBE.
“Kwa mfano mabweni haya yatakapojengwa na kukamilika mwekezaji atalipa kodi kwa serikali lakini kama ingejenga yenyewe ingekuwa huduma tu na hakuna kodi ambayo serikali ingepata kwa hiyo utaratibu huu unainufaisha sana serikali,” amesema.
Mkuu wa chuo hicho, Proesa Edda Lwoga, amesema mabweni hayo yatakayojengwa kwenye kampasi kuu ya Dar es Salaam yatakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,728 hivyo kupunguza pengo kubwa la malazi kwa wanafunzi.
Amesema kwa sasa kampasi ya CBE Dar es Salaam ina jumla ya wanafunzi 12,000, ambapo kwa upande wa malazi kampasi ina majengo mawili tu ya bweni yenye uwezo wa kuchukua vitanda 160 pekee vya malazi kwa wanafunzi wa kike na kiume hivyo vinakidhi uhitaji wa malazi kwa asilimia 1.3 tu.
Mkuu wa chuo amesema mradi huo utakapokamilika unatarajiwa kupunguza changamoto ya malazi kutoka asilimia 1.34 iliyopo mpaka asilimia 30 ya mahitaji ya wanafunzi kwa bweni.
“Hali iyopo imesababisha uhitaji mkubwa wa malazi ya wanafunzi kwa asilimia 98.6 hivyo wengi wanalazimika kutafuta malazi nje ya chuo kwa gharama kubwa, jambo linalosababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kumudu gharama hizo,” amesema.
Hili lipo chini ya Private wenyewe hata kama ni wewe unapesa changamkia tu fursaUnajua kidogo nimeanza kumwelewa huyu Kafulila,
Kama tutajenga Hosteli kwaajili ya CBE kwanini pia PPP wasijenge kwaajili ya shule za Kata au vyuo bidogo na vya kati?
PPP = private public partnershipsUnajua kidogo nimeanza kumwelewa huyu Kafulila,
Kama tutajenga Hosteli kwaajili ya CBE kwanini pia PPP wasijenge kwaajili ya shule za Kata au vyuo bidogo na vya kati?
Mimi naamini Ujenzi ni mchakatoHuyu nae ni chizi zile km2000 za PPP zipo wapi Hawa ndo wanao mwingiza madam king
Kha..unanongwaa isee!Maprofesa na watu wanapoteza muda kuongelea ujenzi wa mabweni.
Hahahahaha, hivi vyuo ndio maana hata elimu wanazotoa zimekuwa changamoto.
Karne ya 21 mnakaa kujadili ujenzi wa mabweni? na kujiona magenius.
dah aisee.
Sasa hapo ni Kafulira ndio katoa wazo au ubunifu wa CBE?Unajua kidogo nimeanza kumwelewa huyu Kafulila,
Kama tutajenga Hosteli kwaajili ya CBE kwanini pia PPP wasijenge kwaajili ya shule za Kata au vyuo bidogo na vya kati?
Nakubaliana na wewe,PPP = private public partnerships
Hapo ni taasisi yenyewe za serikali kuchangamka na wakubwa wa taasisi hizo wabadili mitazamo yao hukusu sector binafsi maana hii Tanzania hawa wakuu wa taasisi wanachukulia sectors binafsi kama mpinzani wao..
Unaweza kwenda na wazo nzuri halmashauri kwa ajili ya shule au vituo vyao vya afya wao wakakuona kama jasusi vile nadhani wanabanwa sana huko juu ni kama huwezi kufanya kitu bila mwanasiasa huko juu kujua hicho kitu kina maslahi gani kwake kwanza..
Anayehimiza PPP ni Kafulila tu nchi hii Mimi nadhani apewe maua yakeSasa hapo ni Kafulira ndio katoa wazo au ubunifu wa CBE?
Samia ni pro-business ndio maana anaweka watu wanaweza kujali biashara
Anahomiza au yeye ni Kamishna wa miradi ya PPP na sheria ameikuta?Anayehimiza PPP ni Kafulila tu nchi hii Mimi nadhani apewe maua yake
kweli wewe nyau,Maprofesa na watu wanapoteza muda kuongelea ujenzi wa mabweni.
Hahahahaha, hivi vyuo ndio maana hata elimu wanazotoa zimekuwa changamoto.
Karne ya 21 mnakaa kujadili ujenzi wa mabweni? na kujiona magenius.
dah aisee.
Wewe raia umefanya Nini?
Kafulila ni Mtanzania halisi kabisa
Mimi PPP Asikuwahi kuijua ila Sasa kwa KAFULILAAnahomiza au yeye ni Kamishna wa miradi ya PPP na sheria ameikuta?
Unajua daraja la Kigamboni limejengwa Kwa utaratibu gani? 🤣🤣🤣🤣
Sababu ni zipi?Ngedere anaweza asiwe raia kweli
Sasa utaijuaje wakati hufuatilii mambo ya Uchumi na Biashara?Mimi PPP Asikuwahi kuijua ila Sasa kwa KAFULILA