erasto Samwel
Member
- Sep 10, 2024
- 78
- 91
Kutokukubaliana na maamuzi ya wananchi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka ni sawa na kuzuia maendeleo.
Wagombea wanapojinadi, wananchi hupata nafasi kubwa ya kuchagua kiongozi wanayeamini ataleta maendeleo.
Hata hivyo, CCM mara nyingi huonyesha utayari wa kupinga maamuzi ya wananchi kwa kuwachagulia viongozi wasiokubalika, kama vile mlevi, fisadi, au mwizi. Hali hii haileti maendeleo bali inarudisha nyuma juhudi za wananchi.
Kuna tukio la diwani mmoja wa CCM katika eneo fulani ambaye, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mitaa, aliwaambia wananchi wake: "Hongereni kwa kumchagua kiongozi mliyetaka, lakini mmetupa mzigo wa kubatilisha matokeo yenu ili kumuokoa Katibu Kata wa CCM asiangukiwe na pikipiki aliyokuwa amepewa na chama. Hata hivyo, huyo tuliyewaletea ni mzigo."
Hii inaonyesha wazi kuwa CCM wako tayari kuwachagulia wananchi viongozi ili waje kusaidia viongozi waliowekwa madarakani na chama, badala ya kuwatumikia wananchi. Hali hii haiwezi kuleta maendeleo ya kweli.
Katika uchaguzi uliopita, CCM walilazimisha matokeo yasiyo na haki kwa kutumia mabavu, ghiliba, na udanganyifu. Hii ni dalili ya chama kisichokubali demokrasia au mawazo mapya ya kiuongozi kutoka kwa watu wengine. Kwa kufanya hivyo, mnakuwa wapinga maendeleo kwa kushindwa kuheshimu maamuzi ya wananchi ya kujiletea maendeleo katika maeneo yao.