CCM, Angelina Mabula na Stanslaus Mabula, hizo nyumba zilizouzwa na Jiji la Mwanza zinaenda kuwa ajenda ya kwanza ya wapinzani. Mtatikiswa!

CCM, Angelina Mabula na Stanslaus Mabula, hizo nyumba zilizouzwa na Jiji la Mwanza zinaenda kuwa ajenda ya kwanza ya wapinzani. Mtatikiswa!

Sasa Malima kazaliwa Dar, wewe umekulia milimani huko unajiita mtoto wa mjini?

Mtoto wa Waziri, tena wa fedha, Ofisi ya msajili wa hazina ilikuwa chini yake, alishakuwa Waziri, anajua taratibu zote za mali za serikali.
Huku kakutana na watu wa kazi na si watu wa maneno mengi, huku akiendekeza uswahili kama wa Dar hatoboi.
 
Acha propaganda, hizo nyumba za matope zilizouzwa katikati ya mji ziliuzwa kufuata taratibu zote na order ilitoka ofisi ya rais, wewe kama umelipwa na hilo zee liswahili maneno mengi(adamu malima), na kama hawakumpa fungu la kutosha mwambie kamnofu kalikuwa ni kadogo.
Haki ya myonge itapatikana tu kama zilifata utaratibu uyo mkurugenzi kasimamishwa kwa kosa gani!?
 
Stanslaus Mabula, wewe ndio mbunge wa Nyamagana, bila shaka unalijua Jimbo linakuwaga la moto, hasa ukizingatia "sponsor kafa".
1673763135811.png
 
Mnakiri mmeuza kwa nusu bei, na huyo wa juu mtasema ni nani, maana maafisa ardhi kwa Sasa Kila wakiuza kiwanja ca serikali wanasema amenunua ridhiwani kikwete na ndiye kawapa order, Kila mmoja atatoa hesabu yake
Unajua kujifirahisha hii ishu imeshaisha lkn huyo mzee ambaye anabebwa na serikali muds wake hapa Mwanza umekaribia kuisha.
 
Haki ya myonge itapatikana tu kama zilifata utaratibu uyo mkurugenzi kasimamishwa kwa kosa gani!?
Hii nchi ni ya ajabu sana, unazani mkurugenzi anaweza kufanya hivyo bila baraka kutoka juu kwani yeye hapendi kibarua chake.
 
Hii nchi ni ya ajabu sana, unazani mkurugenzi anaweza kufanya hivyo bila baraka kutoka juu kwani yeye hapendi kibarua chake.
Sisi tunamwaga maji kwenye shimo, maji yakijaa nguchiro mtakosa hewa, mtaibuka tu, mkiibuka tunakata kichwa
 
Rais Samia amefungulia mikutano ya hadhara, na katika majiji ambayo Chadema wanajiwinda kuyadhibiti ni Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam. Wanatafuta ajenda nzito za kutikisa na kuwashika wananchi.

Arusha walifanya tukio, Sasa hivi wote wananyea debe, angalau wanaarusha wanaelewa hatua zimechukuliwa.

Kwa Jiji la Mwanza, Mkurugenzi wa Jiji na maafisa ardhi nao hawajachelewa kuwapa wapinzani ajenda.

Kuna habari kwamba Jiji la mwanza limeuza nyumba zake katikati ya Jiji kwa bei ya kutupa, bila kufuata taratibu.

Maeneo hayo yameuzwa wakati machinga mjini hawana maeneo ya biashara, wameenda kutupwa igoma nyamongolo huko ambako hakuna wateja, na kiloleli, na bila kuzingatia maelekezo ya Rais ya ubia kati ya sekta binafsi na Serikali, kiasi kwamba wangeongea na taasisi yoyote ile au mtu binafsi, akawekeza, wakawa wanakula faida, na eneo likabali lao.

Ni kwamba, wanamwanza wameibiwa.

Stanslaus Mabula, wewe ndio mbunge wa Nyamagana, bila shaka unalijua Jimbo linakuwaga la moto, hasa ukizingatia "sponsor kafa".

Angelina Mabula, wewe ndio Waziri wa hiyo ardhi ya serikali iliyouzwa, na uhamishaji miliki usingefanyika bila kupitia Ofisi za ardhi. Na sijui kwa nini kama mamlaka ya serikali inapotaka kuuza ardhi isitakiwe kupata Kibali Cha Waziri wa Ardhi au Waziri Mkuu! Au Rais! Uwepo udhibiti.

Mna kazi moja tu, kuirudisha ardhi hiyo, hatutaki Rais aanze kupata shida kupata kura za Mwanza wakati alishanyoosha mapito yake kwa miradi mikubwa ya maendeleo.

Ni hapohapo mwanza machinga aliyekuwa anauza ndizi, Jiji lilimwaga ndizi zake na kumpiga, Leo Jiji Lina ardhi hapohapo katikati ya mji linaiuza!

Njia moja tu, kurejesha hizo nyumba, na Kila Afisa aliyehusika apelekwe mahakamani, wanamwanza wataridhika wakiwaona wahusika wanapanda kizimbani, na kupelekwa gereza la Butimba.
huyu mama hafai alipata kwa nguvu ya jiwe
 
Back
Top Bottom