Na hawa ndiyo magreat thinkers wetu wa siku hizi ambao chuki za udini zimewatawala kwa kila jambo hata pasipohusika!!Kuna mtu ameambiwa avae hijab kweli hapo?hivi unapajua CBE kweli wewe?umeshawahi kuwaona wanafunzi wa kike wanavyovaa?Nauhakika kama wewe ni mzazi usingethubutu kumruhusu mwanao wa kike avae vile,hebu vitu vingine jamani tuache ushabiki usio na kichwa wala miguu!!
Utandawazi upo sana tu lakini tunacopy vibaya,hata hao tunaowacopy hawavai nguo za namna hiyo wanapokuwa shuleni/vyuoni.Hivi dada zetu huwa mnakuwa comfortable kabisa na vile vinguo vyenu kweli?Naunga mkono kwa 100% uamuzi uliofikiwa na uongozi wa CBE juu ya mavazi,wasiishie Campus ya Dar peke yake waende mpaka Dodoma pia maana na ile imekuwa kama danguro la waheshimiwa kipindi cha vikao vya bunge!!
Mkuu umeshindwa kujibu hoja matokeo yake unaingia kwenye "character assassination" Sidhani kama hapa JF kuna vigezo ambavyo eti ndo standard ya great thinker, imekuwa desturi kwa baadhi ya members kama hawakubaliani na mawazo ya wenzao basi jibu lahisi ni kuhoji u great thinker wa wenzao, aibu!!!!
Tukirudi kwenye mada husika
1. CBE kama chuo kinaweza kuwa na mamlaka ya ku enforce a dressing code ndani ya mipaka ya chuo ila nina wasiwasi kama high learning institutions hapa bongo zina dressing code policy, hivyo uamuzi wa namna ya kuvaa umeachwa mikononi mwa wanavyuo wenyewe wa kike na wakiume, na hili ni jambo la kujivunia kwa sababu linawapa watu uhuru wa kuamua juu ya wanavyotaka kuishi maisha yao bila kuingiliwa na mamlaka au wahuni.
2. Kama CBE wamegundua kuwa uvaazi wa wanafunzi wa kike unachangia kutofaulu kwa wanafunzi (wakike? wakiume? wote?) basi jukumu lao ni kuripoti kwa vyombo husika na siyo kujiamlia wenyewe. Kuna mamia ya vyuo nchini vyenye wanafunzi wa kike na kiume je iweje CBE tu ndo wasifaulu kwa ajili ya mavazi na vyuo vingine visiathirike? hapa panahitaji utafiti wa kina sababu inaweza kuwa ni tofauti kabisa na mavazi, je kuna walimu wakutosha wenye qualification zinazostahili kufundisha hayo masomo au ni wale wa kuchakachua vyeti na udungunization? je kuna nyezo za kufundishia za kutosha? je wanafunzi wanapata mahitaji muhimu ya malazi, chakula, umeme, maji nk bila usumbufu au kuingilia utaratibu wa masomo yao? haya yote na mengineo ni lazima yaangaliwe kabla ya mjinga mmoja ku conclude na kutoa maamuzi ya kijinga
3. Enforcement of dressing code, kwanza kwa nini wasichana tu ndo wawe affected?? je hao walinzi wana uzoefu gani na mavazi ya kike ili waamue linalostahili na lisilostahili? Hapa unawapa walinzi nafasi ya kuchukua rushwa ya ngono au pesa kutoka kwa wanafunzi ili kuwaruhusu kutoka na mavazi wanayoyataka na suala zima ni unyanyasaji tu wa kijinsia!!!!
4. Mob justice - kuwahukumu wanafunzi wa kike kwa mavazi yao siyo sahihi hakuna tofauti ya kumkoromea msela mitaani mwizi! mwizi! mwizi! na kumsababishia mauti
5. Mahakama ya kadhi - nimelileta hili jambo kwa sababu ukiangalia mtitiriko mzima wa suala hili unashangaa, Tanzania ni secular country, haina sheria za mavazi au marality. Sasa inakuwaje uongozi wa chuo unajichukulia maamuzi kama haya?? kwa nini suala kama hili ambalo linagusa maisha ya maelfu ya watu liamriwe kiholela holela tu bila kutumia vyombo husika?? Nchi zenye sharia (kadhi) ndo mambo kama haya yanafanyika na kwa vile kuna wale wanaopenda tanzania pia ifuate taratibu hizo wanaweza kuwa wanaanza kujipenyeza kidogo kidogo na kupanda hizo mbegu za kadhi
6. Wale tunaoipenda nchi yetu na tunafurahia uhuru tulionao hivi sasa bila kujali itikadi za kiimani, tusikubali kuingiziwa taratibu tatanishi kama hizi kwenye sekta zetu za umma iwe kwenye mabenki, mashule, vyuoni, maofisini nk . Kuna usemi wa haba na haba ujaza kibaba, tusipokuwa makini sasa hivi tutakuja shtuka when is too late!!!
7. Ushauri wangu wa CBE na watanzania wote ambao tunakerwa na uvaaji wa vijana wetu ni kwamba tutumie sheria na vyombo vilivyopo, mawizara, NGOs, bunge nk ili tupate mwafaka wa suluhisho la hili tatizo badala ya kuwachia wale wenye ajenda za siri kutumia mwanya huo kwa lengo la kutimiza yale waliyokusudia. MUNGU IBARIKI TANZANIA