CCM acheni utaratibu wa kubeba wanafunzi kwenye mikutano kwa maelekezo wasivae nguo za shule. Mnamdanganya nani?

CCM acheni utaratibu wa kubeba wanafunzi kwenye mikutano kwa maelekezo wasivae nguo za shule. Mnamdanganya nani?

Nimeshuhudia hii katika uwekaji wa jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda Cha sukari kilombero K4. Yaani ni aibu
 
Na walimu wote kulazimishwa kuhudhuria na kusaini asiyesani hutishiwa kuchuliwa hatua kali huu ni uonevu na udhalilishaji kwa walimu.
 
Nimeona hii inafanyika maeneo mengi anapopita Rais, sasa hapa sasa lengo huwa ni kumdanganya nanii? Je? Rais, wananchi, vyombo vya habari au nani?

Watoto darasa la 5,6,7 na wanafunzi wa sekondari na vyuo wanabebwa na malori,wengine na mabasi kutoka maeneo mbali mbali hata kama ni siku za masomo.

Watoto wanaahirishiwa masomo kwa ajili ya kubebwa kwenda kwenye mkutano wa Rais ,hii maana yake ni nini hasa? Huu ni ujinga ulio pitwa na wakati kabisa na unakiuka misingi ya haki.

Chama kikishakaa madarakani muda mrefu hupoteza mvuto, baada ya hapo huanza kutumia nguvu ya dola kuhadaa umma kuwa kinakubalika. Matokea yake ndio hayo ya kusomba wanafunzi ili kujaza mikutano yao.
 
Wajanja sana barua inaelekezwa kwa idara ya elimu tuu halafu maelekezo mengine yanakuja kwa mdomo watoto wasivae nguo za shule 🤣🤣🤣
 
Tuma picha ili kuthibitisha hoja yako
Kabla ya mimi kumaliza shule hiyo ilikuwa taratibu tunarudishwa shule nakuambiwa twende kwenye mikutano ya ccm. Hata usiwe na picha hiyo ndio hali halisi labda ukatae tu kwa ubishi.
 
Back
Top Bottom